Popular Posts

Thursday, May 28, 2009

Kupanda kwa gharama za elimu kunakwamisha maendeleo

Miongoni mwa hoja za msingi zinazotolewa kuhusu elimu, ni umuhimu wake unaotafsiriwa kama msingi wa maendeleo ya jamii yoyote duniani. Hapa nchini, gharama kubwa zinatokana na huduma za elimu, zimekuwa sehemu ya malalamiko ya wananchi na kikwazo katika kukidhi mahitaji mengine.

Lakini Tanzania kama Taifa, imeridhia matamko mbalimbali ya haki za mtoto, likiwamo la Umoja wa Mataifa na lile la Umoja wa Afrika linalohusu haki na ustawi wa mtoto, pia unapoangalia mila na desturi za jamii mbalimbali, suala la haki za mtoto, ikiwamo kupata elimu, zinaainishwa kwa namna tofauti kulingana na mazingira na rasilimali zilizopo.

Katika ujumla wake, matamko ya haki za mtoto yanagusa masuala mengi na tafsiri mbalimbali, zikiwa na nia ya kustawisha hali bora (za mtoto) na kumjengea msingi bora hasa wa maisha ya baadaye.

Kutokana na hali hiyo, nilishawishika kuzungumza na wazazi wengi na kuwauliza je, wachukuliaje hali halisi ya gharama za elimu nchni kwa sasa? Je gharama za elimu tulizonazo leo zinzkwenda sawia na hali halisi ya kipato cha mtanzania au zinamkamua masikini na kumwacha aendelee kuwa masikini kutokna na kumpeleka mtoto shule?.

Kuna umuhimu mkubwa wa elimu kwa mtoto, na gharama anazozitumia kumsomesha licha ya kutokuwa na kipato cha uhakika, kutokana maisha ya watanznaia wengi kuwa ya kipato kisicho rasmi, wengi wanafanya biashara ambazo hawana uhakika wa kupata fedha, fundi nakwenda kibaruani, hajui atarudi nyumbani na kiasi gani cha fedha..

Wapo wazazi ama walezi wengi wenye mwamko wa kutambua umuhimu wa elimu, na kujitahidi kwa hali na mali, ili kuhakikisha wanawarithisha watoto wao elimu, kama hazina pekee iliyo endelevu katika kukabiliana na changamoto za maisha kwa kadri zitakavyojitokeza.

Hata hivyo, unapoiangalia elimu, kama sehemu ya haki za mtoto, jambo linaloonekana kutawala zaidi, ni ugumu wa wazazi na walezi kumudu gharama zinazotozwa ili kupata elimu, hasa kwa watoto.

Ukiangalia gharama za elimu kwa shule za binafsi mabzo ndizo zinazotegemewa kuwa zinztoa elimu bora, kutokna na kuingia kwenye ushindani wa kibiashara, ada ya mtoto mmoja kwa mwaka ni wastaniwa sh. 700,000, mpaka sh. 1,500,000, wakati vyo vikuu karo ya mwaka (tuition Fees),kwa shahada zote za wali (undergraduate), ninaaznia sh. 600,000 hadi mil. 2000,000, tunashindwa kuelwa hili la kulingana kwa karo hizi linatokana na kipato cha wananchi kupanda au nini?.

Wazazi, japo kwa nyakati tofauti, wanasema uamuzi wa kuwagharamia watoto hao, kupata elimu katika shule binafsi zinazotoza kiasi kikubwa cha fedha ili kukidhi mahitaji ya uendeshaji wake, unafifisha upatikanaji wa mahitaji mengine katika kaya zao.

Wakati mwingine unalazimika kuacha kugharamia mahitaji mengine katika familia, kama vile kubadili mfumo wa chakula cha kila siku, kutonunua mavazi yenye hadhi, kushindwa kuendeleza mashamba, ili mradi fedha iliyopo itumike kwa ajili ya kumpatia mtoto elimu bora.

Ni kweli kuwa Tunajinyima sana, tunatumia fedha nyingi kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, ili watakapojiunga kuendelea na elimu ya juu, wasipate taabu sana, vinginevyo si wanaowapeleka huko wana kipato kizuri, japo inawezekana kuwapo wazazi wenye kipato kikubwa, hao hawakosekani, lazima wapo.

Wakuu wengi wa shule binafsi weamkuwa wakijitetea na kueleza kuwa gharama zinazotozwa katika shule binafsi, zinakidhi mahitaji yatakayowawezesha watoto kupata elimu bora.

Wamekuwa wakisema kuwa viongozi na wamiliki wa shule binafsi, wanatambua hali duni ya maisha ya wananchi, na hivyo kuhakikisha wanashiriki kugharamia mambo ya msingi, lakini yatakayosaidia kupata elimu bora kwa maslahi ya watoto.

Katika ujumla wake, gharama za elimu zinatoa changamoto kubwa kwa wazazi katika kufikia uamuzi wa kuwagharamia watoto wao shuleni ama kuwekeza kwenye shughuli nyingine.

Lakini ukweli unabaki kuwa elimu ni hazina bora, hasa pale mtoto anapopata elimu bora, ambapo Serikali na jamii katika ujumla wake, wanapaswa kupata njia na mbinu bora zitakazofanikisha kuwapo mazingira yasiyombana mzazi ama mlezi kulipia gharama hizo.
0784/715 686575
www.deotemba.blogspot.com

No comments:

Post a Comment