Na Deogratius Temba
KWA muda wa wiki mbili sasa taifa limeelekeza macho na masikio katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Katika hali isiyotegemewa mwaka huu vyombo vya habari, wananchi na wadau mbalimbali wa siasa za Tanzania wanaelekeza nguvu katika kuangalia mwelekeo wa kinyang,anyiro cha kuwapitisha wagombea watakao shiriki katika uchaguzi huo.
Mchakato umefanyika, watu wameanza kuomba nafasi ya kugombea kupitia vyama vyao vya siasa. Taarifa nyingi zinaonyesha kuwa katika hatua hii ya awali ya kuwapata wagombea tayari kuna matukio ya kutoa rushwa kwa wapiga kura.
Wakati rushwa ikitoka, haionyeshi moja kwa moja kuwahusisha wagombea wenyewe ila wapambe wao ambao baadhi ni viongoiz wa kubwa wa serikali na wanasiasa wakubwa kama wabunge wanhusishwa.
Uchaguzi wa mwaka huu utahusha wajumbe wa serikali za mitaa, na mabalozi wa nyumba kumi kumi kwa serikali za mitaa, Wenyeviti wa Vitongoji, wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji.
Hii ni ngazi muhimu katika utawala unaozingatia mfumo wa kugawanya mafaraka na wananchi, kwani serikali inapokuwa na utawala wa serikali za vijiji /mitaa unawapa wananchi wake nafasi ya kushiriki katika maamuzi na kupokea huduma kwa urahisi.
Hawa ndiyo wawakilishi wa wanasiasa, na ni wawakilishi wa wananchi. Hawa ni mahakimu ambao wanaamua mashauri yanayowahusu wanamtaa. Ni watu muhimu ambao jambo linapowashinda wanalipeleka moja kwa moja ngazi ya juu kisheria ambayo ni mahakama.
Kwa upande wa siasa, serikali kuu inatumia madaraka yaliyopo chini (mitaa na Vijiji), kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Viongozi wa serikali hizi wanakuwa chini ya mtendaji mkuu wa wilaya ambaye anaiwakilisha serikali kuu katika kutekeleza mipango ya maendeleo katika sehumu husika, huyu ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji au wilaya.
Hawa ni watumishi ambao walijulikana kama wanajamii wanaojitolea katika kuwasaidia na kuwaunganisha wananchi wenzao wanaoishi nao katika mtaa. Ni waratibu wa shughuli zsa maendeleo na za kijamii katika mtaa. Ndiyo maana sifa za kuwa kiongozi ajue kusoma na kuandika bila kujali kiwango cha elimu.
Kuna kila sababu ya kujiuliza ni kwa nini rushwa inatumika katika chaguzi ndogo kama hizi?, sote tuna jua kuwa vyeo vinavyogombewa havina mishahara wala maslahi makubwa kama yale ambayo tumezoea kusikia viongozi wengine wakipata.
Ngazi hii ya uongozi haina marupurupu na posho za wabunge. Kwahiyo wnaanchi wanalojukumu la hujiuliza, huyo anayetoa rushwa ili awe mwenyekiti anataka nini?
Katika makala ya Juma lilopita nilieleza umuhimu wa viongozi wanaochaguliwa katika mitaa yetu. Ni lazima kuwa na msimamo kuwa viongozi wa serikali za mitaa wanaotakiwa ni wale wanaosimamia ukweli, uwazi pamoja na kuwa waadilifu.
Tumeangalia kwa hali ya leo, hapa tulipo na hali ya kisiasa ilivyo ambapo serikali inakumbwa na suala la ufisadi, na kughubikwa na matukio ya rushwa, viongoiz wengi wanasiasa wanakunmbwa na kashfa za ufisadi.
Tujiulize kama mtu anataka kumwezesha Mtu fulani awe mwenyekiti ana maslahi gani anataka kupata kutoka kwake? Nje kuna mpnago wa kutaka kuandaa mfumo wa kuendana ambo utawezesha mpango wa kulindiana maslahi?
Kuna haja ya kuangalia suala hili kwa macho ya ziada. Labda tunaweza kulazimika kuwa na mawazo kuwa kuna watu wanao ogopa kuumbuliwa kwa hiyo wanaamua kutengeneza mazingira ya kukomaza kambi na kutengeza mazingaira ya kupata watu wa kuwalinda.
Viongozi wale wale ambao wametawala kwa miaka mitano iliyopita leo wanataka kurudi katika nafasi zao. Wengine walitoa mchango mkubwa wakati baadhi yao ndiyo walioshiriki katika kuharibu maisha ya watu kwa kushirikiana na mafisadi.
Kuna haja pia ya kuuliza ni kwanini wanasiasa wakubwa kama wabunge sasa wamejikita katika vijiji vya majimbo yao wakimamazisha watu kujitokeza kupiga kura. Ni kwanini kwa mwaka huu baadhi ya wabunge wamejenga kambi katika uchaguzi huu mdogo?
Ina maana wabunge wameamua kudhamini kiongozi wa serikali za mitaa, hadi kuhakikisha anayeshinda anakuwa upande wake? Tumeona umuhimu wa kiongozi huyu, wa kitongoji au Kijiji /mtaa kwani anaouwezo wa kuhamazisha wananchi wake wasimchgue kiongozi fisadi na wakafanya hivyo.
Ndiyo maana kila mmoja wetu anapaswa kuchukua jukumu la kutumia nafasi yake ya kuwa mpiga kura kuhakikisha anamleta kiongozi safi, mwadilifu na asiye mla rushwa kwani huyo huyo ndiye atakaye kuwa wakanza kuwatetea mafisadi.
Tutambue kuwa wajumbe wa nyumba kumi, na Wenyeviti hao, ndiyo watakotumwa kugawa nyama, sukari, Khanga, na vitu vingine ili kuwarubuni wapiga kura kuwachagua viongozi wasiostahili.
Tumeona jinsi ambavyo baadhi ya maeneo kura za maoni zimeingiliwa na watendaji wakubwa wavyama, hata ngazi za wilaya. Kwa baadhi ya vyama sasa vinaonekana hata kukosa nafasi hizo kutokana na viongozi wa vyama wilaya kuingilia mchakato na kuwapandikiza watu wao.
Wananchi wamekomaa sasa kisiasa na wanapaswa kutumia ukomavu huo kutaufuta viongozi bora katika uchaguzi huo, mfumo wa kura za maruwani, au kumpitisha mgombea asiyetakiwa au asiye na sifa umepitwa na wakati.
Leo hii ni lazima tukubali kuwa ukombozi unaanzia nyumbani kama hujakombolewa kuanzia nyumbani huna maana. Silaha ya kujikomboa anayo mwananchi mwenyewe kwa kujitokeza kupiga kura na kumchagua mtu safi anayestahili siyo yule aliyenunua pombe za kienyeji au sukari.
Unapokuwa na mjumbe au mwenyekiti asiye mwaminifu, au aliyefisadi, ni dhahiri kuwa tunajenga serikali kuu yenye watu wachafu maana watakumbatiana.
0784 / 715-686575
deojkt@yahoo.com
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
Nimepita kukusalima natafakari ntarudi namalizia kunywa chai yangu kwanza
ReplyDelete