Popular Posts

Monday, July 27, 2009

Heri yako Kingunge kutufungua macho

“WAPINZANI ni waongo, wazushi, na wanafiki, wanasema uongo na hawana ushahidi, hakuna kiongozi fisadi…..”.Hayo ni maneno ya Mbunge wa kuteuliwa na rais Kingunge Ngombale Mwiru, aliyoyatoa Septemba 2007, jijini Dar es salaam.

Kingunge, katika mkutano wake na waandishi wa habari, alitamka wazi wazi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, na wenzake waliojikusanya katika viwanja vya Mwembeyanga-Temeke, na kutaja oridha ya majina ya aibu (List of shame) ni za uzushi na uongo.

Katka mkutano huo Kingunge alijitahidi kujenga hoja na kuwashwishi watanzania waamini kuwa majina yale yalikuwa yametungwa na yalikuwa uzushi mtupu.

Itakumbukwa kuwa katika majina yale ya aibu, orodha ilikuwa wazi wazi, ambayo iligusa watu wengi maarufu, hadi kufikia badhi ya vyombo vya habari kuogopa kuyataja, lakini leo tunawaona wakiwa mahakamani wakituhumiwa kutumia madaraka yao vibaya sanjari na kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

Wakati Kingunge anazungumza hayo, hakuna kiongozi wa serikali wala chama cha Mapanduzi (CCM) ambacho baadhi ya makada wake wa ngazi za juu au waliotuhumiwa ambao waliojitokeza hadharani kuzungumzia suala hilo hadi walipoanza kukamatwa na kupandishwa mahakamani.

Leo hii linapotokea suala la waraka wa kanisa katoliki unaoelekeza waumini wake jinsi ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010,ulioandaliwa na Chama cha wanataaluma wakatoliki (CPT), Kingunge analitolea tamko tena kwa mara hii akiwa Bungeni

Katika historia ya kanisa katoliki, li kanisa linalokweda kwa nyaraka, au barua za kichungaji, amabzo huanzia juu na kutekelezwa na waamini wakiongozwa na mapadre na wa watawa.

Inaonekakana kuwa ni mara ya kwanza kwa waraka wa kanisa katoliki kuwasumbua wanasiasa, kwa kujitokeza hadharani kuupinga licha ya kuwa kumekuwepo na nyaraka zaidi ya 25, ndani ya miaka 20.

Wakati Nyaraka zimekuwa nyingi hivo kwa kipindi kifupi, Kingunge amekuwepo katika serikali tangu uhuru, lakini hakuwahi kulikemea kanisa na kuliambia kuwa liache kusambaza waraka wake.

Waraka wa kanisa wa Mwaka 1989 juu ya rushwa ulikuwa mkali na ulitosha kuwasambua watu wengi kutokana na kuokuzoeleka kwa changamoto za kisiasa wakati ule.

Inakuja na inalazimu watu waamini kuwa hizi ni kelele za CCM, Chama kimekuwa ikitumia wazee kama akina Kingunge, John Malecela, na wengine kuzungumzia masuala ambayo pengine wanajua kuwa yanakiangusha chama , lakini wanataka jamii iamini maneno ya wazee hao hata kama hayana ukweli.

Waraka wa wanataaluma umejenga hoja, unahamazisha wananchi kuacha kupoteza haki yao ya kutokupiga kura, kutokuuza kadi/shahada za kupigia kura, kukataa kupokea rushwa, takrima, kupokea chakula au nguo ili wampigie mtu fulani kura.

Wanataaluma wakatoliki, wameliona hilo na hasara ambayo inawakumba wananchi baada ya kupoteza haki hizo, matokeo ya rushwa ni kilio, tena cha muda mrefu.

Kanisa kwa kutumia wanataaaluma wake hasa waamini wake ambao ni wana jamii, hawawezi kuvumilia kuona nchi inaendelea kuongozwa au kupatiwa viongozi wasio waaminifu na waadilifu.

Neno rushwa leo hii limekosa nguvu, kuna neno kali zaidi ambalo ni ufisadi, “Ufisadi” unatisha, katika waraka ule wa kanisa neno hilo ambalo ni msamiati mpya wa kisasa, limetumika mara kadhaa, na nafikiri huo ndio mwiba kwa CCM.

Katika waraka ule hakuna mahali panapomtaja mtu, kiongozi, au chama chochote kwamba kisichaguliwe, isipokuwa maudhui yake ni maumivu kwa baadhi ya watu, hasa vyama kama CCM, ambavyo vimeshidnwa kijisafisha na kuwaondoa wanachama wasio waadilifu.

Ubaya wa waraka ule unaweza kuwakumba hata watu wa vyama vya upinzani kama siyo waadilifu, hasa baadhi ya vyama ambavyo vimekaa kimaslahi, na vile vinavyotetea ufisadi na kuendesha mijadala inayoelekea kulinda baadhi ya watu wasiguswe.


Tatizo la CCM na wapiga kelele wengine lipo hapa, badala ya kikisafisha chama na kutafuta watu waadilifu, watako kubalika na jamii wapewe nafasi za kugombea uongozi, leo hii chama kinaangalia matukio, pale kinapoguswa kinawatumia wazee vibaya.

Pengine Kingunge, katumwa, na vijana wake aje atikize kiberti Bungeni, alishtue Bunge,na waanchi kwa ujumla, wakati wanajua kabisa kuwa kanisa, hasa kanisa katoliki lina msimamo usiobadilika kiurahisi.

Kwa hali ilivyo sasa, huwezsi kulibadilisha kanisa, ikiwa waamini wake wanakubalina na mfumo wake ni vigumu kwa mtu kutoka nje kulisisitiza kubadili mfumo yake iliyosimama kwa zaidi ya miaka 2,000 sasa.

Kwa maneno mengine hali inavyo kwenda kauli za viongozi wa serikali, wanasiasa juu ya Waraka huo kutoa elimu ya uraia kwa wananchi zinazidi kuufanya ujulikane zaidi na kuhitajika huku watu wengi kila kona ya nchi hii wakiuhitaji.

CCM, na wanasiasa wengine wanapaswa kutambua kuwa wazee ni hazina, na hawapaswi kutumika vibaya kwa kuwatuma kuzungumzia masuala kama hayo, kama kuna aibu inayoweza kumpata mtu ni kukanusha ukweli yaani jambo la ukweli wewe unasema ni la uongo.

Bila shaka ipo wazi kuwa kama Kingunge aliona umuhimu wa kulitahadharisha kanisa kuwa waraka huo una kasoro, na kudai kuwa alishausoma wote, alipaswa kuandika maoni yake au kuandika barua ya kuelezea vipengele ambavyo ni hatari ili virekebishwe.

Kwa mtu wa kiwango chake, na heshima yake kama kiongozi mwandamizi, bila shaka angesikilizwa na waraka huo ungefanyiwa marekebisho.

Wakati Kingune akizungumzia msuala hayo, inaleta picha za wazi kuwa kuna makundi ya watu hayapendi kuguswa au kusikia vikundi vya kidini au taasisi za kijamii zikihamazisha au kuelimisha watu juu ya kuepuka maovu.

Hali hii imewafungua wananchi macho, na kutambua kuwa kumbe baadhi ya watu hawataki kabisa kusikia habari njema za kukataa dhambi ya rushwa zikihubiriwa, wanaziba masikio yao kwa pamba nzito na kuwakimbiza wanaohubiri injili ya kukataa rushwa.

Imewahi kutokea watu wanaogopa sana wahubiri, hasa wale wanaohubiri wazi wazi ukweli, wale wanaotamka hata majina ya watenda maovu, kwa mahali pengine watu kama hao, huwa wanahamishwa nchi au kufutiwa uraia.

Kulibadilisha Kanisa ni vigumu, ndiyo maana watu wanaheshimu kauli za viongozi wa kidini, watu wameelewa wazi wazi kuwa waraka huo una ukweli ndani yake na ndiyo maana umekuwa shubiri kwa viongoiz wetu.

No comments:

Post a Comment