Uzembe, ufisadi unavyoangamiza Mapato ya taifa
*Wizara ya Mali Asili na Utalii inaibiwa
WAKATI sakata la ufisadi unaohusu kutafunwa kwa fedha za wafadhili ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii linaendelea kufukuta imebainika kuwa wizara hiyo inapoteza mabilioni ya fedha kila mwaka kwa uzembe wa viongozi wake wakuu.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwa baadhi ya wakubwa ndani ya wizara ambao wamekuwa wakifanya maamuzi yenye maslahi kwao ambayo yatalikosesha shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), zaidi ya shilingi bilioni 50, katika mwaka huu wa fedha.
Fedha hizo, zilikuwa zipatikane kutokana na mapendekezo ya bodi ya wadhamini ya Hifadhi za Taifa ya kutaka ada ya hoteli za kitalii zilizoko ndania ya hifadhi zipandishwe kutoka kiwango cha sasa cha asilimia zisizozidi 10 ya bei ya malazi na chakula kwa kila mtalii kiasi ambacho ni karibu dola za Kimarekani 10 hadi kufikia 25.
Kutokana na uamuzi wa kigogo mmoja ndani ya Wizara hiyo, TANAPA ambayo kwa mujibu wa mapendekezo hayo ilikuwa ikusanye zaidi ya shilingi bilioni 100 hadi mwisho wa mwaka huu wa fedha, sasa itaambulia bilioni 69.
Kwa kawaida mapato ya TANAPA yanatokana na ada mbalimbali kama ada ya kiingilio ndani ya hifadhi, ada ya kuweka mahema, ada ya kupanda mlima na ada ya hoteli kwa wageni wanaolala.
Uchunguzi zaidi umeonyesha kuwa ada nyingine zote ukiacha ambayo kigogo huyo amekataa kupandishwa zimepandishwa kwa asilimia kati ya 100 hadi 300 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Tofauti na ada nyingine ada za mahoteli hazijawahi kubadilishwa tangu zilipowekwa miaka ya mwazo ya 1990, licha gharama ya malazi katika hoteli hizo za kitalii kupanda mara kwa mara.
Hivi sasa watalii hulipa kati ya dola za kimarekani 150 hadi 1,000 kwa siku na kati ya hizo dola 10 hulipwa kwa TANAPA kama ada.
Habari kutoka ndani ya wizara zinasema hatua ya kigogo huyo,sio tu imewakatisha tamaa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya TANAPA, bali pia menejimenti na watumishi wa hifadhi kwa vile wameshindwa kukidhi mahijati na malengo yao kwa mujibu ya mipango na mikakati wa shirika hilo kongwe nchini.
Habari hizo zinaendelea kudai kwamba, mapendekezo ya Bodi ya wadhamini ya kupandishwa kwa ada za hoteli hizo pia yaliridhiwa na aliyekuwa waziri wa Mali Asili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, lakini baadaye alihamishwa wizara.
Habari zimeeleza kuwa kabla ya kutekeleza ombi hilo pia kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mali Asili na Mazingira, ilitoa maependekezo kama hayo, lakini kigogo huyo alikataa kuidhinisha mapendekezo hayo kwa kuzingatia masilahi yake binafsi badala ya masilahi ya taifa.
Pia imeelezwa kuwa inadaiwa kwamba, pamoja na TANAPA kuwa na sababu za msingi za kutaka ada hizo zipandishwe kigogo huyo alikataa mapendekezo ya wataalam wake na kuendelea kusikiliza wafanyabishara wakiokodi hoteli hizo.
“Inashangaza, mnaweka mipango leo, wale wafanyabiashara wakijua tu wanakimbilia kwa wizarani, mapendekezo yenu yanapuuzwa na wakubwa,”alisema mmoja wa wafanyakazi wa TANAPA bila kufafanua.
Licha ya ada hizo kuwa ziliwekwa zaidi ya miaka 15 iliyopita wenye mahoteli wamefanya mabadiliko ya kiwango cha malazi zaidi ya mara tatu kiwango kilichopitishwa na kigogo huyo ni cha kuifanya Tanzania iendelee mapato ambayo ni mabilioni ya fedha.
Baadhi ya watumishi ndani ya wizara ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, wamesema kwamba tabia ya vigogo kufanya maamuzi kwa masilahi binafsi imeshamiri hivi sasa na madhara yake ni kama ilivyotokea hivi karibuni shirika hilo la hifadhi kushindwa kujiendesha kwa sababu za ukosefu wa fedha.
‘Sio kweli kwamba matatizo ya mwaka huu ya TANAPA yametokana na mtikisiko wa uchumi duniani, kama ilivyodaiwa na uongozi wa wizara, hii inatokana na uroho wa baadhi ya vigogo wa kufanya maamuzi mabaya,”aliongeza Mafanyakazi huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambavyo Tanzania daima, ilifanikiwa kuviona, hadi serikali ya awamu ya tatu inaondoka madarakani shirika hilo lilikuwa na akiba benki ya dola za marekani zisizopungua milioni 20.
Kutokana na kulikosesha shirika hilo kiasi hicho kikubwa cha pesa shirika sasa limeshindwa kuboresha huduma kwa watumishi wake na hususani askari wanaothibiti ujangili ambao ndio uti wa mgongo wa kazi za uhifadhii na kupelekea kushamiri kwa ujangili.
Aidha, shirika limeshindwa kuboresha huduma mbambali ndani ya hifadhi ikiwa pamoja ya ukarabati wa mara kwa mara wa miundo mbinu hasa mabarabara kwa ajili ya utalii.
Chanzo chetu kutoka ndani ya TANAPA kimeeleza kuwa hali ya kifedha ndani ya shrika hilo kwa sasa ni mbaya kiasi ambacho watumishi wametishia kugoma endapo masilahi yao hayataboreshwa.
Pia,wachunguzi wa masuala ya uhifadhi wanadai kwamba hali hiyo huenda ndio imepelekea Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Gerald Bigurube, kuandika barua ya kutaka kustaafu kabla ya kikomo chake cha ajira kufika.
Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Wizara hiyo, Bigurube, tayari amemwandikia rais Jakaya Kikwete, barua akiomba kustaafu Juni 30, mwaka huu na kukubaliwa, akieleza kuwa anataka kufanya shughuli zake binafsi.
Taarifa zimeeleza kuwa Mkurugenzi huyo ameamua kustaafu kutokana na wizara kutotoa ushirikiano kwa menejementi ya mashirika yaliyochini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na ubabe wa baadhi ya vigogo.
Habari zilizopatikana kutoka Arusha zimeeleza kuwa Wafanyakazi wa TANAPA, wanampango wa kugoma muda wowote kuanzia sasa kutokana na kuishi maisha ya shinda wakati uongozi wa Hifadhi ukisema kuwa hauna fedha.
Tanapa, inasimamia Hifadhi tano ambazo ni Tarangire, Serengeti, Ngorongoro, Manyara na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment