Popular Posts

Friday, September 9, 2011

Co-trimoxazole na ARVs kupunguza vifo

KAMPALA Uganda
Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), zinaweza kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa asilimia 50.
Co-trimoxazole ni mchanganyiko wa aina mbili za dawa ambazo ni trimethoprim na sulfamethoxazole, imekuwa ikitibu magonjwa mengi kama vile kifua, kuua bacteria wanausababisha magonjwa kama alimonia, bakteria wa mkojo, masikio na kutibu magonjwa ya kuhara.
Utafiti uliofanywa na Jarida la Kisayansi la The Lancent umebainisha kuwa dawa hizo ambazo mgonjwa hupewa mara baada ya kuonekana ameathirika na kinga za mwili (CD4) kupungua zinaweza kuokoa maisha ya mgonjwa au kupunguza vifo hivyo.
"Tumefanya utafiti kwa kumtumia mgonjwa ambaye alikuwa akianza kupata matibabu ya VVU kwa mara ya kwanza, akatumia Co- Trimoxazole, ameonyesha kuwa na uwezo wa kuishi muda mrefu na vifo vinavyotokea kwa watu kama hao ni vichache wakati kwa wale wanaotumia dawa za ARVs pekee wanauwezekano wa kupoteza maisha yao mapema zaidi,” alisema Profesa Diana Gibb, kutoka Baraza la Utafiti wa Madawa la Uingereza (MRC), alipozungumza na Shirika la IRIN.
"Tunajua kuwa ARVs pekee yake inapunguza vifo kwa asilimia hata 90, ila kuwa kutumia dawa hiyo inapunguza zaidi

Utafiti wa kuangalia tu umeonesha kuwa washiriki wa kutoka 3,179, Uganda na Zibambwe waliotoka katika Shirika la Kushughulikia Maendeleo ya afya na Matibabu la Afrika (DART), uliendeshwa na MRC nchini Uganda na Zimbabwe kwa kilipindi cha miaka mitano. Washiriki wote walikuwa na CD4 chini ya 200, wakati utafiti ulipoanza.

Shirika la Afya la Umoja wa mataifa (WHO), limependekeza matumizi ya dawa za Co-trimoxazole, kwa waadhirika wa Ukimwi wenye chini ya CD4 350, hasa wale walio katika maeneo yanayopata malaria kwa urahisi.

Licha ya miongozo hiyo utafiti huu wa DART, matumizi ya dawa kali haufanani kwa nchi za Uganda na Zimbabwe.

"Co-trimoxazole hizi ni dawa za bei rahisi ni za kawada na zimetengenezwa katika nchi za afrika kwahiyo ni rahisi kuzipata na zimekuwa zikitumika kwa kiasi kikubwa kwa kutibu magonjwa kama Almonia

“Mbali na idadi hiyo ndogo ya wagonjwa waliofanyia utafiti umeonyesha mafanikio makubwa”, anasema Gibb, na kuongeza kuwa matumizi ya dawa kali(Ant-biotics) umepunguza pia kasi ya ugonjwa wa malaria ambao ni ugonjwa wa kikanda.

Utafiti umependekeza kuwa co-trimoxazole, zitumike angalau kwa wiki 72 kwa watu wazima wanaoanza kutumia ARVs Afrika.
Mwisho

21 comments:

  1. Shukrani sana lakini vipi kuhusu side effect ya hizo dawa kwa watumiaji wa kawaida HIV negative

    ReplyDelete
  2. Je inaonyesha kuwa wenye vvu watumie hii dawa

    ReplyDelete
  3. Kipimo kizuri cha HIV nitumie kipi

    ReplyDelete
  4. Umri wa miaka 18 na kuendelea anatakiwa atumie vindonge vingp?

    ReplyDelete