Na Deogratius Temba
KATIKA Mfululizo na mwendelezo wa ripoti hii ya ziara ya viongozi wa dini waliofanya katika migodi ya madini nchini, wiki iliyopita tulimalizia na kuangalia sehemu ya tadhimini ya fidia ya mali ambapo, viongozi hao katika ziara yao hiyo waliangalia jinsi ambavyo fidia katika baadhi ya sehemu imepunjwa na wananchi wamebaki wakilalamika.
Leo tunaangalia viongozi hao wana tia maoni gani juu ya usalama wa raia na mali zao katika maeneo ya migodi ili kulinda utu na ubidamu kwanza kabla ya kupata mali au madini.
Hali inavyoonekana Geita
Mazungumzo kati ya viongozi wa dini na wahanga huko Geita yalikuwa hivi: “Tuliondolewa katika maeneo yetu usiku wa manane na wakala wa mahakama, akisaidiwa na polisi na kutolewa nje ya nyumba zetu. hatukupewa hata muda w a kuchukua vitu vyetu. tuliamriwa kupanda malori yaliyokuwa nje huku mizigo yetu ikifungwa na watu tusiowajua , wengine walipora vitu vyetu wakati wakifunga. tulipoteza vitu vingi pamoja na haki ya kuvimiliki.
Tulikwisha vuna kahawa mashambani tayari kwa kuuza, tulipoteza kuku, nguo na vyombo vya ndani. kinacho tuumiza zaidi ni kwamba walifukia hata kahawa yetu tuliyovuna ambayo kama tungeiuza tungepata fedha za kununulia chakula cha watoto wetu”.
Kwa bahati mbaya watu hawa waliondoka bila chochote walichokuwa wanakimiliki, zaidi ya hayo wanalaumiwa kwa kupinga maendeleo ya uwekezaji katika sekta ya madini. mmoja wao alipokuwa akitueleza malalamiko yake alionekana kushangaa “ tuinaishi katika hali ngumu, hatuna maji, hatuna vyoo, tuna watoto 25 hapa wanasoma watoto wachanga na wazee kwanini serikali inatufanyia yote haya?
“Na je sisi ni watu wake wakati wa uchaguzi tu?tunaitaka serikali ije kutusaidia. Tunaiomba serikali ije kutuisaidia na itueleze kama wizara ya sheria imegeuka kuwa wizara ya ukiukwaji wa sheria, lakini pia tunataka kujua ni kwanini tunaghafilika?
Ujumbe wa viongozi wa dini pia ulikuwa na swali linalofanana na hilo, inawezekana je kudhalilishwa vile kwa wananachi? hasa katika suala nyeti la utu na hakazi binadamu kama hilo? hali hii ilileta uchungu na mshituko kama ilivyoainishwa na Askofu, Dk. Steven Munga, kwa kusema “ Sijawahi kuona katika maisha yangu mahakama ikighafilika; na hali ya mambo yanavyoonekana kuna mchezo mchafu uliosababisha maamuzi hayo yaliyosababisha maisha ya kaka na dada zetu kuwa magumu,”anasema Baba askofu.
Sheikh Fereji, wa Bakwata Mkoa wa Mwanza, alimshauri Mkuu wa Wilaya ya Geita kwamba “Yote yaliyotokea yamewaathiri vibaya wananchi wa kijiji cha Mtakuja. Hawa ni watu wako wa wilaya ya Geita, nakuomba uwasaidie. Jitahidi kufanya kila uwezalo kuwasaidia maji safi na mahitaji mengine wakati maamuzi ya mahakama yakisubiriwa. Wewe ni mwakilishi wa serikali wa hapa na ni serikali hiyo hiyo iliyowaondoa watu hawa katika maeneo yao. Watazame watoto, ingekuwaje kama wangekuwa wa kwako?
Hali ilivyoonekana North Mara
Wakati ujumbe uliotembelea Nyamongo, watu waliulalamikia mfumo uliopo wa uongozi na kampuni. “Ni miaka 14 sasa tangu shughuli za uchimbaji zianze Nyamongo na North Mara. Wachimbaji wadogowadogo wamekuwa wakipata fedha katika machimbo haya kwaajili ya kujikimu katika mahitaji yao.
Wawekezaji waliahidi kuboresha huduma za kijamii na kujenga uhusiano mzuri lakini hii haikufanyika kwani hakuna mahusino mazuri hakuna maji safi na salama hakuna umeme kuzunguka vijiji hivi na hakuna ajira kwa vijana. Hakuna soko kwa mazao yetu (wao huagiza nyama , mbogamboga kutoka nje) vipande vya mawe vinaonekana kuzunguka maeneo haya, kuna uchafuzi wa hewa na harufu ya kemikali.....”
“Tafadhali fikisheni malalamiko yetu kwa rais “ alisema mmoja wa wanakijiji.
Hali ya kutoridhika katika maeneo ya migodi inaonyesha kuwa kama matatizo haya hayatatuliwa kwa busara yanaweza kuwa chanzo cha vurugu. kama alivyosema Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mgogoro wa dhahabu Geita mbele ya wajumbe wa kamati ya viongozi wa dini, serikali ilielezwa vya kutosha kuwa hilo lilikuwa sawa na bomu linalosubiri muda wa kulipuka.
Mwanafalsafa Mtakatifu Augustine amesema : “Hisani haiwezi kuwa mbadala wa haki iliyonyakuliwa au haki iliyonyakuliwa haiwezi kufidiwa kwa hisani”.
Wiki ijayo tunaendelea na sehemu ya saba ambayo tunaangalia uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment