Na Deogratius Temba
WIKI iliyopita katika mfululizo wa ripoti hii muhimu ambayo imetolewa na viongozi wa dini mara baada ya kufanya ziara katika migodi yote nchini tulieleza tadhimini ya fidia na mali kwa wakazi wanaopisha upanuzi wa migodi.
Ni muhimu kutambua kuwa ripoti hii ya viongozi wa dini haipingani sana na ile ya tume ya rais ya kuchunguza mikataba na hali ya migodi iliyoongozwa na Jaji Mark Boman, mwaka 2007 na kuhitimisha kazi yake mwaka 2008, bali inaongeza na kusisitiza mambo kadhaa ya msingi kwa jamii.
Wiki iliyopita tulianza na maneno ya mwanafalsafa, Mtakatifu Augustino anayosema kuwa’ Hisani haiwezi kuwa mbadala wa haki iliyonyakuliwa au haki iliyonyakuliwa haiwezi kufidiwa kwa hisani”.
Sehemu hii leo ni mwendelezo wa tathimini na fidia ya mali za wananchi: ripoti inasema inasema: ........... kitu kikubwa kinachokosekana hapa ni kuona kuwa fidia inayolipwa inapaswa kufidia hasara ya njia za kiuchumi zilizoharibiwa. Cha muhimu kuzingatia hapa ni ardhi iliyochukuliwa, majengo, mazao na mifugo. Imebainika pia kuwa wahisani wanatumia mbinu za kuwagawa wakazi ili wapate mbinu za kuwatawala(divide rule) kwani watu 44 waliolipwa fidia walichukuliwa kama watu pekee waliostahili kulipwa.
Kuhusu wanyama, mali na vitu vingine ambavyo bado umiliki wake haujadhibitishwa, Serikali inatakiwa kufanya uchunguzi wa kubaini ukweli na hatmaye fidia iweze kulipwa na kama fidia waliyokwishalipwa ndiyo hasa waliostahili kulipwa.
Kuna haja ya kuwahoji watunga sheria wetu, watufahamishe ni lini na vipi sheria zetu zitazingatia hali halisi inayowaadhiri wananchi mbele ya wawekeaji hawa matajri. Je kuna nafasi ya kuzifanyia mageuzi sheria zetu ili wananchi wajisikie wanatendewa haki katika njia zao za uchumi zilizopotea?
Uhamishaji na uodoaji wa wakazi katika maeneo yao
Tulipofika Nzega, tulikutana na kundi la wachimbaji wadogowadogo. Hali zao za mwonekano wao ulikuwa wa watu waliokata tamaa na waliopoteza matumaini ya kuishi. Kulikuwa na manunguniko kila upande, kulikuwa na nyuso zilizojaa machozi ya ndani kwa ndani.
Hata hivyo tatizo linabaki kuwa wakati ambapo mwekezaji anadai kuwa ameshawalipa fidia wachimbaji wadogo walihamishwa suala la wachimbaji hao wadogo kunyimwa haki zao linabaki kuwa kitendawili.
Wachimbaji wadogo wa Nzega waliyataja mambo yafuatayo kuwa ndiyo yanayowaumiza sana kwa sasa. Kuondolewa katika maeneo yao bila kufanyiwa tadhimini yeyote wala kulipwa fidia yoyote. Kuondolewa katika maeneo yao bila kupewa maeneo mbadala.
Kushindwa kusomesha watoto wao kutokana na ugumu wa maisha na kuhamahama, Upungufu wa maji ukosefu w a huduma za afya na huduma nyingine za kijamii.
Lakini kamati yetu ya viongozi wa dini ilibaini kuwa namna ya kuondolewa kwa wakulima katika maeneo yao kunatofautiana. Kinacho onekana Geita, Mara, Bulyanhulu, na Nzega ni kwamba kampuni za madini zinajichukulia maeneo makubwa ambayo wananchi wake wamekuwa wakiyategemea katika kuendesha maisha yao bila ridhaa yao na bila fidia inayostahili.
Shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu
Mara tulipofika Bulyanhulu, ili kukutana na wahanga walitupokea kwa mashaka na maswali mengi. Wengine walisikika wakisema “tumechoshwa na tume. Tunaamini ninyi nanyi hamjatumwa na serikali, tumeruhusiwa kuishi hapa lakini hatujui hatima yetu kwani muda wowote tunaweza kuondolewa kwasababu hatukupewa hati miliki ya ardhi”
Katika ziara ya Bulyanhulu tulitulikutana na kundi la watu waliokuw a wachimbaji wadogo wadogo walitueleza jinsi walivyoondolewa katika maeneo yao na jinsi walivyoadhirika.
Kulikuwa na madai kwamba katika mgodi wa Bulyanhulu wachimbaji wadogo wadogo 50 walizikwa wakiwa hai wakati wa zoezi la kuwoandoa kwa nguvu katika yao mwezi Agost 1996, shutuma hizi zimeshuhidiwa na baadhi ya watu pia mama wa watoto wawili wanaosadikiwa kuuawa katika harakati hizo.
Shutuma hizo pia zilipatakana kwenye filamu zenye matukio yaliyorekodiwa kuhusu uchimbaji madini na adhari zake kwa jamii na wananchi waliohamishwa.
Ingawa ujumbe wetu haukuweza kupata ushahidi wa kutosha kuhusu shutuma za mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ni jukumu la mamlaka husika au serikali kusuluhisha mgogoro iliyopo ili kuepusha kueleweka vibaya au kupoteza imani kw a wanaanchi kunakoweza kusababisha wananchi kuwachukia wawekezaji, viongozi na vyombo vya dola.
Ipo hatari ya kukaa kimya na hata kunyamazisha maelezo yanayosadikiwa kuendelea kuumiza nafsi za ndugu ama wahanga ni vema kutafuta njia itakayoleta suluhisho na kuondoa mashaka katikati ya jamii husika.
mwisho
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment