Popular Posts

Friday, September 9, 2011

DPP umemskia Manji? Anawaweza kuwa shahidi Muhimu

Na Deogratius Temba.
NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni 40 kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Kwa kipindi chote hicho, serikali imekuwa na kigugumizi cha kukataa kumtaja mmiliki halali wa kampuni hiyo, licha ya mamlaka ya usajili wa makampuni (BRELA) kutaja majina ya wamiliki ambao hata hivyo Watanzania waamini kuwa ni wamiliki ‘feki’.
Kwa muda mrefu Watanzania wamkuwa na uchungu dhidi ya wizi wa rasilimali zao na watu wachache kuliibia taifa hili na kunufaika wao binafsi wakati mamilioni ya Wananchi wakitaabika na umasikini wa kutupwa. Watanzania wameitaka serikali kumtaja mmiliki halali wa Kagoda na mahusiano yake na Chama Cha Mapinduzi(CCM), lakini imekaa kimya. Mfanya biashara Yusuf Manji, anaweza kuwa shahidi muhimu sana wa kesi hii, akatueleza mahali ofisi za Kagoda zilipo na wamiliki wake na aliyempeleka Kagoda kufanya nao mikataba.
Kuna usemi usemao “za Mwizi ni arobaini” sasa zimefika, kila kitu dhidi ya Kagoda kitaanikwa na ulimwengu utaujua ukweli na nchi yetu itakuwa huru.
Bunge limelalamikia mara kadhaa juu ya mmiliki wa Kagoda lakini serikali haikutaka kumtaja mmiliki, serikali imetakiwa kuwataja hadharani walioiba fedha za EPA kupitia Kagoda lakini imekataa, lakini nchi hii ilivyo na za mwizi zinavyotimia, wanajitaja wenyewe na wanajianika waziwazi. Tunasubiri kuyaona mengi zaidi. Manji amejua kuwa maji yamemfika shingoni, pamoja na usiri wa serikali na vyombo vya dola kutomtaja, lakini yeye anaona hali yake inazidi kuwa mbaya kwasababu anashambuliwa na ameamua kukiri kuwa amekwapua fedha za EPA. Hii ni hatua nzuri.
Na hii ni ngumu ya umma imezaa matunda, lamsingi ni kwamba watanzania wazalendo hawatachoka kurusha mawe kwenye mapango walimojificha wahujumu uchumi hadi wachomoke wenyewe.
Tunajiuliza ni kwanini serikali imeendelea kuwa na Manji karibu kama rafiki wao na mfadhili wa CCM wakati moja ya kampuni zake kama hii ya Quality Finance Cooperation Limited imechukua fedha za wananchi na kukaa nazo bila kulipa riba? Je huu sio wizi wa rasilimali za wananchi masikini? Je kama serikali isingeshinikizwa na vyombo vya habari na wanaharakati mbalimbali, juu ya wizi wa EPA Manji angerejesha fedha hizo?
Manji mwenyewe amekuwa msiri kwa kipindi kirefu, kama kweli angekuwa mzalendo na mwananchi mwenye uchungu na taifa hili angekuwa amejitokeza tangu awali na kutangaza kuwa kampuni yake ni moja ya waliokopa Kagoda na kueleza ukweli juu ya utapeli aliofanyiwa na KAGODA, lakini hajawahi kujitokeza waziwazi hadi alipotajwa mara kadhaa kuwa yeye ni mmiliki. Sasa anajitoa.
Kwa mara ya kwanza, pamoja na kutajwa na wanasiasa kuwa ni mmoja wa waliokwapua fedha hizo, uhusika wa Manji kwenye EPA ulianza kuonekana na kudhibitika kwenye vielelezo vya ushahidi kwenye kesi yake ya madai ya shilingi 1, dhidi yake na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi. Watanzania wanaotafakari kwa haraka na kupata majibu waliliona hilo na kulihitimisha. Lakini Mahakama haikutaka vielelezo hivyo viwe wazi.
Kitu cha kujiuliza kwa kipindi chote hicho, pamoja na kushinikizwa serikali imegoma kabisa kuwataja Manji na washirika wake wengine kuwa ni watuhumiwa wa EPA, imegoma hata kuwataja waliorudisha fedha hadi wanajitaja wenyewe. Hii ndio serikali tulioiweka madarakani, tunajidai kuwa eti ni serikali ya demokrasia, uwazi, na ukweli. Je kweli hapa kuna utawala bora?
Kwa hili la kumficha Manji hadi anajitokeza mwenyewe nidhahiri kuwa nchi yetu ipo mikononi mwa kundi la watu wachache na serikali haiwawezi. Tusipoteze muda kumjadaili Manji na kampuni zake ila atusaidie ushaidi. Akihojiwa kiukweli kama vyombo vyetu vya dola vipo huru basi anaweza kupelekewa mahakamani.
Na kama Kagoda ni mali ya serikali basi tuelezwe ukweli, na kama ni CCM tuambiwe kwasababu sasa Manji ametangaza mgogoro na Kagoda na anawadai ina maana anaweza kulipwa kwa fedha za walipa kodi. Wakati waliozitumia fedha hizo ni wengine. Tunataka kupata mwongozo wa wazi, na serikali ivunje ulimya kwenye suala la Kagoda.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) analojukumu la kutekeleza sheria na kuonesha dhana ya utawala wa kisheria hapa nchini kwa kumkamata Manji na kumhoji, na sio kumhoji tu atoe ushahidi muhimu kabisa juu ya kampuni ya Kagoda, kama hili halitafanyika tuamini kuwa Kagoda ndio imeiingiza serikalki madarakani na siku ikitajwa serikkali itavunjika.
Pamoja na kuwa Manji analalamika nay eye ameshatuibia kwa kumiliki fedha za walipa kodi masikin wa taifa hili bila huruma huku akishuhudia wazee wetu wakifariki kwa kukosa asipirini hospitalini, kukosekana kwa maji safi ya kunywa na zahanati wakati yeye anafaidi faida lukuki kwa mabilioni yetu, atoe ushaidi halisi wa kumtaja mmiliki halali wa Kagoda.
Pamoja na kuwa Manji hajataja kiasi hali cha fedha alichochukua Kagoda asiendelee kulalamika kuwa amepata hasara kwa fedha (mabilioni) ambayo amekaa nayo miaka mitatu. (2005-2008) huwezi kukaa na mabilioni ya mtu kwa kipindi hicho ukawa huna faida.
Pia Manji arudishe sehemu ya faida kwa wananchi kwa kujenga zahanati vijijini na dawa ili watanzania wamsmehe.
DPP anatakiwa kuheshimu katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumkamata Manji ali amsaidie usahhidi muhimu. Kama DPP atashindwa kuwapeleka mhakamani wamiliki wa Kagoda kwa atakuwa ameshiriki kuwaibia watanzania rasilimali zao na atakuwa amevunja katiba inayompa mamlaka ya kumshitaki, kumkamata mtuhumiwa na kumfungulia mashataka pale anapojiridhisha kuwa amehusika na kosa.
Kila la heri na jumapili njema!

11 comments:

  1. Hello, Neat post. There's an issue together with your site in web explorer, could test this? IE still is the market chief and a good component to other folks will pass over your magnificent writing due to this problem.

    Feel free to visit my weblog: money making opportunity

    ReplyDelete
  2. If you want to increase your knowledge just keep visiting this website and be updated with the hottest news
    posted here.

    My site: Private Krankenversicherung Wechseln

    ReplyDelete
  3. There is certainly a lot to know about this issue. I
    really like all of the points you made.

    Take a look at my webpage it business idea

    ReplyDelete
  4. This paragraph is actually a fastidious one it helps new the web users,
    who are wishing in favor of blogging.

    Here is my web page: Günstige Reisen Türkei

    ReplyDelete
  5. What's up, every time i used to check blog posts here early in the dawn, as i love to gain knowledge of more and more.

    Here is my blog; seo advertising

    ReplyDelete
  6. It is the best time to make some plans for the future and
    it is time to be happy. I have read this post and if I could I want to suggest
    you some interesting things or advice. Perhaps you could write next articles referring to this article.
    I desire to read even more things about it!

    Here is my weblog: krankenkassen freiwillig versichert

    ReplyDelete
  7. You really make it seem so easy with your presentation but
    I find this matter to be really something that I think I would never understand.
    It seems too complicated and very broad for me.
    I am looking forward for your next post, I will try to get the hang of it!


    My weblog can i get a house loan with bad credit

    ReplyDelete
  8. Hey there, You've done an excellent job. I'll certainly digg it and personally suggest
    to my friends. I am confident they will be benefited from this website.


    Look into my webpage ... affiliate programs that pay

    ReplyDelete
  9. Thank you for sharing your thoughts. I truly appreciate your efforts and I will be waiting for your next post thank you
    once again.

    my page: buy here pay here used cars in nj

    ReplyDelete
  10. luckyclub.live: The casino site of the lucky club
    luckyclub.live: The casino site of the lucky club. Live: The casino site of the lucky club. Live: The casino site of the luckyclub.live lucky club. Live: The casino site of the lucky club.

    ReplyDelete