Popular Posts

Sunday, May 10, 2009

Tumewajiwa mafisadi, tuwakamate sasa

NI wazi kuwa tunaposikia watu wakisema taifa limefikia pabaya kuna ukweli ndani yake, hakuna ubishi kuhusiana na hilo, hata kama wengine wataendelea kukataa au kupinga lakini ukweli unabakia ukuwa ukweli.

Maandiko matakatifu yanatuambia kuwa ukweli utatuweka huru, kama tutakubali kuwa wakweli daima hatutakuwa watumwa wa watu wengine, tutakuwa huru kifikra na kiuchumi.

Ni ukweli taifa limefika pabaya, hayo yameandikwa na yamesemwa na wengi, na waliolifikisha taifa hapa ni watanzania wachache kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza hasa wasio na nia nzuri huku wengine wakifanya hivyo kwa kulazimishwa au kutokujua.

Kwanini ninasema hivyo?, hali inayoanza kujiotokeza ya baadhi ya watu kushambiliana hadharani ina madhara makubwa na haina maslahi kwa taifa hasa kwa mwananchi masikini aliyeko kijijini, ila inaonekana kuna tabia imejengeka miongoni mwa watu kutumia mwanya wa suala la ufisadi, rushwa na mambo mengine machafu yanayotokea nchini kujinufaisha kisiasa na kutafuta umaarufu.

Watu wanataka wazungumze waonekane, wasikike , wanataka vyombo vya habari vitumie muda mwingi kutoa yale ambayo wanayasema hata kama hayana maslai kwa taifa, huko ni kuwalisha wananchi yale wasiyoyahitaji.

Binafsi sina raha kutokana na hilo, na ninasema itafikia mahali waandishi watawagomea baadhi ya wanasiasa, hakuna haja ya kupoteza muda na baadhi ya watu, kama taifa hili litaangamia, kwasababu ya ktumia muda mwingi kuwapa hawa watu nafasi, dhambi hii itawatafuna waandishi wa habari.

Mwanzoni mwa wiki, Mwenyekiti, Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, alitoa masimamo wake juu ya suala la ufisadi na rushwa linaloendelea hapa nchini, aliwataja anaowajua.

Kauli ya mengi, haikuwafurahisha wengi, ni kweli kuwa ukitajwa huwezi kufurahia, unachafuka vibaya mno, na pia ukweli unauma.

Aidha, marafiki na maswahiba wa wanaotajwa huwa hawana furaha, hujisikia kama kitumbua chao kinaingia mchanga, maana kama “boss” au rafiki yako wa karibu ni fisadi na anakusaidia ukisikia anatajwa ni lazima uamshe chuki juu ya aliyemtaja.

Chuki imesambaa , sasa watanzania wachache wasiozidi 500 wanataka kuwagawa watu milioni 38, kwa sababu tu, watu wao wanatajwa au wao wenyewe watahusishwa na ua=chafu huo.
Hawafurahii, kwa watu kusimama na kuwataja watu wachafu, wala rushwa, mafisadi walioliingizia taifa hili hasara ya mabilioni ya fedha.

Kundi hili halitaki kuangalia tulikotoka, wala tuliko sasa na wajiulize ni kitu gani kimetufanya tukawa hapa? Ni kwanini tumekwama kwa kila sekta? Ni kwanini Nchi ina fedha nyingi, ina rasmali nyingi, ina pata misaada mingi kutoka nje ya nchi na jumuiya za kimataifa zinasaidia lakini hatupigi hatua kimaisha, bqado tunajiita masikini?

Hawa watu hawataki kujiuliza, ni kwanini nchi imejaa watu masikini, kila kukikucha umasikini unaongezeka, vifo vya watanzania wanaopoteza maisha yao kwa kukosa dawa hospitalini, mama wajawazito na watoto wachanga wanavyokufa kwa kudaiwa fedha au kukosa huduma za msingi za afya kutokana na misaada inayotolewa kubebwa na kundi la wachache.

Hatuoni watu wachache wanavyomiliki rundo la mabilioni ya fedha, hata kutishia uhuru wa mahakama zetu?, hautoni jinsi mtu mmoja anavyoweze kutoa fedha nyingi pale mahakama ya Kisutu ili adhaminiwe?, kazipata wapi?.

Leo hii Mengi, anapotaja mafisadi, hatutaki kuuliza kama amewataja serikali imewachukulia hatua gani?, je hivi tunafikiri kuwa Mengi alikwenda kuwataja watu mbao serikali haina taarifa nao?, alizungumza lakini bila shaka taarifa zipo Ikulu kuhusu watu hao, Taasisi ya Kuthibiti na Kuzuia na Rushwa (TAKUKURU) wana taarifa zao usalaama wa taifa wanajua, lakini wamenyamazia, mwananchi wa kawaida kaamua kuwaanika, tunamwona mwehu!.

Hoja ni kwamba, ni kwanini kumeibuka makubndi ya watanzania ambao hawafurahii kauli za Mengi, ukiachia mbali wale waliotajwa na familia zao ambao ni lazima wachukie?

Hili kundi, la wanasiasa, viongozi wa serikali linalokasirishwa na hatua hiyo, badala ya kupongeza linatoka taifa lipi?, je hatuoni kuwa linataka kutugawa ? ni kundi dogo lenye sumu kali inayosambazwa na fedha, linafanikiwa kwa kasi ya ajabu, watanzania tuwe macho.

Sitaki makala yangu umkasirishe mtu, ila kila mtu afungue macho yake aone hali ilivyo, na atafute hukumu mwenyewe, tunakila sababu ya kuwa macho na watu hawa, hebu tufikiri, na kutafakari, labda, baadhi ya watu wamekuwa wakijikia vibaya kwasababu wana nmamlaka ya kuwakamata mafisadi, na wameshindwa kufanya hivyo? Sasa wanaona aibu kwa uzembe na lawama inayowaangukia?.

Ni lazima tujiamini na kusimama imara katika kutetea rasimali za taifa hili, tupate watu watakao jitoa muhanga, hatumbembelezi mtu, kama unaona ukitajwa unaumia sana, basi kimbia nchi, au acha, kabisa kupokonya mali za watanzania, na pia kujisafisha omba msahamha na kurrudisha kile ulichokichukua.

Pia kuna haja ya kujiuliza kama wewe umekuwa ukiitwa fisadi kila mara ina maana kweli kati ya watu milioni 38 au 40, unaonekana wewe tu? Jiulize kuna nini, unatakuiwa kubadilika tu, jiulize hivi kwanini watu wananichukia kiasi hiki?,

Je ni kwanini ni wewe tu?, tuhuma zikikuandama kuna jambo, nawashauri wahusika wajitahidi kubadilika, au kujirekebisha ili majina yaio yasiendelee kutajwa kila mwaka, anagalao tuwasahahu tumechoka kusikia kila siku gulani katajwa kwelye hili, kesho tena anatajwa, hii ni hatari.


Ninasema hivyo kwasabu inawezekana baadhi ya watu hawakamatiki tena, wameshakua tembo, ni wakubwa, wanaogopeka na dola, serikali inawaona kama mioyo yao, pamoja na kuwa ni wachafu, hapo tunahitaji watu jasiri, kama walivyofanya wabunge wetu wa kambi ya upinzania, wakawaanika hadharani Septemba 2007, pale Mwembeyanga, Temeke.

Tuliko fikia ni mwisho, tunataka watanzania wenye nia ya kujitoa sadaka kwaajili ya kuteeta maslahi ya taifa ambayo yanaangukia kwa wengi.

Nawatakia watanzania safari njema ya kupambana na ufisadi , hali ni ngumu lakini Kwa neema za mwenyezi Mungu tutafika, tupo wengi tunaopigania haki ni lazima tupate haki yetu, wachache hawataki haki lakini wengi waanaitaka, “wengi wape”.
0784 / 715-686575

No comments:

Post a Comment