Popular Posts

Friday, March 5, 2010

Kakobe kumalizana na serikali wiki ijayo

Na Deogratius Temba

MGOGORO kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na waumini wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, kuhusu kupitisha njia ya umeme wa msongo wa Kilovoti 132 mbele ya kanisa hilo, unatarajiwa kufikia ukiongoni wiki ijayo baada ya wadau wa pande zote kukutana kati ya leo na kesho.

Akiungumza jana na waandishi wa habari Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja, alisema juzi alipokea taarifa kamili ya kitaalamu kutoka kampuni ya Bico ambapo jana hiyo hiyo aliwasiliana na wadau wengine wanaohusika akiwepo askofu wa Kanisa hilo, Zachary Kakobe, ili waijadili kwa pamoja na hatmaye kufikia muafaka wa suala hilo.

“Suala hili litamalizika kwa amani na hatutashindwana, leo (jana) nitaenda kuwasiliana na wadau wengine wanaohusika, tutakutana na kuchambua ripoti hiyo mpya ya Bico na askofu Kakobe akiwepo, na baadaye tutafikia muafaka na kutoa taarifa kwa wananchi,” alisema Waziri Ngeleja.

Waziri alisema mahali walipofikia kuhusu suala hilo, ni wadau wanasubiriwa kukutana ili kushirikishana kile kilichopendekezwa na Bico, ili kutafuta suluhu ya suala hilo.

Alisema taarifa ya Bico ya awali mbayo ilipingwa na Askofu Kakobe, mwenye na waamini wake ilikuwa ni rasimu tu ripoti kamili ni hiyo aliyoipokea jana ambayo itajadiliwa pamoja na mapendekezo yaliyokuwa yametolea na wadau kwa maandishi ambayo tayari yaliwasilishwa ofisini kwake wiki mbili zilizopita.

“ Kama milivyosiki wiki mbili zilizopita wadau wote waliwasilisha ripoti zao, na Kakobe mwenyewe naye alitaka ya kwake, tulikuwa tukisubiri hii ya Bico, imefika sasa mchakato wa kutafuta ufumbuzi una anza,” alisema

Akizungumzia suala la kuhamishwa kwa mfanyakazi aliyekuwa Katibu mhutasi wa Wizara hiyo Doroth Mtweve, anayedaiwa kuwa muumini wa kanisa hilo, Waziri Ngeleja alisema uhamisho huo ni wa kawaida na umefanywa katika wizara nyingine zote.

“ Nimeshangaa suala la uhamisho kuhusishwa na mgogoro huu, halihusiani kabisa, na tena sisi hatujui kama huyo dada ni muumini wa kanisa hilo, fanyeni uchunguzi, Wizara zote zimefanya mabadiliko ya wafanyakazi wake wizara na wengine wameenda mikoani katika idara mbalimbali, na katika wizara yetu wamehamishwa wengi tu siyo huyo pekee,” alisema

Muumini huyo aliyekuwa Katibu ya Wizara alikabidhiwa barua hiyo Februari 22 mwaka huu na Katibu Mkuu wa Wizara, akitakiwa kuhamia ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki.
mwisho

No comments:

Post a Comment