WABUNGE wa kamati ya Fedha na Uchumi, wameitaka serikali kutoa tamko juu ya uhalali wa mkataba wa kampuni ya Kimataifa ya Kupakua na kupakia makontena Bandarini(TICTS), kutokana na kuendelea kushuka kwa utendaji wa kampuni hiyo.
Kauli hizo zilitoka jana jijini, Dar es salaam, mara baada ya makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA), Daustan Mrutu, kuwasilisha ripoti ya utendaji ya TPA, kwa wabunge ambayo ilielezea mafanikio na changamoto ambazo zimefanya mamalaka hiyo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Akizungumza Mbunnge wa Kigoma, Siraji Kaboyonga (CCM), alisema Mamlaka ya Bandari, imekuwa kimya kutokuichulia kampuni hiyo hatua wakati imeonyesha wazi wazi kuwa haiwezi kazi, na kukwamisha upatikanji wa mapato serikalini.
“Yule Bwana TICTS amekaa pale, kazi ameshashindwa nyie mnamkumbatia tu, ni kama kuku aliyekalia mayai yote wakati hawezi kutagisha, tunamwogopa nini?.
“Anatakiwa kupakua mzigo wa zaidi ya tani mil.15, kwa mwaka lakini hawezi hata nusu yake, hii nchi ni nchi moja ya ajabu kabisa katika dunia hii ya leo, tunapoteza mabilioni ya fedha kila siku kwa sababu ya kumwogopa mwekezaji,” alisema Kaboyonga, na kuongeza:
“Kama tunampenda sana TICTS kwa maana yoyote abaki kama mwendeshaji wa kawaida, na tufungue milango kwa wawekezaji wengine wenye uwezo nao watoe huduma hiyo,” aliongeza.
Alisema kuwa kampuni kama TICTS inayotoa huduma ya kupakua makontena nchini Dubai, inapakua makontena 100, kwa saa, wakati hapa Tanzania kontena hizo zinaweza kupakuliwa kwa kipindi cha wiki mbili kutokana na urasimu na utendaji mbovu.
Wabunge hao, waliokuwa wakizungumza kwa hisia za uchungu, kutokana na chini kupoteza fedha nyingi, walisema kuwa bandari ya Tanzania imebaki jina tu kwa sasa kwani wafanya bishara wengi wa ndani na nje ya Nchi hasa kutoka Uganda, Burundi, Rwanda, DRC na Zambia wameshajito kupitisha makontena yao Tanzania.
“Tanzania ni Dubai ya Afrika ya Mashariki, makampuni yote makubwa ya magari yanaweza kuja hapa yakafungua viwanda vyao kama tungetoa huduma nzuri na kuiboresha bandari yetu,” aliongeza.
Akijibu maswali ya Kaboyonga, makamu Mwenyekiti, Mrutu, alisema, tatizo la Tanzania, ni kwamba serikali imejito katika kuwekeza bandarini tofauti na Kenya ambao wameweka nguvu kubwa katika bandari zao.
Akieleza jitihada ambazo TPA wamezichukua dhidi ya utendaji mbovu wa TICTS, na kukiuka masharti ya mkataba alisema ni kweli kuwa wamekiuka mkataba lakini mamlaka hiyo haina uwezo wa kuihukumu kampuni hiyo kwani suala lake linasimamiwa na serikali.
“Ni kweli kuwa TICTS wamevunja makubalino yaliyoko kwenye mkataba hili lipo serikalini na ninaomba niendelee kushikwa na kigugumizi, sina majibu sana juu yao;”alisema Mrutu.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Happiness Senkoro, alisema kutokana na kutokueleweka kwa hatma ya kampuni hiyo, imesababisha wafanyakazi wake kugoma kwa siku kadhaa wakidai menejimenti ya kampuni hiyo iwape ukweli juu ya uwepo wa kampuni hiyo.
“Mgomo umekwisha lakini walikuwa wakishinikiza uongozi kuwapa ukweli juu ya hatma yake walitaka kujua kama mkataba wa TICTS utakoma au utaendelea tumekaa nao tukashauriana na sasa wanaendelea na kazi,” alisema Senkoro.
Naye Mbunge wa Mvomero, Suleiman Sadick Miraji,(CCM), alisema watendaji wa bandari wamkuwa na urasimu mkubwa na utendaji wao unashuka kila siku mapaka wakurupushwe na rais au waziri ndiyo wafanye kazi.
Katika ripoti hiyo bandari iliyowasilishwa jana ilionyeha kumwekuwepo na mafanikio ya kiutendaji kuanzia Mwezi machi mwaka huu baada ya Rais Kikwete alipofanyaziara bandarini hapo.
“Hawa wanataka mpaka wakurupushwe, ripoti yao imejaa maelezo tu, haya yamefanyika baada ya rais Kutembelea huko hata hizi changamoto walizozitaja hapo wanaweza kuzimaliza kama watajituma,” alisema.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakati Rais Kikwete, anatembelea bandari hiyo, kulikuwa na mulundikano mkubwa wa makontena bandarini lakini kwa sasa wamefanikiwa kuyapunguza.
Mwisho
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment