Na Deogratius Temba
UTARATIBU wa kuagiza mafuta kwa pamoja nchini kwa kutumia mfumo wa Bulk Procurement, uliokuwa ukipingwa na makampuni ya kuuza mafuta sasa utaanza kutekelezwa kuanzia Septemba mwaka huu.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza kufungua semina ya wadau wa mafuta nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, amesema pamoja na kuchelewa kutekelezwa kwa utaratibu huo sasa utaanza rasmi kutekelezwa baada ya miezi sita ijayo.
“ Baada ya kukaa na wadau hawa tumependekeza utaratibu mpya uanze kutekelezwa baada ya miezi sita yaani mwezi septemba mwaka huu, bila shaka sasa tutakuwa tumeongeza udhibiti wa biashara ya mafuta nchini, na kuongeza faida,” alisema Waziri Ngeleja.
Waziri Ngeleja alisema kikubwa kinachotafutwa hapo ni kupata bidhaa hiyo kwa bei nzuri ya ushindani ili kuondoa kabis a ukiritimba kweneye biashara ya mafuta na kumfanya mlaji asiumie.
“Wapo wafanyabiashara ambao wanalalamikia kuwa bei ya mafuta ni kubwa, na kuamua kupandisha bei sasa hawataweza tena kwani bei itajulikana wazi wazi ikutokana na muingizaji wa mafuta kuwa mmoja,” alisema
Alisema utaratibu huo utaongeza uwazi, kudhibiti mapato ya serikali, na kuongeza ubora wa mafuta kutokana na chanzo kuwa kimoja.
Waziri alisema pamoja na mfumo huo kuwa na takwimu sahihi, kutakuwepo na adhabu kali kwa wafanyabishara wa mafuta watakaokiuka taratibu ikiwemo kulipa faini y a sh. sh. Milioni 10, kufutiwa leseni na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya mafuta nchini(TAOMAC), Salum Bisarara, alisema umoja wao unahitlafiana na mpango huo wa EWURA na Serikali katika upande wa namna utakavyotekelezwa.
Bisarara alisema TAOMAC imependekeza kuwepo na boya kubwa la kutega nanga meli za mafuta la kuegesha meli kubwa yenye uwezo wa zaidi ya tani 35,000, ambao Mamlaka ya Bandari(TPA) wameanza kulijenga.
“Sisi tulishauri utaratibu huu uchelewe angalau kwa mwaka mmoja ujao, ili boya linalojengwa na TPA likamilike na meli kubwa ya mafuta iweze kuegeshwa hapo, kwa sasa linatumika ambalo haliwezi kuchukua meli kubwa ambalo lipo kule KOJ,” alisemea Bisarara.
Awali Bisarara alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na Ewura imeonyesha kutokuitambua TAOMAC katika mpango huo na inawezekana ukikamilika wasipate nafasi yao kama wadau muhimu wa bidhaa hiyo.
Alisema kitu cha muhimu ni kuangalia kuwa suala hilo linagusa biashara za watu, kwahiyo ni kungalia na maslahi ya wadau muhimu ambao wapo kwenye biashara husika ili wasifilisike.
Mwisho.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment