*Tanesco: Tunakabiliana na hali hiyo
Na Deogratius Temba
SIKU moja baada ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kuzima mitambo yake ya kuzalisha umeme wa Megawat 100, iliyoko Tegeta jijini Dar es salaam, serikali imesema haihusiki kununua mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo.
IPTL ilitangaza kuzima mitambo sita yenye uwezo wa kuzalisha Megawat 60, kati ya 70, ambazo zimekuwa zikiingizwa kwenye grid ya Taifa tangu mwezi Novemba kutokana na kile walichodai kuwa ni ukosefu wa fedha za kununuliwa mafuta.
Akizungumza katika mahojiano na Tanzania Daima jijini Dar es salaam, jana Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha, alisema serikali haihusiki katika kusimamia suala la kuagiza mafuta kwani IPTL inazalisha umeme ambazo inauuza kwa Tanesco, kwa hiyo kukosekana kwa mafuta wanapaswa kuwajibika.
“Sisi serikali ni wasimamizi wa sera tu, hatuhusiki na mafuta, kama tuliwapa mafuta kipindi kile sasa wanazalisha umeme na wana uza kwa Tanesco, na Tanesco anawalipa fedha, wazitumie fedha hizo kununulia mafuta,” alisema Tesha.
Alisema kwa sasa serikali imeiachia suala hilo IPTL, Tanesco, na Msimamizi wa mitambo hiyo, Wakala wa usajili wa Vizazi na vifo(RITA) walijibu kwani wao ndiyo wanajua kama wanauhitaji umeme au la.
“Huyo IPTL amezalisha umeme kwa siku zote hizo tangu mafuta yalipokuja, anapeleka wapi umeme anaouzalisha, anatupa shimoni? huyo Tanesco naye anaponunua umeme IPTL si anapata fedha? kama anahitaji umeme wa kuuza kwanini asimlipe IPTL ili azalishe,”aliongeza
Alieleza kuwa Tanesco inapaswa kuomba umeme ambao ina wateja wa kuutumia kwahiyo kama inaendelea kununua umeme wa IPTL ni dhahiri kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya nisahti hiyo na anapaswa kuulipa IPTL fedha ili inunue mafuta.
Pia Tesha alisema kuwa hadi sasa vyanzo vyote vya umeme nchini yakiwemo mabwawa ya kuzalisha umeme, kama Kidatu, Mtera, hale na Pangani vina maji ya kutosha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbali na vyanzo hivyo alisema mitambo ya Songas ya kutumia gesi asilia ni mizima, na mitambo ya serikali ya kuzalisha umeme wa Megawat 45 ya kutumia gesi asilia nayo inazalisha umeme wake wote kwa sasa.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema wao wanajipanga kukabiliana na upungufu huo wa megawat 60, kwa kuangalia vyanzo vyake vya umeme ili mgao usijirudie.
“Sisi Tanesco tunapambana na upungufu huo, tunachosisitiza ni kuhakikisha tunakabiliana na hali hii tusiingie tena kwenye mgawo. Tunawaomba wananchi wasishtuke wala kuhangaika, wavute subra wakati mbao tunapambana,” alisema
Badra alisema wanachofanya kwa sasa ni kuhakikisha wanaangalia vyanzo vyote vya kuzalisha umeme vya maji, gesi asilia na mafuta ili kufidia kiwango hicho cha umeme kinachopungua.
Alipotakiwa kueleza mahitaji halisi ya umeme nchini kwa sasa na kama bado Tanesco inahitaji umeme wa IPTL baada ya mitambo iliyoharibika kupona alisema: “Bado tunauhitaji umeme wao, cha msingi tuacheni tupambane na hali hii kwanza,”alisema Badra.
Serikali iliingiza nchini mafuta ya kutumika kwa siku 15, yenye thamani ya sh. bilioni tisa kiasi cha metriki za ujazo tani 7,524 sawa na lita za ujazo milioni 7.52, baada ya agizo lililotolewa na rais Jakaya Kikwete, kutokana na kukidhiri kwa mgao wa umeme uliolikumba taifa kuanzia mwezi septemba mwaka huu,
HABARI HII INAPATIKANA KATIKA AGZETI LA TANZANIA DAIMA LA KESHO
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment