Popular Posts

Monday, July 27, 2009

Mgogoro wa ardhi Arumeru na hitoria yake

MAPEMA Mwezi Juni mwaka huu wananchi wa kijiji cha Sing’isi, wilaya ya Meru, walivamia shamba la Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) na kuharibu mali zilizokuwa shambani hapo.

Jambo hilo lilipelekea kujeruhiwa kwa watu kadhaa na wengine kukamatwa kutokana na mapambano ya wananchi na polisi wakati wa uharibifu huo, wakati baadhi ya wananchi wakiwa wamefunguliwa mashitaka, bado chanzo cha vurugu hizo kinabakia kuwa tete.

Ieleweke wazi kuwa suala la Meru, tatizo siyo Mbunge Kimaro, wala CCM, na halihusiani na siasa kama wengi wanavyofikiri, ni suala la maamuzi ya kiutendaji kutoka serikali kuu.

Munge Kimaro, amewekeza katika eneo dogo sana kati ya eneo lenye mgogoro, yeye ana ekari 50, wakati wananchi wa Meru wanalilia Ekari zaidi ya 1000.

Suala hilo mara baada ya kutokeana wananchi kufanya uharibifu limeishia kimya kimya, bila shaka serikali haipo tayari kuchukua hatua za kuangalia chanzo cha mgogoro wa wananchi wa Meru, na kuangalia namna ya kuumaliza.


Mgogoro huu wa Meru ni changamoto kwa serikali hata kama hautatatuliwa leo, lakini itambue kuwa una madhara baadaye, na kama suala hili linaendelea kunyamaziwa na sehemu nyingine pia zenye matatizo ya ardhi basi tujue kuwa litatugharimu.

Hivi karibuni kumeibuka makundi ya wenyeji Wameru yanayodai kuwa yapo katikavuguvugu la kudai ardhi yao walionyanganywa miaka kadhaa iliyopita.

Kwa mujibu wa mwanakijiji wa Sing,isi,, Yohane Simba Kimuto, yeye anasema kuwa kijiji cha Sing’isi ni kijiji ambacho kina mgogoro wa ardhi kuliko kijiji kingine hapa nchini.

Mfano shamba la Madiira, na shamba la Mito miwili farm yenye ukubwa wa ekari 1,114, yanamilikiwa na mtu mmoja, wakati kijiji hicho kina wakazi zaidi 8,000 ambao wamebanana na mifugo yao katika eneo lenye ekari 300.

Kama sio kuwa makini, suala la ardhi ya wameru ni kama la wapalesta na waisraeli, huko mashariki ya kati, kwani hili la wameru linaonekana kuanza takribani zaidi ya miaka 50, iliyopita.

Juni 30, 1952, wananchi wa eneo hilo, walimchangia marehemu Japhet Kirilo Ayo, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, nauli Pamoja na wakili wao siku hiyo asubuhi waliwasilisha malalamiko ya wananchi wa wilaya ya Arumeru, mbele ya kikao cha Baraza la udhamini cha Umoja wa mataifa huko New York, Marekani.

Malalamiko hayo ya wananchi yalipangwa kusikilizwa Julai 27,1952, mnamo Disemba 2, 1952, baraza la udhamini la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la pamoja la kuitaka serikali ya kiingereza (Tanganyika wakati huo),kuwarudishia wananchi mashamba yote ikiwa ni pamoja na kuwalipa fidia.

Katika azimio hilo waliotakiwa kulipwa fidia ni wananchi wa Ngarenanyuki,ambao nyumba, mali, mifugo, zilikuwa zimechomwa moto na jeshi la kikoloni.

Tunapojaribu kunagalia historia fupi ya mgogoro huu tunaona kuwa serikali ya Kiingereza(Kikoloni), haikuitikia wito wa UNO, hadi Tanganyika ilipopata uhuru na hadi leo, zaidi ya miaka 57, ardhi hiyo ipo mikononi mwa serikali.

Kinachochanganya watu, ni kwamba serikali ya awamu ya tatu, kwa nyakati tofauti imewahi kkubali kuyagawa mashamba hayo kwa wanachi, mfano, April 25,2003serikali ilikubali kuygawa mashamba hayo kwa wanachi kwa barua kutoka kwa mkuu wa mkoa wa arusha, yenye Kumbukumbu namba:RC/AR/CL.2/X1.

Hezron Kaaya,ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu, Habari, Teknolojia na utafiti(RAAWU) na ni mmoja wa wazawa wa Meru, yeye anasema kuwa kuna haja ya serikali kuhakikisha inayarudisha mamshamba hayo kwa wazawa.

Kaaya, anaeleza kuwa mashamba kama vile Arusha Duluti Coffee Estate, Miniots Coffee Estate,Jayami Coffee Estate,yameuzwa kw aviongoiz wa serikali na kuwaacha wananchi wakazi wa eno hilo wakiwa hawana ardhi.

“Sina tatizo na wazungu, tatizo ni utaratibu unaotumika kuyauza mashamba hayo, kwa mtazamo wangukwa mtazamo wangu,kama siyo ustaarabu wa hayati Mwalimu Nyerere, mashamba yalipaswa kutaifishwa”

“suala la kuuzwa kwa mashamba yaliyoachwa na wazungu yalipaswa, kutangazwa na siyo kuuzwa kinyemela’anasema Kaaya.

Suala hili lipase kuchukuliwa hatua muafaka, kumaliza masuala ya ardhi hasa kuangalia utaratibu wa kuuza mashamba ambayo yanawazunguka wananchi.

Kwa upande wa Meru, hakuna ardhi tena, iliyokuwepo awali imegawanywa, imemalizika, ni vigumu wao kuendela kuvumilia kuona ardhi haitumiki au mtu mmoja anamiliki eneo kubwa wakati wao hata la kunuua awana.

Ieleweke kuwa huwezi kla pialu wakati watu wanalala njaa, kwahiyo kwa hali hii huwezi kumiliki eneo kubwa kati ya watuy wasio na ardhi na wakanyamaza kimya.

Kwa mujibu wa wakazi wa Meru, ni kwamba mgogoro wa shamba la Kimaro, ulitokana na kukatazwa kukata majani ya ng’ombe, hapo ndipo hasira zikaibuka na kushambuliana.

Uchunguzi unaonyehsa kuwa kuna vuguvuku la kudai ardhi ya wameru nchi nzima mbalo linakuja na penine kama serikali isipokuwa makini hali hio itaighaimu.

No comments:

Post a Comment