Na Mwandishi wetu na Mashirika ya Habari
Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Makundi ya Mimea na Wanyama Walio Katika Hatari ya Kutoweka (CITES), wamezitaja Tanzania na Zambia, kuwa ni vyanzo vikubwa vya biashara haramu ya pembe za ndovu
Imeleezwa kuwa tani nyingi zimekamatwa zikisafirishwa kinyume cha sheria zikiktokea katika nchi hizo katika miaka ya 2002, 2006 na 2009.
Hayo yamedhihirishwa katika mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine pia unajadili mapendekezo ya Tanzania na Zambia, ya kuruhusiwa na Makubaliano ya Biashara ya Kimataifa ya Makundi ya Mimea na Wanyama Walio Katika Hatari ya Kutoweka, kuuza hifadhi ya pembe za ndovu walizonazo.
Wanaoshiriki katika Mkutano huo unaoendelea mjini Doha, Qatar, wamesema kuruhusu Tanzania na Zambia kuuza akiba yake ya pembe kutaongeza kwa kiasi kikubwa mauaji ya wanyama hao katika bara la Afrika.
Makundi yameibuka miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano huo kwa upande mmoja ni ukanda wa nchi zinazopinga biashara ukijumuisha Kongo, Ghana, Kenya, Liberia, Mali na Sierra Leone.
Kwa upande mwingine, kila mmoja ikiwa na pendekezo lake ni Zambia na Tanzania, ambazo zinataka kuruhusiwa kuuza hifadhi ya pembe za ndovu zilizonazo katika mkutano ulioanza Machi 13 hadi 25 mwaka huu.
Katika miaka 30 iliyopita aina ya Tembo wa Afrika wamekuwa wakipungua kwa asilimia 35, na hadi leo wamebakia chini ya 500,000.
Hivi karibuni Waziri wa Mali Asili na Utalii, Shamza Mwangunga, amekaririwa akisema kuwa kati ya Machi na Mei mwaka jana, wizara yake ilipokea taarifa kupitia polisi wa kimataifa (Interpol-NCB-Dar es Salaam) kuwa kontena hizo zikiwa na meno ya tembo zikitokea Dar es Salaam zilikamatwa nchini Ufilipino na Vietnam.
Alisema baada ya taarifa hizo, Idara ya Wanyamapori kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Interpol Dar es Salaam, Lusaka Agreement Task Force na World Customs Organisation waliendesha upelelezi, ambapo watuhumiwa tisa walikamatwa na kupandishwa mahakamani.
Wajumbe wa mkutano huo wameeleza kuwa kuongezaka kwa mahitaji ya pembe katika nchi za Japan, China na Thailand, ni sababu za kuongezeka kwa kishawishi cha kutaka kuuza nyara hizo muhimu kuanzia mwaka 2000.
Mkutano huo umeanza Jumamosi iliyopita na utakuwa na ajenda nyingine zaidi ya hiyo ya Tanzania na Zambia.
Makubalino ya awali ya kusanyiko la Kimataifa la kulinda wanyamapori, liliweka aina mbili za kanuni za kulinda tembo, ambazo zimekuwa zikitumika pia kwa Tanzania na Zambia, inayokataza uuzaji wa Pembe, kuruhusu uuzaji mdogo kwa makubaliano maalumu na kila nchi kuhakikisha inawalinda tembo wake na kudhibiti uwandaji haramu.
Waziri wa Mazingira wa Uingereza Hillary Benn, ameongoza kwa kupinga mapendekezo hayo na kusema kuwa ni nchi yake itapiga kura kupinga.
“Katika mkutano wa CITES Uingereza itapiga kura kupinga mapendekezo hayo kutokaTanzania na Zambia ya kuuza pembe za ndovu, na tutazitaka nchi nyingine kupiga kura ya kupinga uuzaji huo,”alisema Waziri Benn.
Katika taarifa ya waziri Mwangunga, ilisema kuwa Machi mosi mwaka jana maofisa wa forodha katika Bandari ya Manila walikamata tani tatu za meno ya tembo yakiwa yamefichwa kwenye maboksi 18 ndani ya kontena lenye namba ECMU 1642240 na yaliyosafirishwa Oktoba 25, 2008 kwa meli iitwayo Delmas Nacala kupitia Bandari ya Dar es Salaam, yakiwa yamesajiliwa kama mzigo wa vifurushi 80 vya plastiki.
Alisema Machi 3, mwaka huu, maofisa wa forodha wa Bandari ya Manila Kusini, nchini Ufilipino, walikamata meno ya tembo tani 1.483 yakiwa yamefichwa kwenye makasha ndani ya kontena namba TSLU 6219947, ambayo yalisafirishwa Oktoba 25, 2008.
Mwangunga alisema Machi 2, 2009 maofisa forodha wa Dinh Vu (Nguyen Thi Thanh Binh) Hai Phong Vietnam Local walikamata vipande 1,224 vya meno ya tembo yenye uzito wa tani 6.232 yakiwa yamefichwa kwenye takataka za plastiki ndani ya maboksi 114, kwenye kontena namba ECMU 1721884, yaliyosafirishwa Desemba 28, 2008, kwa meli ya Delmas Nacala, kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Aidha, waziri huyo alisema Julai 4, 2006, maofisa wa forodha wa Bandari ya Kaohsiung, Taiwan Kusini walikamata meno ya tembo tani 5.217 yakiwa yamefichwa katika maboksi 18 yaliyokuwa ndani ya makontena mawili yenye namba PONU 0713898 na Maeu 7915043 ambayo yalisafirishwa Aprili 14, 2006 kwa meli ya Munstar kupitia Bandari ya Tanga.
Alibainisha kuwa, makontena hayo yalipitia Bandari ya Tanga yakiwa yamesajiliwa kubeba marobota 60 ya mkonge kwenda nchini Ufilipino.
Kutokana na hilo, wizara ikitenga kiasi cha sh milioni 25 kwa ajili ya kuiwezesha timu ya wapelelezi kutoka Idara ya Wanyamapori, Polisi wa Interpol (Dar es Salaam) na Lusaka Task Force kwenda Vietnam kufuatilia na kupata vielelezo zaidi.
Katika mkutano huo, Tanzania inawakilishwa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Usimamizi wa Hifadhi ya Afrika, James Lembeli, ambaye pia ni Mbunge wa Kahama (CCM).habari hii imechapwa kwenye gazeti la tafakari la Machi 19 hadi 23 2010
Mwisho
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment