Popular Posts

Friday, September 9, 2011

Rais Kikwete, watajie Polisi wauza dawa za kulevya

Na Deogratius Temba
KATIKA moja ya kesi ngumu za jinai zinazohitaji upelelezi na ushahidi wa uhakika na udhibiti ni dawa za kulevya. Dawa za kulevya sinatakiwa zidhibitiwe siziingie wala kutoka. Na udhibiti wake ni kwa njia za nchi kavu, angani, na majini.
Ukiwauliza Polisi wanakuambia kuwa wanajitahidi kulinda mipaka na njia zote husika kuhakikisha dawa haziingii wala kutoka. Tangu alipoingia madarakani Rais Kikwete mwaka 2005, amekuwa akitamka waziwazi kuwa tatizo la dawa za kulevya ni nzito na linawasumbua hata yeye na wenzake.
Lakini cha kushangaza kwa kipindi kifupi rais amekuwa akitangaza kuwa anayo majina ya wauza unga (madawa ya kulenya) lakini hawataji. Wakati huo huo tunajua wazi wazi kuwa kumjua na mtuhumiwa wa kosa la jinai ukakaa kimya ni kosa la jinai au kumficha mtuhumiwa asikamatwe wakati anatafutwa ni kosa. Kwa hiyo hapa rais wetu yupo juu ya sheria? Kwanini asiwakamate? Kwanini asiwaelekeze polisi wawakamate wauza unga, kwa lugha hizo ina maana anajua wanavyo safari na kurudi wakiwa na mzigo(madawa) lakini hawakamatwi.
Cha kushtua zaidi rais wiki iliyopita ametamka tena mbele ya viongozi wa dini kuwa anawafahamu viongozi wa dini wanaouza unga, hakuwataja wala kusema ni kiongozi yupi au wa dini gani. Rais Kikwete analalamika badala ya kuchukuwa hatua? Tujiulize tatizo la rais wetu ni nini? Biashara ya madawa ya kulevya ni kosa, na sii kwamba sheria zipo? Sasa analalamika na Nani anatakiwa kulishughulikia hili. Rais anatamka mambo ya dawa za kulevya hadharani bila kuwa muwazi wakati huu ambapo kuna wasiwasi mkubwa wa wanasiasa wengi wakilalamika kuwa wanaandamwa na baadhi ya kundi la watu linalojulikana kama mtandao wa mafisadi ili wawekee dawa za kulvya. Wanaolalamika kutaka kuwekewa dawa ni makada wa CCM, ambao wanadai kuwa makada wenzao wanataka kuwabambikizia mzigo huo. Tayari baadhi ya wanasiasa kama Mbunge wa Kinondoni Idd Hassan, amesharipoti kutaka kuwekewa dawa za kulevya, hakuna hatua za haraka zilizochukuliwa na wahusika hata Jeshi la polisi kufuatilia. Wamepuuza huku Mkuu wa nchi akisema kuwa anawafahamu wauza unga.
Mwaka jana, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi alitoa taarifa ya wazi kuwa kundi la wanaCCM wenzake aliloliita matajiri kwa kushirikiana na vigogo wa Jeshi la Polisi walitaka kumwekea Mtoto wake dawa za kulevya. Serikali, Ikulu, Tume ya kudhibiti dawa za Kulevya, Ofisi ya Waziri Mkuu, Usalama wa Taifa, walisikia hawakuchukua hatua hadi leo.
Mengi alihitimisha taarifa yake kwa kusema yupo tayari kulisaidia jeshi la polisi au kuhojiwa lakini hakuhojiwa na hadi leo, vigogo watuhumiwa wanaendelea na kazi zao, hawakumshitaki Mengi kwa kuwakashfu na kuwachafulia majina, wala serikali inayojidai kupambana na dawa hizo haramu haikuchukua hatua. Je hii sii kusema kuwa tunaongozwa na serikali yenye makosa? Isiyo heshimu hata sheria zake yenyewe?
Rais wa nchi, hana uhakika na maelezo yake, jeshi la polisi halina uwezo wa kumhohi wala kumuuliza kwasababu anawateua wakuu wa Jeshi hilo, Takukuru, usalama wa taifa, na vyombo vingine vinamwogopa, kwasababu yeye ndiye bosi wao ndio maana tunataka mabadiliko ya katiba haraka ili tumpunguzie Rais madaraka.
Kama sii katiba yenye mapungufu tuliyonayto leo, rais angeweza kuhojiwa na chombo cha usalama na kueleza majina ya waunza unga, au viongozi wa dini wanaousa unga kwa sababu amesema anawafahamu. Ninamshauri rais Kikwete awe makini na maelezo yake ambayo yanaleta utata!!!!!!
Tutaendelea wiki ijayo…deojkt@yahoo.com, 0715686575

No comments:

Post a Comment