Popular Posts

Sunday, May 10, 2009

SERIKALI KUMSULUBISHA MENGI LEO?

Serikali kumsulubisha Mengi leo?

FIsadi Subhash Patel naye iabuka na kusmea kuwa kachafuliwa na Mengi

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, John Mkuchika, amesema kuwa wizara yake leo itatoa msimamo wa serikali kuhusiana malumbano yaliyoibuka hivi karibuni baina ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Regnald Mengi na Mbunge wa Igunga (CCM), na mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz.

Mkuchika aliyasema hayo jana mjini Katoro, wilayani Geita katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao ulihusu zaidi kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mdogo wa ubunge, jimbo la Busanda.

Alisema hadi jana kauli ya serikali ilikuwa tayari imetayarishwa na itatolewa kwenye mkutano wa waandishi wa habari, utakaoitishwa leo na Naibu Waziri wa Wizara yake, Joel Bendera, jijini Dar es Salaam.

Wakati serikali ikitarajia kutoa tamko lake leo, tayari wafanyabiashara watatu wenye asili ya kiasia, kati ya watano waliotajwa wameshajitokeza na kujibu shutuma hizo hadharani.

Malumbano hayo yalianza pale Mengi alipoitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwataja wafanyabiashara watatu akiwemo Rostam, kwamba ni mafisadi papa wa nchi hii.

Mengi katika mkutano wake huo, aliwataja wafanyabiashra, Jeet Patel, Rostam Aziz, Yusuf Manji, Subhash Patel, na Tanil Sumaiya, ambao aliwatuhumu kuwa ndiyo mafisadi Papa wanaoliibia taifa mabilioni ya Fedha.

Wakwanza kujitokeza hadharani kujibu tuhuma hizo alikuwa Rostam, ambaye naye alimtuhumu Mengi kuwa ni fisadi Nyangumi, kwa kumuhusisha na kukopa pesa na kushindwa kuzirudisha katika Mpango wa kusaidia wafanyabishara (Commodity Import Support) na kuhusika kuifilisi iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Rostam, alikwenda mbali zaidi na kuwasilisha vilelezo vyake kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), na kudai kuwa atakwenda mhakamani kumstaki Mengi.

Wakati Rostam akienda Takukuru, tayari Mengi alipangua tena tuhuma za Rostam alizozielekeza kwake kwa kutumia velelezo na nyaraka kuwa alishamaliza madeni yote na hadaiwi na taasisi yoyote sambamba na kutoa maelezo kuwa hahusiki katika kuifilisi Benki ya NBC.

Mengi amefungua Kesi Mkahakama Kuu akimshitaki Roastam kwa kumkashifu na amemtaka amlipe sh. Bil.10.

Mbali na hao, Yusuf Manji, bila kutoa maelezo hadharani au kupangua tuhuma kama wenzake yeye amekwenda mahakamani moja kwa moja na kumshitaki Mengi, akidai amlipe sh. moja, kama fidia kwa kumchafua jina lake.

Jana mfanyabishara, Subhash Patel, ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Motisun Holdings Limited, , inayomiliki na kuendesha hoteli na viwanda hapa nchini amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kuwa ni miongoni Mafisadi papa nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi za makao Makuu ya Kampuni hiyo, zilizoko Mikocheni jijini, Dar es salaam jana, alisema lengo la kuitisha mkutano huo ni kutaka kujibu shutuma zilizotolewa na Mengi na kutoa ufafanuzi kwa umma, juu ya shutuma ambazo zinaendelea kutolewa na kutangazwa na vyombo vya habari juu yake.

Patel, ambaye hakuonekana katika mkutano huo, kama alivyofanya Mfanyabiashara Mwenzake Rostam, wakati wa kujibu tuhuma kama hizo, aliwatuma Afisa Uhusiano na Mawasiliano, wa kampuni hiyo ya Motisun Holdings, Aboukary Mlawa, Mwanasheria Deusdedit Dankan na Mkurugenzi wa Miradi Laurence Manyama, ambapo Mlawa alikuwa msemaji na kudai kuwa wamekuja kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo za Mengi na nyingine ambazo alisema zimekuwa zikiandikwa katika magazeti ya Mengi.

Bila kusema kama Mengi aombe radhi au watampeleka mahakamani, Mlawa, alisema Mengi amekuwa akimchafua Patel, kwamhusisha katika mchakato wa kumpata mbia wa kushirikiana na serikali katika mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na mradi wa Chuma cha Liganga yaliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Iringa.

“Kwa mfano katika gazeti la Kulikoni, la januari 16, mwaka huu kulikuwa na taarifa zenye kichwa cha habari Shabhash Patel katika ufisadi wa Mchuchuma, katika taarifa hiyo Shabhashi, alihusihwa na Nasir Karamagi, na Basil Mramba, watu ambao kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa mawaziri wa Viwanda na Biashara,”alisema Mlawa.

Bila kuelezea kwa undani juu ya tuhuma hizo, alisema gazeti la Kulikoni, pia limewahi kuandika kuwa kampuni ya MMI STEEL MILLS LTD, inayomilikiwa na Subhash Patel, ilitoa rushwa kwa wanakijiji.

Alitaja tuhuma nyingine mbayo Mengi amekuwa akimhusiha nayo kuwa ni kuhusu yeye Shubhash Patel, kumiliki gazeti la SAUTI HURU, analolitumia kuandika habari za uongo na za kumchafua Mengi na watu wengine.

Aidha, alisema kuwa katika tuhuma nyingine ambayo Mengi ameielekeza kwake ni kumuita yeye kuwa ni “Fisadi papa” na kuwa anaiba mabilioni ya Fedha za watanzania na kwenda kuzificha nje ya nchi.

Akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya Shutuma hizo, Mlawa, alisema kuhusu Mradi wa Chuma wa Liganga na makaa ya mawe ya Mchuchuma, bado hakuna kampuni yoyote, siyo yeye Shabhsh, wala kampuni yoyote imepewa mradi huo.

“Kilichopo ni kwamba moja ya kampuni zetu iitwayo MM STEEL RESOURCE PUBLIC LIMITED COMPANY, na siyo kampuni iliyotajwa na Mengi ya MM STEEL INDUSTRIES LIMITED ilishiriki katika zabuni namba PA/068/2008/NDC/PPP/01 ya mwezi April 2008 ya kutafuta mwekezaji wa ndani ambaye atakuwa na ubia na shirika la Maendeleo la Taifa kwa kuzalisha chuma kiitwacho “sponge”, chuma kilichopo katika mlima mdogo wa Maganga Matitu wilaya ya Ludewa na si Liganga wala Mchuchuma,”alieleza.

Aliendelea kueleza kuwa chuma hiki cha “Sponge iron” ni muhimu sana kwa viwanda vya chuma na taifa kwa ujumla kwani itasaidia kupunguza na kuondoa kabisa chuma chakavu, matumizi yanayolalamikiwa na kuhusishwa na uharibifu mkubwa wa Miundombinu ya taifa letu iliyojengwa kwa kutumia vyuma na kwa gharama kubwa.

“…Kampuni yetu ya MM STEEL RESOURCES PUBLIC LIMITED, ilishiriki zabuni hii kwa kufuata sheria na taratibu zote zinazohusiana na manunuzi ya umma,” alisema na Kuongeza.

“Kwa taarifa hii ya serikali iliyotolewa Bungeni na kwa mujibu wa maelezo yetu, mtaona kuwa shutuma za zimekuja katika wakati ambao siyo sahihi, yaani mapema mno. Mtaona pia kwamba tuhuma dhidi Subhash Patel, na kampuni yake ya MMI Steel Industries Limited, sio za kweli, ni za uzushi za na zina mapungufu makubwa.

“Ukiziangalia shutuma hizi kwa undani, utaona wazi kuwa zina nia ya kuingilia mamlaka zinazohusika katika mchakato unaoendelea wa kuwaopata wawekezaji katika miradi hii miwili ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na mradi wa chuma cha Liganga, ambacho kama tulivyoeleza awali hauhusiani na Ndugu Subhash Patel wala mojawapo ya makampuni yake,” alisema.

Kuhusu tuhuma dhidi yake ambazo Subhash anadaiwa kutoa kutoa rushwa kwa wanakijiji, alisema kuwa tuhuma za Mengi hazikutaja na kusema kuwa hajawahi kutoa rushwa kwa wanakijiji katika sehemu yoyote ya Tanzania.

Afisa Uhusiano, huyo alieleza kuwa anachofanya Subhash, ni kusaidia jamii, ya watu wenye matatizo mbalimbali na kusaidia miradi ya maendeleo ya kijamii hapa nchini

“Subhash, yeye mwenyewe na kupitia kampuni zake amekuwa akitoa misaada mbalimbali kwa makundi tofauti ya kijamii kama afanyavyo Mengi,” alisema

Hakuishia hapo, alisema kuwa mwaka 2008, kampuni ya MOTISUN HOLDINGS LIMITED, na makampuni mengine yanayomilikiwa na Subhash, yametoa misaada yenye dhamani ya sh. milioni 800, misaada hii inajumuisha pia misaada iliyotolewa mkoani Kilimanjaro ambako Mengi anatoka.

“Napenda watanzania waelewe kuwa si watu wote wanaotoa misaada kwa jamii ama makundi ya watu wnapenda kujitangaza na kutafuta umaarufu kupitia umasikini, matatizo ama ulemavu, wa watu wengine, sera ya makampuni yetu ni kutoa misaada kwa jamii na watu wote,” alimema.

Akizungumzia uhusuano wake na gazeti la SAUTI HURU, alisema Subhash Patel, hana hisa wala haimiliki gazeti hilo wala chombo chochote cha habari.

“Patel, hamiliki, hafadhili, wala hana hisa katika gazeti la SAUTI HURU wala chombo chochote kingine cha habari kama ambavyo Mengi alidai katika tuhuma zake, tunaamini kuwa Uhuru wa habari uachiwe waandishi wa habari wenyewe, sisi tufanye biashara tu,” alisema.

Akizungumzia tuhuma alizotuhumiwa kuwa anatorosha fedha na kuzipeleka nje ya nchi, alisema hiyo ni tuhuma nzito ambayo inamfanya Subhash Patel, kuonekana ametenda kosa la jinai linalojukana kitaalamu kama “Money Laundering”, na kusema kuwa Subhash Patel ni mtanzania halisi aliyezaliwa na kukulia nchini.

“Naomba watanzania waelewe na kutambua kuwa Subhash, Patel, ni mtanzania halisi aliyezaliwa na kulia katika kijijhi cha Lugoba, Bagamoyo mkoani Pwani hivyo Tanzania, ni kwao na ni kwake,’ alisema na kuogeza.

“Naomba itambulike kuwa katika kipindi chote cha uwekezaji Tanzania, Subhash, amewekeza ndani ya nchi hii katika miradi mbalimbali ya viwanda na mahoteli kama mjuavyo ndugu Subhash, ni mmiliki wa mkampuni za kuzalisha vifaa vya ujenzi kama vile nondo, bati, mantanki ya maji, rangi na vinywaji baridi kwa hiyo ni vigumu kuhamishika,” alisema

Alihitimisha hoja zake kwa kusema kuwa anashangaa ni kitu gani wanachogombania na Mengi, kwani mahusiano yao ni ya kibiashara kutokana na sehemu kubwa ya maeneo ambayo Subhash Patel anayatumia kwaajili ya viwanda vyake kuwa imewahi kumilikiwa na Mengi.

“Maeneo mengi yanayokuwa yanamikiwa na Mengi yamenunuliwa na Subhash Patel, baada ya viwanda vya Mengi kufa, kama kulitokea matatizo katika biashara basi matatizo haya yatatuliwe kibiashara na si kwa kuchafuliana majina binafsi,” Alisema.

Idadi hii imefanya wafanyabiashara waliojitokeza kuonyesha kupambana na Mengi baada ya kuwatuhumu kufikia wawili sasa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment