Ukata wa fedha wakwamisha mradi wa kusambaza gesi Dar
*Mapato ya gesi kwasasa yanalipa deni la Songas
*Magari ya serikali kubadilishwa kutumia gesi
Na Deogratius Temba
MRADI wa kusambaza gesi asilia katika kwa ajili ya matumizi ya majumbani jijini Dar es salaam, umekwama kutokana na ukosefu wa fedha baada ya mapato yanayotokana na mauzo ya gesi kulipa deni la kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Songas Limited, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa muda umabaini kuwa mradi huo ambao awamu ya kwanza ulizinduliwa mwezi Julai Mwaka jana na Waziri wa Nisahti na Madini, Wiliam Ngeleja, sasa umekwama kutokana na kukosekana kwa sh. Bilioni 3.5 kati ya 7 ambazo zimepangwa kutumika ili kukamilisha mradi huo.
Pamoja na mradi wa kusambaza gesi majumbani kukwama, ule wa kuhakikisha magari ya serikali yanageuzwa kutoka katika matumizi ya mafuta ya Petroli kwenda gesi nao unasua sua baada ya Wizara ya Miundombinu inayosimamia magari ya serikali kutokuonyesha nia ya kupeleka magari ya serikali kubadilishwa.
Shirika la maendeleo ya Petroli(TPDC) linalosimamia mradi huyo kwa niaba ya serikali limejikuta likiambulia mapato sifuri baada ya tumia kidogo kinachopatikana kumlipa mbia mwenza Songas ambaye alitoa mtaji wa kuasisi mradi huo.
Alipoulizwa Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha juu ya kukwama kwa mradi huo alisema waulizwe TPDC kwani wao ndiyo wanaousimamia na wanafanya biashara ya gesi, kwahiyo wanatakiwa kutumia fedha wanazopata kuuendesha mradi.
“Hilo ni suala la TPDC ninachojua ni kwamba wanafanya kazi hiyo kw a ushirikiano na Pan African Energy, na wanauza gesi kwa sasa. Muulize mtu anaitwa Kilangani wa TPDC atakusaidia,” alisema Tesha.
Ofisa Mtafiti mwandamizi na Maendeleo ya miradi wa TPDC, Charles Sangweni, aliliambia gazeti hili ofisini kwake kuwa kukwama kwa mradi huo kunatokana nsa kukosekana kwa kiasi hicho cha sh. bilioni 3 baada ya mapato yanayotokana na mauzo kulipa deni la Songas.
“Mradi hauwezi kuendelea kwasababu hatuna fedha, tunapouza gesi kwa sasa tunalipa deni TPDC haibakiwi na chochote. Kwa sasa TPDC inauza kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Energy, lakini mapato yanafidia deni la mtaji baada ya hapo kuna gharama za uendeshaji, asilimia 12 ni kulipa serikalini na kinachobaki kinagawanywa,’ alisema Sangweni.
Sangweni, alisema tayari kwa awamu ya kwanza, mradi huo umefanikiwa kutandaza bomba kubwa la kusambaza gesi katikati ya jiji, ujenzi wa vituo viwili vya kuhifadhia gesi, na viwili vya kushindilia.
Alisema mipango ya awali ni kuunganisha hoteli kubwa mbili za katikati ya jiji na taasisi sita. Nyingine ni nyumba 13 za TPDC zilizoko mikocheni, na kuhakikisha magari 200 yanabadilishwa kwa awamu ya kwanza.
Alisema kuwa kituo cha kujaza gesi kwenye magari kilichojengwa Ubungo maziwa, kitazinduliwa rasmi mwaka huu. Na tayari karakana mbili za kubadilisha magari kutoka kwenye mafuta kwenda gesi zimeshakamilika katika Chuo Kikuu cha Dar es slaam, kitendo cha ushauri wa ufundi(BICO) na taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam,(DIT).
Naye afisa uhusiano wa TPDC, Felix Haule, alisema mradi huo hauwezi kuendelea bila kuwa na fedha, kwasababu deni la zamani ni lazima lilipwe ndiyo faida iweze kuonekana.
“Ni kweli mradi umekwama, sababu ni kukosekana kwa fedha, kama hakuna fedha tutaendeleaje?, tunasubiri, lakini serikali nayo inachukua fedha zingebaki zingeweza kusaidia kuimarisha mradi ukaendelea,” alisema Haule.
Hivi karibuni Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, amesema usambazaji huo wa gesi asilia iliyoshindiliwa unatarajiwa kupunguza matumizi ya mkaa kwa Jiji la Dar es Salaam kutoka magunia 30,000 kwa siku sasa hadi kufikia magunia 15,000.
Mradi umepanga kubadili magari 8,000 ili yatumie gesi asilia. Faida zinazotokana na matumizi ya gesi asilia ni pamoja na kuokolewa kwa takribani shilingi bilioni 50 kwa mwaka ambazo zingetumika kununulia kuni, mkaa na petroli kwenye magari, kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu na uchafuzi wa mazingira.
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Energy inatekeleza awamu ya kwanza ya mradi huo ambayo itagharimu Dola za Marekani milioni tatu.
Baadhi ya maeneop yaliyoteuliwa kuanza kuufaidi mradi huo ni magereza ya Keko na Ukonga, hoteli kubwa za Southern Sun, Holiday Inn, Kilimanjaro Kempsinki, Movenpick, JKT Mgulani, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na nyumba 70 eneo la Mikocheni.
Mwisho.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment