Popular Posts

Monday, December 7, 2009

Miundombinu mibovu chanzo cha bei kubwa ya saruji

Na Deogratius Temba
WADAU wa sekta ya uzalishaji wa Saruji Afrika ya Mashariki(EACPA), wamesema kupanda kwa bei za saruji nchini kunasababishwa na ubovu wa miundombinu.

Pia wamedai kuwa kubadilika kwa sera kila mara na kupanda kwa gharama za Nishati ya umeme imekuwa tatizo kubwa ambalo linaongeza gharama za uzalishaji.

wakizungumza na waandishi wa habari wandamizi wa habari za biashara, wadau kutoka katika sekta hiyo, walisema gharama za kusambaza saruji nchini au kusafirisha malighafi zinapanda kwa kasi kuliko zile za kuingiza kutoka nje ya nchi.

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Mbeya , Mbuvi Ngunze, alisema Miundombinu ni tatizo kubwa kwani kusafirisha tani moja ya mzigo wa Saruji kutoka Dar es salaam, hadi Kigoma ni dola za Kimarekani 86 wakati kutoka Karachi kwenda Dar es salaam, kwa Meli ni dola 25 tu.

Alisema tofauti iliyopo kwa gharama za kusafirisha saruji kutoka nchini Uganda na Kenya kuingiza Tanzania, hasa katika mikoa ya kanda ya Ziwa inatokana na miundombinu yao kuwa nzuri.

Wadau hao walikanusha kusafirisha saruji kwenda nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kutengeneza viwanja vya mpira, wakisema kuwa bei ya saruji hapa nchini ipo juu kuliko nchi nyingine kwahiyo siyo rahisi kupeleka saruji uliyoizalisha katika mazingira ya gharama kubwa vile.

Mwisho

No comments:

Post a Comment