Na Deogratius Temba
WIKI iliyopita katika mfululizo wa ripoti hii inayoelezea ziara nzima ya viongozi wa dini katika migodi ya madini Tanzania, na kujionea hali halisi ya wananchi wanaoishi jirani na migodi au wanaofanya shughuli ndani ya migodi, tuliangalia ziara ya mkoa wa Mara na Mwanza katika migodi ya Geita na North Mara.
Wiki hii tuna angalia mchango wa Mawazo na uchambuzi wa viongozi hao walikiwa katika maeneo hayo.
Wanasema: “Wengi wetu katika ziara hii tulitarajia kuziona jamii za maeneo ya karibu na migodi hii zikiwa zinanufaika katika maeneo yao kwanjia moja au nyingine na shughuli za migodi. Ishara ya kwanza iliyokuwa kinyume na matarajio hayo ilikuwa ni barabara ya upande wa pili wa kivuko cha Kamanga, barabara iendayo kwenye mgodi mkubwa wa Geita haina lami na mbaya zaidi ina mashimo.
Njiani tulishuhudia nyumba za wenyeji nyingi ya nyumba hizo ni za udongo, na matofali mabichi ya tope. Hali kama hii pia tuliishuhudia katika maeneo ya mgodi wa Norh Mara ambapo hali ilikuwa mbaya zaidi, hasa kwa upande wa barabara kwa eneo linalozunguka mgodi wa Buhemba ambao umefungwa kwa sasa.
Muonekano wa watu na watoto ulituleza hali halisi, nguvu ya maneno yasiyosemwa na kauli sizizoandikwa zilileta haja ya kuionea wenyewe maana ya kuishi katika eneo lililochangia kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika. Shauku yetu iliongezeka zaidi na kutamani kuona zaidi ili kukidhi fikra zetu kwa kujionea maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi katika eneo hili.
Uharibifu wa vyanzo vya maisha
Inasemekana kwamba, “Watu zaidi ya milioni moja walitegemea ajira za migodini kati ya miaka ya 1980 na 1990, wamepoteza vyanzo vyao vya kujipatia riziki,” utafiti mmoja ulikadiria kwamba kufikia mwishoni mwa miaka ya 1990,sekta hii ilitoa ajira ya watu kati ya 500,000 na milioni 1.5, kufikia mwaka 2006 taarifa iliyotolewa na Benki ya Dunia ilionyesha kwamba Tanzania ilikuwa na wananchi wachimbaji wadogo wadogo 170,000 ni vigumu kupata idadi kamili ingawa utafiti unaonyesha kuwa idadi ya wanaopoteza ajira inakua kila mara
Wakati wa Ziara katika mgodi wa Dhahabu wa Geita, na maeneo yanayouzunguka ilibainika kuwa familia 86 zimeondolewa katika maeneo yao katika kijiji cha Mtakuja katika Wilaya ya Geita kupisha kampuni ya mgodi wa dhahabu wa Geita.
Familia hizo zilipewa hifadhi katika eneo lililotelekezwa na mahakama ya mwanzo. Jengo hilo hadi tulipolitembelea lilikuwa na takribani watu 250 na watu hao ambao wanaishi katika mazingira magumu na wanailaumu serikali na vyombo vya kutetea haki Tanzania kwa kufanya maisha yao kuwa magumu kiasi hicho.
Wengi kati ya hawa walitueleza kwamba zoezi la kuwaondoa katika maeneo yao lilifanywa usiku chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi. Zoezi hili liliwaadhiri hata wale ambao walihitaji uangalizi maalumu kama alivyotuleza mama Febrona Selestine jinsi alivyolazimishwa kuhama akiwa mjamzito na watoto wake sita wakati mumewe akiwa hayupo.
Watu hawa wanaeleza wenyewe kuwa walikwenda mahakamani ambako walishinda kesi na hivyo kuruhusiwa kurejea katika maeneo yao na kubaini kuwa maamuzi ya awali yalikuwa na hitlafu.
“Tulipeleka suala hili mahakamani ambapo tulishinda kesi mara ya kwanza; lakini kampuni ya mgodi wa Geita ilikata rufaa na ikapewa hati ya kutuondoa. hata hivyo muda muda mfupi baadaye, amri nyingine ya kutaka turejeshwe katika maeneo yetu tuliyoporwa ilitolewa.
“Lakini hadi sasa mahakama hijafanya lolote kutuondolea matatizo yetu Kinacho tushangaza ni kwamba: Kwanini mahakama Kuu iliharakisha kutuondoa katika maeneo yetu lakini ilichukua muda mrefu kuturejeshea maeneo hayo?”
Akielezea hali ya maisha katika kambi, Febrona anasema “Ni hatari kwa watoto hapa, kuna watu miongoni mwetu wanaumwa Kifua kikuu na sasa wameanza kufa tuko watu 249 katika eneo hili dogo, wanaume wanawake watoto na wajukuu vikongwe na ndugu wengine tumesongamana humu, jambo hili lina achwaje litokee?”
Shughuli za kiuchumi za watu walioondolewa katika maeneo ya migodi na maeneo mengine ya jirani zilikuwa ni kilimo na uchimbaji mdogo mdogo wa madini. Jamii hizi kwa sasa zimeadhirika sana kwani hakuna ardhi kwa shughuli zao hizo.
Kulikuwa na watu ambao hawakuwahi kuwa na upungufu mkubwa wachakula; lakini tangu waondoke katika maeneo yao wanaishi kwa kuomba omba.
Tukiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, tulimuuliza ni kwa namna gani serikali imezisaidia familia zilizohamishwa kutafuta namna ya kuishi na kupata huduma muhimu za kijamii kutoka katika serikali yao.
Mkuu wa wilaya ya Geita alieleza kwamba” hatma ya familia 86 ipo zilizohamishwa ipo mikononi mwa mahakama ya rufaa ambayo imetoa amri ya kurejeshwa katika maeneo yao ya awali.
Kitu pekee tulichoweza kuwasidia ni kuwatafutia mahali pa kujihifadhi kwa muda wakati tunasubiri mahakama itekeleze amri hiyo. mahali walipohifadhiwa si pazuri lakini hatuna mahali pengine. Mimi ni ofisa wa serikali na nilitamani kuwasaidia, lakini shauri lao lipo mahakamani na siwezi kuingilia mahakama, Ninachoweza kufanya katika mamlaka yangu ni kujaribu kuwapa ahueni”,watu hawa hawaishi kama binadamu wengine .hawana mahitaji muhimu.
Hali iliyoshuhudiwa na ujumbe wetu ni tofauti na matarajio ya kuwa na sekta imara ya madini yenye tija kwa taifa. ingawa kulikuwa na dai la kuboreshwa kwa huduma za kijamii kwa maeneo yanayozunguka mgodi kilichoonekana wakati wa ziara yetu ni hiki kifuatacho.
Jamii bado inaendelea kupata huduma duni za kijamii, kama vile Maji. afya, na elimu wanajamii wa Geita bado wanatumia maji toka katika visima ambavyo sii salama, wanajamii wa Kakola hawana kituo cha afya ingewa madini yanachimbwa mita chache karibu na eneo lao. Viongozi wa vijiji pale North Mara walisema kwamba ingawa wawekezaji wa Barrack wanadai wamefanya kazi kubwa ya ujenzi(Ukiachilia mbali shule moja walioijenga mbayo walimu wake wanalala madarasani), sehemu kubwa ya ukarabati huo ni ukarabati wa miundombinu.
Huduma za kijamii zilizoko katika maeneo yanayokaliwa na wawekezaji kama vile uwanja wa michezo wa Geita, maji toka ziwa Victoria, yanayopitia katika kijiji hicho huduma za afya na nyinginezo ni hadhi ya juu.
Lakini watu wanaoishi kuzunguka maeneo hayo, hawana fursa ya kuzitumia, hivyo ni sawa na kuwa wawekezaji na wanajamii wanishi katika dunia mbili tofauti.
Vijiji saba vya Tarime vimesaini makubaliano na serikali ya kulipwa asilimia fulani ya pato toka mgodini wakati wa mkutano huo wanakijiji hao walithibitisha kuwa hawajawahi kulipwa hata senti moja na mwekezaji.
Mwanzoni mwa mwaka 2007, kundi la vijana katika kijiji cha Kakola karibu na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu walifunga barabara iendayo mgodini .Kitendo hicho kililenga kuishinikiza serikali na mgodi kuwaondolea kero zao.
Itaendelea ..........
0784 /715 686575
deojkt@yahoo.com
ripoti hii itatoka pia katika gazeti la Tanzania daima la Alhamis 10/12/2009
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment