Popular Posts

Friday, September 9, 2011

Magunzo ya uwezeshaji ngazi ya kitaifa

Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ngazi ya kijamii, hadi kitaifa kwa kuwajengea uwezo wawezeshaji wa ngazi ya kitaifa ili waweze kufika vijijini.
GTI ambacho ni chuo pekee kinachotoa mafunzo ya Jinsia nchini, kilianza kama program za TGNP wakati shirika lilipoanzishwa mwaka 1993, na mwaka 2008 GTI imeandikishwa kama Chuo au taasisi ya mafunzo katika baraza la elilimu ya ufundi (NACTE).
Wakati harakati zikiendelea GTI kimeweza kutoa mafunzo na kuandaa mitaala katika ngazi ya 1,2,3,4 na 6, na kupata kibali cha kutoa cheti na stashahada(Diploma).
Akifungua mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya kitaifa yalkiyopfanyika kuanzia …… katika Mambibo dare s salaam, Mkurugenzi wa GTI, Dk.Diana Mwiru, amesema Watanzania wote hawatatulia hadi ukomboziz wa mwanamke kimapinduzi ufanikiwe na taifa likubali mabadiliko hayo “ TGNP tunatambua kuwa suala la vuguvugu na mapambanao dhidi ya ukombozi wa mwanamke na usawa wa kijinsia hapa nchini sio letu pekee. Tunajikita zaidi kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuwajengea watu wengi uwezo ili waweze kufanya maamuzi yao wenyewe”Amesema Dk. Diana
Kwa mujibu wa Dk. Diana Ni jukumu la TGNP kujenga uwezo kwa watu wa ngazi zote hatua inayoifanya taasisi hiyo kuwa na jukumu kubwa la kutekeleza mipango yake ya kuibadilisha jamii na kuifanya ikubali mabadiliko hasa yale ya kimapinduzi.
“katika kutekeleza hilo hatuwezi tukiwa na watu wachache kwani kidole kimoja hakivunji chawa; harakati zinahitaji nguvu ya pamoja ili kupaaza sauti kwa nguvu kupigania haki za wanyomnge.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo, walitakiwa kuheshimu muda wanapokuwa katika mafunzo,kujiweka tayari kupokea, kwani malengo ya mafunzo hayo yalikuwa ni kuwajengea washiriki uelewa na maarifa zaidi katika kuhoji na kufanya uraghbishi katika ngazi ya kijamii.
Pia mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo wawezeshaji kuelewa dhana na muktadha wa kimapinduzi ikiwemo kukuza namna ya kuwa waraghibishi zaidi. Kutaka kujenga vuguvugu la kimapinduzi na kukuza namna ya kuw waraghibishi zaidi.

15 comments: