Popular Posts

Sunday, January 17, 2010

Wawezaji Kilimanjaro chanzo cha migogoro ya maji,ardhi

*Mikataba yapitishwa bila kufuata taratibu
*waadhirika wakubwa ni wanawake,watoto
*maji yawa chanzo cha vurugu, kawaha yatelekezwa

Na Deogratius Temba

WAWEKEZAJI wa Mshamba ya kulima zao la Kahawa Mkoani Kilimanjaro, wamekuwa chanzo cha migogoro kati yao na wananchi wanaowazunguka kutokana na kushindwa kutekeleza masharti ya mikataba walioingia na vyama vya ushirika vya msingi na serikali.

Mashamba mengi yaliyobinafishwa au kukodoshwa kwa wawekezaji mkoani Kilimanjaro yanamilikiwa na vyama vya ushirika vya msingi vilivyokabidhiwa na serikali baada ya kuyataifisha kutoka kwa Wazungu mwaka wa 1971.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, mkoani Kilimanjaro kwa msaada wa asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Gemsat)kwa muda mrefu unabaini kuwa migogoro hiyo imepelekea kuibuka kwa vurugu ambazo zimesababisha uharibifu wa miundombinu na baadhi ya wananchi kukosa huduma za msingi.

Mgogoro wa maji
Kutokana na mwekezaji wa Shmba la Vasso Agriventure, kukiuka masharti ya mkataba kati yake na Chama cha Ushirika cha Kibosho kati( Kibosho Central) wakazi wa Kijiji cha Dakau Maembe, Kata ya Okaoni, Wilaya ya Moshi Vijijini, waliingia katika mgogoro na mwekezaji wakilalamika kupunjwa maji ya kutumia ya Mfereji wa Mure.

Tatizo katika kijiji hiki limeleta madhara mbayo wananchi wake wanayaeleza kama donda kwao kutokana na kukosa maji kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili mwaka jana. Migomba iliyokuwa imekauka kwa kukosa maji kipindi hicho matokeo yake yanaanza kuonekana kutokana na kukosa ndizi amabzo ni tegemeo kubwa kwa wananchi.

Wananchi wa kijiji hicho wanakiri sasa kuwa hali ya amani imeanza iliyokuwa imetoweka kipin di hicho sasa inaanza kurejea. Hii inatokana na mwekezaji kukubali kuwaachia vijana sita aliokuwa amewashitaki na kuwafungulia kesi ya jinai kwa kuharibu mabomba.

Pia wanasema kuwa amani inarejea kutokana na mvua kunyesha na maji kuongezeka ikiwa ni pamoja na kukarabatiwa kwa mabomba yaliyovunjwa kutokana na hasira ya wananchi baada ya mwekezaji kuwanyima maji.

Vurugu zilisababishwa na nani?
Mkurugenzi wa Shamba hilo, Fons Nijenihuis anakiri kuwepo kwa tatizo hilo, mwaka jana na kusema kuwa tatizo ni maji. Anaeleza kuwa wananchi nmdio wana makosa kwasababu wanavamia miundombinu yake na kuiharibu.

Pia anasema kuwa tayari anayo hati miliki ya maji hayo, aliyopewa wakati akikodishiwa shamba hilo, hati namba 3350.

Hata hivyo anakiri kuwepo kwa mapungufu ya kisheria katika sheria ya maji inayotumika ya mwaka 1959, kifungu cha 16.

Kwanini migogoro itokee?, uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya vyama vya msingi vimeingia mikataba na wawekezaji wasiokuwa na mitaji ya kutosha kuweza kufufua na kuendeleza zao la Kahawa.

Aidha baadhi ya wawekezaji hawalipi kodi ya pango la ardhi, kulingana na mkataba wa uwekezaji. Na mikataba hiyo imefanyika haraka bila kuangalia madhara yake wakati wa utekelezaji hasa matumizi ya rasimali kama maji, na miundombinu ya barabara.

Pia wawekezaji wengine wanakodisha mashamba hayo kwa wafanyabishara wengine badala ya wao wenyewe kuyafufua na kupelekea kutumika kulima mahindi, Alizeti na Maharagwe.

Hali kadhalika wawekezaji wasio na uwezo kimtaji wameanzisha migogoro na wamiliki wa mashamba au wananchi kwa lengo la kufungua kesi mahakamani ili wapate nafasi ya kuendesha mashamba hayo kwa muda mrefu bila kulipa kodi wakati kesi ikiwa mahakamani.

Udhaifu wa mikataba Kilimanjaro
Wawekezaji waliopewa mashamba hawana mitaji ya kutosha kuweza kufufa zao la kahawa na kuliendeleza,baadhi ya wawekezaji wanatakiwa kulipa kodi ya kodisho wengi wao hawalipi.

Wawekezaji wengi hawatoi mipango yao ya kuendeleza shamba (development plans) kw a wamiliki wa shamba japo ni sharti moja wapo mlilioainishwa kwenye miktaba na kufanya wamiliki kushindwqa kufatilia mashamba.

Wawekezaji wasio waaminifu wameanzisha migogoro na wenye mashamba. Wajummbe walioko kwenye kamagti ya kusimamia mali za vyama vya ushirika hawana elimu ya kutiosha kuelewa mikataba, mawakili wa wawekezaji wamekuwa wakifaidi kutokana na kutyokumba na changamoto yoyote.

Uchunguzi umeonyesha kuwa hata utaratibu uliotumika kumpitisha mwekezaji huyo ulikuwa wakupiga kura za wajumbe wa Chama cha Msingi kusimama upande wa mwekezaji wanayemtaka.

Mapema mwaka jana mgogoro wa kugombania maji kati ya mwekezaji na wananchi wa kitongoji cha Maembe Dakau, uliibuka na kupelekea uharibifu mkubwa wa mazao yaliyokauka kutokana na kukosa maji.

Mrajisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kasya Kasya, anakiri kuwepo kwa migogoro hiyo na kusema kuwa tayari ofisi yake inaishughulikia ile iliyoripotiwa kwake ikiwa ni pamoja na kushauri baadhi ya mikataba ivunjwe na mashamba kurudishwa kwa wamiliki.

“Tulipopata taarifa za migogoro hiyo, tuliunda kamati ya kupitia mashamba yote ambayo ilituletea mapendekezo ambapo tumeshauri mikataba yote ya mashamba ipitiwe upya ikiwa ni pamoja na kuivunja ile inayoonekana kuwa na utata.

“Tatizo lingine ni kuwa wajumbe wa vyama vya msingi wanaokaa na kumpitisha mwekezaji hawana uelewa wa mikataba hiyo ambayo imeandaliwa kisheria, ina wapa mwanya mawakili wa wawekezaji kuisaini bila shida,’ anasema Kasya.

Wananchi walioadhirika
Nilitemmbelea kijiji hicho Mwezi Machi na nikarudi Desemba mwaka jana na kukutana na wananchi mbalimbali. Wengi wao wanakiri hali ilivyo kwa sasa kuwa imerekebika tu kwa muda kutokana na mvua kunyesha, lakini kama serikali haitaushughulikia mgogoro huo na kutafuta ufumbuzi mapema kiangazi kianza kuna uwezekano wa kuibuka tena.

Bado kilio kikubwa kwa serikali ni juu ya maji kupewa wawekezaji hasa yale ya mtoni ambayo kiasili ni wa wazawa wa eneo husika. Mfano kwa mfereji wa Mure imetoa hati miliki kwa mujibu wa sheria ya maji ya mwaka 1959.

Kwasababu hakuna maridhiano ya uhakika yaliyofanyika kati ya pande zote mbili, Wakazi hao wanahofu ya kuingia katika mgogoro mwingine na kuitaka serikali kutafuta vyanzo mbadala haraka.

Leopold Kimaro ni mjasiriamali wa kijiji hicho, ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa mstari wa mbele kutetea wenzake, anasema bado hali haijawa nzuri kwasababu, mvua zimenyesha, na hakuna tatizo kubwa la maji, mwekezaji anapata na wanakijiji wanapata, lakini mvua zikikatika maji hayatatosha.

Mathias Kimaro(71), ni mzee wa kijiji hicho, ambaye amekuwa mwenyekiti wa Mfereji wa Mure kwa kipindi kirefu anasema kwa uzoefu wake kijijini, anajua kuwa mifereji ya asili ni ya watu wote kwani ilitumika kwa wakazi hao kwa ajili ya kujipatia maji ya kunywa na kunyweshea mashamba yao ya kahawa na migomba.

Wanachi wanaeleza pia kuwa mkataba wa mwekezaji huo umezusha mgogoro kutokana na yeye kukataa kulima kahawa kama alivyotakiwa na kulima maua ambayo yanatumia maji kwa kiasi kikubwa.

Moris Makoyi, ni mjasiriamali mwenyeji wa kata hiyo, anashauri kupitiwa haraka kwa mkataba huo ili kuondoa vurugu, kwani kukiukwa kwa makubalino ya mkataba ndiyo kumesababisha mgogoro.

“Hapa migogoro haiwezi kuisha bila kuangalia upya mikataba kwani mwekezaji amevunja makubaliano, amelima maua leo hii wananchi wanaanza kugombania naye maji kwa sababu maua yanahitaji maji mengi na maji hamna hapo huwezi kukwepa vurugu, anasema Makoyi.

Pamoja na hao, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha msingi Kibosho Kati, Martin Mallya, anakiri kuwa mwekezaji analima mazao ambayo siyo waliokubaliana.
Mallya anaseme walikubaliana alime kahawa kwa asilimia 60 na asilimia 40 mazao mengine.

Bonde la mto pangani wanasemaje?
Ofisi ya Bonde la Mto Pangani ndiyo mamlaka iliyopewa jukumu na serikali la kusimamia vyanzo vya maji mkoani hapa, pamoja na kukubali kuwa maji hayo yanamilikiwa na mwekezaji, imeshauri serikali kutafuta njia mbadala ya kuuondoa mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na kuongeza vyanzo vya maji.

Afisa wa ofisi hiyo, Mhandisi, Philipo Patrick, anasema kuwa kinachotakiwa ni kuangalia kama mwekezaji ameomba kiasi gani cha maji na atumie hicho hicho bila kuhitaji zaidi ili kuondoa mgogoro wa maji katika kijiji hicho.

“Tunawashauri wakulima wakuwa wachukue maji kwenye ardhi waache kutumia haya ya vyanzo vya asili ambayo wananchi wanayahitaji,”anasema.

0784 686575
deojkt@yahoo.com
www.deotemmba.blogspot.com
Mwisho

No comments:

Post a Comment