Popular Posts

Saturday, November 21, 2009

kwanini Sophia Simba asifukuzwe uwaziri?

KATIKA vitu vinavyowakera Watanzania watu wazima wenye akili timamu na wazalendo wa taifa hili ni pale kiongozi aliyepewa dhamana ya kuongoza taifa anapokuwa mropokaji na mtoa maneno hovyo bila kujali heshima ya nafasi aliyonayo.

Mtu anayetoa maneno hovyo hana heshima wala haihitaji kwa sababu mara nyingi hazungumzi hoja wala maneno yenye kujenga taifa, na yenye heshima, ila ni yale yanayochochea machukizo na hasira kwa wananchi.

Ni lazima tuelewe kuwa nchi hii ni masikini, watanznaia wameteseka kwa muda mrefu, wanataabika wanataka kupata maisha safi, wanafikiri ni nani mwenye nia njema ya kutaka kuleta mabadiliko ya kiuchumi ili waondokane na umasikini unaowatesa.

Kwa hali ilivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, hawezi kuwa na heshima mbele za jamii na jamii kama ataendelea kutoa maneno ya hovyo hadaharani, dhamani yake inashuka na anakoelekea anapotea. Na kama hapotei basi analengo la kuiangamiza ofisi yake.

Kibinadamu huwezi kutamka maneno tu kila mara mbele za watu huku ukijua wazi kuwa wanahabari wapo katika aeneo hilo na kazi yao ni kutafuta habari na kuzitoa, na unajua maneno unayoyasema siyo mazuri masikioni kwa wananchi wastaarabu.


Binafsi ninamheshimu sana Mheshimwa huyu, kwani ni kiongozi wangu na katiba ya nchi inampa heshima kubwa ambayo kwa mtu unayeheshimu mamlaka za nchi ni lazima utampa heshima yake kiongozi kama huyu. Lakini anapokidhiri kwa kukiuka maadili ya viongozi hasa wangazi ya juu ya serikali kwa kutoa maneno bila kujali mbele za watu nafasi na hadhi ya Uwaziri wake inakuwa aibu na kadhia mbele za watu.

Kwanza ieleweke kuwa unapokuwa mteule halafu ukawa mropokaji unamdhalilisha hata huyo aliyemteua kuwa Waziri, pili anaidhalilisha ofisi yake, tatu anaidhalilisha Ikulu ambayo Wizara hiyo inahusika moja kwa moja.

Pia inadhalilisha mpango mzima wa sera ya taifa ya kuelekea katika kutafuta na kuboresha Utawala bora nchini. Kwani kila mtu anayetakiwa kuguswa na mpango mzima wa kuboresha utawala bora anamtazama wazuiri waker anachofanya.

Hali ilianza kujionyesha wazi wazi kuwa Simba ameanza kupoteza mwelekeo, na bila shaka anatulazimu tuamini kuwa anatumiwa na kundi la watu au anataka kuilazimisha Ikulu ifanye yale anayoyataka.

Alianza kwa kumsafisha hadharani rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kuwa aachwe apumzike na hakufanya kosa lolote katika utawala wake, hiyo haikuwa kazi ya Simba, alipaswa aziachie mamlaka zinazohusika.

Simba huyo huyo alifikia hatua ya kumtetea hadharani aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, kuwa hakuhusika kwa namna yoyote na kashfa ya rada, Sophia Simba anatamka hayo wakati akijua wazi wazi kuwa bado suala hilo lipo kwenye vyombo vya dola na linachunguzwa.

Kuhusu suala la Rada, hivi karibuni Taasisi ya uchunguzi wa makosa makubwa (SFO) nchini Uingereza imekiri kuwa bado inaendelea na uchunguzi wa kashfa ya rada na itatoa taarifa baadaye, yeye Waziri wa Tanzania anapingana nao na kudai kuwa mtuhumiwa hausiki. Hapo ni kuvuruga kazi ya uchunguzi.

Wakati wa mkutano wa Wabunge wa CCM mbele ya kamati ya rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, mjini Dodoma, Simba huyo huyo aliibuka tena na kudai kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya Richmond, naye ni mtu safi na hausiki. binafsi sinto hukumu kuwa wanahusika tunachoangalia hapa ni mamlaka zinapoingiliana.

Mtu anachunguzwa, mamlaka kama Bunge na mahakama zinaendelea na kazi zake wakati huo huo, waziri anawapongeza na kuwatetea waziwazi.

Mbali na hilo Simba ambaye ni waziri anayehusika moja kwa moja na kudhibiti ufisadi na rushwa nchini, aliwajia juu wabunge wenzake wa CCM wanaodai kuwa wanapambana ana ufisadi kuwa wafukuzwe ndani ya chama. Tena bilaq kuogopa alifikia hatua ya kutoa maneno ya mitaani ambayo viongozi wakuu wa nchi hawazungumzi hadharani.

Binafsi nimelazimika kuamini kuwa maneno hayo aliyatamka yeye kwasababu hakujitokeza kuyakanusha, aliyasema na wanahabari wayadaka na kuyaandika.

Tena wakati ambapo Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba amekuwa akilalamikiwa na wabunge wenzake na viongozi wa CCM, kuwa anashiriki katika kukiangamiza chama hicho, yeye anasimama na kumtetea hadharani ili rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa taifa wa CCM, asimguse Makamba hapa watu wanajiuliza nani anamtuma huyu Mama kufanya kazi hizo?.

Juzi katika mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) unaoendelea mjini Dodoma, alitamka bila kutoa ufafanuzi kuwa vyama vya upinzani vinafadhili chama cha waandishi wa habari Wanawake(Tamwa) katika matangazo yake hasa lile la “sindanganyiki”.

Kauli kama hizi sizizo na ushahidi wala maelezo ya kutosha zinaweza kuwa na mganganyiko na kusambabisha chuki miongoni mwa jamii, lakini jamii ni lazima ielewe kuwa huko ni kukosa uelewa.

Kinacholeta shinda na ugumu wa kumwelewa Simba ni juu ya kauli zake, hivi tangazo la “sidanganyiki’ linalowahimiza watoto wetu wa kike kuepukana na ngono za umri mdogo ili wasome na kupona na Ukimwi linahusiana nini na siasa za nchi?

Je kama Tamwa wanapewa fedha na hao wapinzani aliowasema yeye, ili wapambane na mimba za utotoni na ukimwi wanakiadhibu CCM?

Je si serikali imekuwa ikipiga kelele kila mara kuwa watu wanaowapa mimba watoto wa shule itapambana nao? Na pia imekuwa mstari wa mbele kupigana dhidi ya Ukimwi?, yeye hili linamuumiza nini?.

Kuwepo kwa Sophia Simba ndani ya Baraza la Mawaziri na kuendelea kwake kutoa maneno kama hayo kunaishushia heshima kabisa serikali ya awamu ya nne, na aliyempa madaraka hayo na inapoteza kabisa dhana ya utawala bora na maadili ya utumishi wa umma.

Huu ni mzigo kwa rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa chama, hana jinsi ni lazima aupokee kwani aliuingiza mwenyewe. Kilichobaki asafishe safu yake kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu 2010.

Inasikitisha na kuhuzunisha inapotokea kiongozi anayetegemewa kubadilisha hali ya nchi anapokubakubali kuwa sehemu ya tatizo.

Kwa hatua hiyo, Sophia Simba anastahili kupumzika uwaziri afanye kazi ya kusimama makwaani kurusha maneno kwa wanasiasa wenzake kwa sababu uwaziri ni kazi ya heshima.

Waziri hapaswi kuwa sabuni kwa watu wachafu wanaotuhumiwa hata siku moja hata kama anamaslahi binafsi na wahusika hao. Kwanza kwa kuheshimu nafasi yake anatakiwa kuwa kimya amwachie bosi wake (rais )afanye maamuzi.
0784/ 715 686575
deojkt@yahoo.com
http://www.deotemba.blogspot.com/
Mwisho

No comments:

Post a Comment