Na Deogratius Temba, Kahama
MBIO za uchaguzi mkuu umepamba moto katika Wilaya ya Kahama, zaidi ya kadi mpya 10,000 zimenunuliwa kwa ajili ya kuwagawia bure wanachama wapya katika jimbo moja la uchaguzi wilayani humo.
Habari kutoka Kahama zinadai kwamba mmoja wa vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo alizinunua kadi hizo ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, Dar es salaam, na kuzipeleka wilayani humo ili zigawiwe kwa wanachama wapya katika jimbo ambalo amepanga kugombea.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwa mpango wa kugawa kadi hizo ni kuhakikisha mgombea huyo nakuwa na wanachama hai wengi kabla ya uchaguzi mkuu ujao ili kupata ushindi kwenye kura za maoni.
Pia imebainika kuwa jambo hilo limezua limezua mtafaruku miongoni mwa wanachama na viongozi wa CCM wilayani humo.
Wilaya ya Kahama ina majimbo mawili ya uchaguzi, jimbo la Msalala ambalo hivi sasa linashikiliwa na Ezekiel Mayige na Jimbo la Kahama ambalo mbunge wake ni James Lembeli.
Joto la uchaguzi katika majimbo yote mawili linashika kasi wakati katika jimbo la Kahama inadaiwa kwamba aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo hadi mwaka 2005 Raphael Mlolwa na Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja, wanajipanga kumng’oa Lembeli.
Katika Jimbo la Msalala, Maige anakabiliwa na upinzani mkubwa toka kwa wanachama watatu wa CCM, akiwamo mbunge wa zamani wa jimbo hilo ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Emmanuel Kipole, ambaye pia alikuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo mwaka 2005, na kuangushwa na Maige katika kura za maoni na daktari wa mifugo anayeishi na kufanyakazi dare s salaam dk.massele na jaji mstaafu Stephen ihema ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kujiandaa kupambana na maige.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wilayani humo wanasema kwamba pamoja na njama hizo za kupandikiza wanachama,hali ya ushindani katika majimbo yote mawili sio ngumu kutokana na wabunge waliopo sasa kuwa na nguvu za kisiasa.
Katika jimbo la kahama, wana ccm wanaosemekana wanajipanga kumngoa lembeli itabidi wafanye kazi kubwa kutokana na lembeli kuwa amejipatia sifa nyingi miongoni mwa wananchi kwa kujali hasa wapiga kura wake.Lembeli anakubalika zaidi katika maeneo ya vijiji ambako amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara na kushiriki kikamilifu katika kusukuma maendeleo vijijini.
aidha,katika maeneo ya mjini,Lembeli anaungwa mkono na wananchi wa kipato cha chini hususani wanawake wajasiriamali ambao amekuwa msaada mkubwa kwao kwa kuwaanzishia mfumo wa kuweka na kukopa wa VICOBA.
Hata hivyo,anakabiliwa na upinzani kutoka kwa vijana hasa wa mjini kahama ambao inadaiwa amewatelekeza kwa kushindwa kutekeleza ahadi alizowapa wakati wa kampeni ya uchaguzi ya mwaka 2005.
Alipoulizwa kwa njia ya simu akiwa jimboni kwake Kahama-lembeli alisema kwamba amesikia taarifa hizo na baadhi ya watu wakimtuhumu kwamba ni yeye amemwaga kadi hizo.Alisema hii ni aina nyingine ya ufisadi unaofanywa na watu wasiowaadilifu kwa chama lakini pia kwa wananchi wanaowaongoza.
“Mimi sijui habari za kadi hizo,nenda kamwulize katibu wa ccm wa wilaya lakini kama ni kweli kuna mtu au watu wamefanya hivyo-basi wananchi wa Kahama wajiandae kuendelea kuwa nyuma kimaendeleo na masikini kwa kuwa viongozi watakaochaguliwa watakuwa ni wale walionunua uongozi kwa masilahi yao binafsi au ya wale wanaowafadhili”, alisema Lembeli.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
خدمات دبى – النجم
ReplyDeleteدهان رخيص بدبى
اعمال الصباغة بدبى