Popular Posts

Thursday, May 28, 2009

Chuo cha madaktari kinapokuwa kichafu, hatarini

CHUO Kikuu cha Tiba na afya cha Muhimbili, ni miongoni mwa Taasisi nyeti za umma, ambazo zinawaandaa wataalamu wafya nchini katika ngazi ya shahada za kwanza na uzamili.

Kwa jinsi hiyo msomi wa Shahada ni mtaalamu na tunaamini daktari anayetoka katika chuo hicho, atatumika kuokoa maisha ya watu, anapaswa kuwa mfano mzuri, wa kuigwa katika usafi na hata afya yake inatakiwa kuwa nzuri na imara ili ushauri anaoutoa kwa jamii uweze kuzingatiwa.

Hivi karibuni, uchunguzi umeonyesha kuwa hali ya usalama wa afya za wanachuo hao wa Muhimbili, zipo hatarini kutokana na kukidhiri kwa uchafu katika mazingira ya chuo.

Unapoingia ktika mazingira ya chuo hicho kiilichopo karibu kabisa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kama itakuwa imenyesha mvua. Utakutana na madimbwi ya maji machafu yaliyotwama, katika milango ya kuingilia katika ofisi za utawala, madarasani, kantini, na mabwenini,vyooni ambapo maji husimama kwa siku kadhaa na kubadilika kuwa kitu kingine.

Hali inaonyesha kuwa miundombinu ya maji chuoni hapo, imechoka na serikali imekaa kimya bila kufuatilia.

Hatari hii inawakumba wanafunzi na wakazi waishio karibu na Chuo hicho, muda wowote wanaweza kukumbwa na magonjwa ya milipuko.

Mwingiliano au kuchanganyika kwa maji safi na maji taka ni hatari kwa binadamu, katika baadahi ya mabomba ya chuo, ambayo wanafunzi wanayatumua kuchotea maji ya kunywa, maji yaka huchanganyika nayo.

Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa na kufuatilia kwa karibu mazingira ya chuo hicho wakati mvua zinaponyesha umebaini kuwa miundombinu ya maji machafu ya chuo hicho imezeeka na kuachia maji machafu ya chooni kuchanganyika na maji safi na kusambaa hovyo katika vyumba na ofisi za Chuo.

Pia imebainika kuwa mvua zinapo nyesha ni vigumu kuingia katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Kisali Palangyo, na darasa la wanafunzi wa udaktari (MD), wa mwaka wa tatu.

Mazingira ya kanteeni ya chuo, sehemu ya jikoni, nayo siyo salama, hapa kuna haja ya kujiuliza kwnaini serikali inyamze kimya mpaka watu wadhirike?.

Yahya Yusuph, ni Rais wa serikali ya wanafunzi (MUHASSO), chuoni hapo nilizungumza naye na kuumuuliza juu ya afya za wanafunzi wenzake, kutokana na kukidhri kwa hali hiyo ya uchafu.

Yeye anasema kuwa serikali yao imeliona tatizo hilo, na imefuatilia kwa uongoiz wa chuo ambako amejibiwa kuwa chuo hakina fedha za kukarabati Miundombinu hiyo.

“Ni kweli kuna uchafu kama unavyosema lakini tulisha wasiliana na uongozi wa chuo wakatuambia kuwa hakuna fedha kutokana ana bajeti kidogo kinayotengewa.

“Tunashangaa hali hii kuanchwa kendelea, muda wowote watu watapatwa na magonjwa ya ajabu hapa, hiki ni Chuo cha kulelea madaktari lakini ni kichafu vile, jamii inaona serikali nayo imenyamaza, kama ni kweli serikali haitoi fedha tunaishauri iongeze bajeti ili kukinusuru chuo na aibu hii,” anasema Yusuph.

Anasema kuwa wao kama serikali ya wanafunzi walishaandika barua kwa uongozi wa Chuo kuueleza juu ya hali hiyo na kuelezea kwa kina madhara ambayo yanaweza kuwapata wanafunzi wenzao.

Yahya Yusuf, anaeleza kuwa kuwa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, haiamini kama yanahitajika mabilioni ya fedha kukarabati miundo mbinu ya Chuo hicho.

Pia naye waziri Mkuu wa MUHASSO, Nathaniel Sirili,anapoulizwa juu ya afya za wenzake anaowaongoza anasema, baada ya hali ya uchafu kuzidi chuoni hapo, na kutafuta jinsi ya kulitatua waliamua kuandaa siku ya mazingira ambayo ilitakiwa kufanyika Mei 27, mwaka huu, chuoni hapo, lakini hata hivyo wamekwama.

Alisema chuo hicho kinaweza kugeuka muda wowote kuwa kituo cha kufanyia utafiti wa magonjwa ya milipuko kama hali hiyo haitadhibitiwa mapema.

“Hiki ni chuo cha madaktari, lakini mwisho wa siku kinaweza kugeuka kuwa kituo cha utafiti wa magonjwa ya milipuko, serikali isisubiri tuandamane kudai usafi, itakuwa aibu,” anasema Nathaniel.

Itambulike kuwa katika mazingira ya Chuo Kikuu, kama cha Dar es salaam, IFM, CBE, Duce na vinginevyo ambavyo vipo katikati ya mji, huduma zao za chakula zinatumika na wakazi au watu wote wanaofanyia shughuli zao katika eneo hilo.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa Muhimbili, wagonjwa, wageni,na hata wakazi wa maeneo hayo wanatumia huduma za Chuo na hata kula katika kantini hiyo.

Serikali kupitia wizara ya afya na Wizara ya elimu inapswa kuliangalia hili, hata kama hakuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukisaidia Chuo hiki, lakini tunaingia kwenye mwaka mpya wa bajeti 2009/2010 hivi karibuni, wanapaswa kukiangalia chuo hicho.
0784 686575
www.deotemba.blogspot.com

No comments:

Post a Comment