Popular Posts

Thursday, November 19, 2009

Mwandishi ahojiwa na polisi kwa kumwandika vibaya RC

Na Deogratius Temba

MWANDISHI wa habari wa kujitegemea wa magazeti ya Kulikoni na Tanzania Daima, Jumbe Ismailly wa Singida, jana aliwekwa kitimoto na maafisa upelelezi wa jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi Singida.

Mwandishi huyo alitakiwa kutoa maelezo mbele ya polisi kuwa ni kwanini amekuwa akimwandika Mkuu wa mkoa huo Vicent Paleseko Kone, vibaya na amekuwa akishiriki vikao vyake na wananchi na kuandika habari bila idhini yake.

Akizungumza jana na Tanzania Daima, kwa njia ya simu kutoka Singida, Jumbe alisema alianza kuhojiwa jana asubuhi kuanzia saa 5:00 hadi saa 7:06, na kudai kuwa wakati akihojiwa askari hao walikuwa wameshika mikononi karatasi za vipande vya magazeti vyenye habari alizoandika juu ya RC.

“Niliitwa nikaelezwa kuwa RC amelalamika kuwa nimemkashifu na nimekuwa nikimwandika sana bila ruhusa yake. Pia niliulizwa ni kwanini nilishiriki katika mkutano wa hadhara wa RC na wanakijiji wa Kisasida wa Machi 5, mwaka huu na kuandika habari,”alieleza Jumbe

Alisema kuwa katika mahojiano hayo alielezwa kuwa Mkuu wa Mkoa analalamika kuwa amekuwa akishiriki mikutano hiyo na wananchi wanapotoa maneno ya kashfa kwa RC yeye anayaandika yote.

Baadhi ya taarifa ambazo Mkuu wa Mkoa amezilalamikia ni ziliyochapwa katika gazeti la Tanzania Daima la Januari 18, 2007, iliyokuwa na kichwa cha habari “RC Singida amsimamisha kazi mume wa mbunge,” na nyingine iliyotoka kwenye gazeti la Kulikoni Machi 5, mwaka huu kuwa mkutano wa wanakijiji na RC wavunjika.

Jumbe aliendelea kueleza kuwa katika maojiano yake na askari huyo, aliyetambulika kwa jina la Koplo Lugendo, habari nyingione ambayo ililalamikiwa ni ya Machi 17, mwaka huu iliyokuwa na kichwa cha habari “RC kuburuzwa mahakamani’

Aidha Jumbe alisema kuwa licha ya kuelezwa kuwa wanalalamikiwa waandishi wengi wa habari lakini alijikuta akiwa yeye peke yake mbele ya mashushu hao huku wakiwa wameshika habari zake alizokwisha toa kwenye magazeti.

mwisho.

No comments:

Post a Comment