Popular Posts

Wednesday, November 18, 2009

Mawaziri walizwa

Andrew Chale na Shehe Semtawa,Dar

MTANDAO wa matapeli wa kimataifa unaotumia mbinu mbali mbali za kutapeli, umewaliza vigogo wa ngazi za juu serikali, wakiwemo mawaziri na wakuu wa idara nyeti nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jeshi lake linawashikiria baadhi ya watu hao, ambao alisema wanatumia mbinu za kimataifa kutapeli.

“Matapeli hawa wao wanapojua wizara fulani ipo karibu na kampuni fulani, hujifanya waziri na wakati mwingine kuigiza hata sauti ya mawaziri hao na kufanya utapeli wa mamilioni ya fedha,”

Aliendelea kusema kuwa ili kutimiza lengo lao matapeli hao wakati mwingine hupiga simu na kujitambaulisha kuwa yeye ni waziri fulani na ana shida ya fedha kwa ajili ya ada, safari na mambo mengine na kwa kawaida kiasi cha fedha wanazoomba huwa ni mamilioni,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, wakurugenzi wa makampuni yanayoombwa fedha hizo wakikubali, matapeli hao hutumia madereva wenye magari ya Serikali ama kuweka namba za bandia za STK na kuwataka wampe fedha dereva huyo ambaye hulazimika kujitambulisha kama dereva wa waziri husika.
Aidha matapeli hao ambao hawapendi kukutana ana kwa ana na watoa fedha wakati mwingine huwapa namba ya akaunti katika benki yeyote ili fedha ziwekwe katika akaunti hiyo.

Alisema kwa utapeli huo, tayari vigogo kadhaa wa Serikali na taasisi kadhaa, zimelizwa kwa kuibiwa mamilioni ya fedha kwa njia ya utapeli.

Kamanda Kova alisema jeshi lake litaendelea na msako mkali kubaini mtandao huo mkubwa ambao tayari umeshasababisha hasara kwa makampuni na viongozi wa Serikali.

“Lazima tahadhari izingatiwe kwani ina haribu sifa kwa viongozi wetu, hivyo kila mmoja ajihadhari asikubali kurubuniwa na mtu ambaye hamjui,” alisisiza Kova.

Mbali na kuwashikiliwa matapeli hao ambao hakupenda kuwataja majina yao, Kova alisema jeshi lake limeimalisha ulinzi kwa raia na mali zao katika kipindi cha kuelekea siku kuu za Idd El Haji, X- Mass na Mwaka mpya.

“Tumeimalisha ulinzi maeneo yote ya ndani na nje ya jiji kwa kuweka vikosi maalum vitakavyokuwa vikifanya doria usiku na mchana,” alisema Kova.

Katika hali nyingine jeshi hilo limefanikiwa kuutia mbaroni mtandao wa watu wanne akiwemo mwanamke wa wizi wa magari jijini Dar es Salaam.


Kamanda aliwataja watuhumiwa wa mtandao huo kuwa ni pamoja na mwanamke pekee, Happy Mremba (20), mkazi wa Kurasini, Abdala Ulanga (30), mkazi wa Sinza, Hassani Sengo Mdoe (20), mkazi wa Tabata na Alfred Japhet Masawe (35).

Kova alimtaja Alfed Masawe kuwa ndiye kinara wa wizi wa magari, akimtumia Happy Mremba ambaye alikuwa akiwarubuni madereva kwa kuwawekea sumu ama kirevi kwenye vinywaji pindi wanapolewa achukua gari na kukimbia nalo” alisema Kova.

Kova alitoa wito kwa madereva kuwamakini na vitu wanavyopewa na watu wasio wajua pindi wanapowabeba katika magari yao.

Kwa kukamilisha zoezi zima la msako wa jeshi hilo lililoendeshwa kwa hivikaribuni, liliweza kufanikiwa kukamata majambazi sugu 15 ambao mpaka sasa bado wanaojiwa kwa uchunguzi maalum, Pia Kova alisema jeshi hilo limefanikiwa kupata bastola moja aina ya Revova Wimbly yenye namba A 38906, iliyokuwa na risasi tano kwewnye magazine.

Kova alisema watu hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.


Mwisho

No comments:

Post a Comment