Popular Posts

Tuesday, September 15, 2009

Ngeleja ahidi kuchunguza ufisadi Tanesco

Na Deogratius Temba

WAZIRI wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, amesema atafanya uchunguzi juu ya tuhuma za ufisadi mwingine ulioripotiwa kufanyika ndani ya shirika la ugavi na umeme (tanesco) hivi karibuni.

Hivi iliripotiw akuwa kuna harufu ya ufisadi mwngine umeibuka ndani ya shirika hilo, wa sh. 1.4 bilioni, ambapo Tanesco imeingia mkataba wa bima ya afya wenye thamani karibu ya Sh3.7bilioni na kampuni ya Strategies Insurance Limited and Pharmaccess International kwa ajili ya wafanyakazi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza na Tanzania Daima, Waziri Ngeleja, alisema ndiyo anaopata taarifa za suala hilo, atahakikisha analifanyia uchunguzi wa kina mara moja na kulitolea tamko kama ni kuunda tume ya kuchunguza ijulikane.

“ Nilikuwa safari jimboni kwangu, ndiyo nimerudi leo, nitalifauatlia na kulitolea majibu haraka, kama ni kweli wamejiinghiza katika mktaba kama huo ni kosa. Bodi ndizo zenye uamuzi wa kuamua na serikali imeweka mikono wake kwenye bodi,”alisema Ngeleja.

Katika tukio hilo mmoja wa wajumbe wa bodi ya Tanesco anadaiwa kuwa ni mkurugenzi katika kampuni hiyo iliyopewa zabuni hiyo nono.

Taratibu zinataka kama mjumbe wa bodi ana mahusiano na shirika au taasisi inayoomba zabuni ya kutoa huduma au mali, atoe taarifa kwa maandishi ya kuelezea maslahi yake asihusishwe na mchakato unaohusu kampuni yake.

Mkataba huo ulisainiwa na mkurugenzi mkuu wa Tanesco, Dk Idris Rashid na Sanjay Suchak kwa niaba ya kampuni ya Strategies Insurance Limited na Consortium of Alexander Forbes (T) Ltd.

Baadhi ya watu walioshuhudia utiaji saini mkataba huo ni pamoja na mwanasheria wa Tanesco, Godson Makia na Dominic Osumo, ambaye aliiwakilisha Strategies Insurance Limited and PharmaAccess International.

"Makubaliano hayo yamefikiwa leo 25 Mei 2009 kati ya Shirika la Umeme Tanzania Tanesco (mwajiri) na kwa ubia wa makampuni ya Medical Consortium of Alecander Forbes (T) Ltd na Strategies Insurance Limited and PharmAccess International," inasema sehemu ya mkataba huo.
mwisho

No comments:

Post a Comment