Na Deogratius Temba
Baada ya wiki iliyopita kucheza santuri ya Wizara ya Nishati na Madini juu ya tuhuma ya rushwa iliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Jairo. Pamoja na kutuhumiwa waziwazi na ushahidi wa wazi kuwa amejihusisha na masuala ya rushwa bado David Jairo ni Katibu Mkuu aliyeko likizo. Yupo likizo anapokea mishahara ambayo ni fedha za walipa kodi. Hii ni nchi ya ajabu, watanzania masikini wanajifunza nini hapa? Je wanaionaje serikali yao isiyozingatia usawa katika sheria?
Je ina maana Jairo anachunguzw ana Taasisi ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa (Takukuru) kwa kuhisiwa au amekamatwa na nyaraka ziko wazi? Je anachunguza ili afanywe je?.
Wiki iliyopita vyombo vya habari na Watanzania kwa ujumla walikuwa wakijadili juu ya wizara ya Nishati na hali halisi ya umeme nchini ambao umekuwa kero kubwa. Mgao wa umeme umekuwa mwiba, mjini tunapa umeme kwa shida kijijini hali ni mbaya zaidi. Wiki iliyopita nchi nzima na hata katika safu hii, mjadala ulikuwa ni rushwa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini, jinsi ambavyo watendaji wanaendelea kujinufaisha na rasilimnali za taifa hili kwa kujilinda na rushwa na kuwaaacha Watanzania wakiwa hoi. Umeme! umeme! umeme! Ndicho kilio chetu.
Nchi ipo gizani hali ni mbaya uzalishaji umesimama, ajira simesimama, rais wetu yuko Afrika ya Kusini, baadaye amerejea akaeleekea Mtwara, lakini hazungumzii suala hilo kwasababu nchi haipo kwake tena, imeshaporwa wenye nayo ni watu wengine.
Kilichobaki kwasababu serikali imechoka na haihitaji kujiumiza, au kuhangaika na wananchi wake, inaingiza ujanja wa kuibua mambo (sanjuri mpya kila mara). Vikao vya bajeti, mijadala ya bajeti inaendelea Dodoma. Bunge kama chombo cha kutunga sheria, chombo cha kujadili masuala ya wananchi hasa mustakabali wa maisha yao linaendelea. Serikali kutokana na kuwa imeshaporwa rasilimali za nchi hii na kwa sasa haina kitu, imechanganikiwa na sasa inachokifanya ni kuzima masuala ya msingi. Bunge ambalo Watanzania waliamini kuwa ndicho chombo chao sasa limeingiliwa na serikali na linatumika vibaya.
Wakati watu wanalalamika sababu za kumpa Jairo, likozo ya malipo, yaani kuendelea kumlipa kwa kodi zetu wakati alikuwa hana nia nzuri ya kututoa katika giza hili, tena amevunja sheria. Sanjuri ikabadilika ghafla na kuwekwa ya wabunge wakizomeana, wakitukanana, wakivunja kanuni za bunge na mengine. Majadala juu ya suala la Jairo,na Waziri wake, Wiliam Ngeleja, Naibu Waziri Adam Malima kutakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa nzito ya wizara yao na pia kushindwa kuondoa kero ya umeme ikazimwa. Huu ndio ujanja pekee uliobaki serikalini.
Serikali iliyoshindwa kusimamia rasilimali za wananchi wake, ambayo imekata tamaa, imeishiwa na maarifa, inaishia kukopi hotuba za bajeti na kupesti tu. Hakluna kufikiri zaidi kitu kipya cha kuleta maendeleo. Kazi ni kutafuta namna ya kutumia rushwa kunyamazisha hoja za msingi. Kazi ni kuwasahaulisha wananchi kujadili masuala ya msingi ayanayowahusu. Serikali kama hii ipo tayariu kuanzisha hata michezo na burudani nhyin gi ili wananchi wake wacheze bure wasahau kuihoji juu ya rasiliamli zake.
Haya nciyo yanayofanyika bungeni. Serikali inatumia mbinu ya kuwavuruga hata wabunge ili wasiwe kitu kimoja katika kujadili masuala ya msingi. Tunajua jinsia ambavyo wabunge waliuangana kuikataa bajeti ya Nishati na Madini, lakini serikali hii haikuridhishwa na kitendo kile. Sasa inatumia mbinu ya “divide and rule”(wagawe uwatawale) wabunge wanagawanywa kimafungu, wanafarakana, wanajengewa chuki ikiwezekana wapigane ili wasambaratike wasipate muda wa kujadili na kuihoji serikali. Sijui kama wabunge wameligundua hili, lakini bila shaka wabunge kama John Cheyo(UDP) na Augustine Mrema(TLP) wanaelewa. Chadema, CUF na NCCR Mageuzi wanapaswa kuwa makini na hili
Leo hii bunge limekuwa kama clabu ya pombe za kienyeji kwasababu hakuna kinachoendelea wala kinachofanyika kwa maslahi ya wananchi. Malumbano yanazidi ili wabunge wapoteze muda kujadili malumbano na kuachana na masuala ya msingi baadaye tutaambaiwa kuwa muda iliisha na taratibu au kanuni hazikuruhusu kuongeza muda wa bunge.
Mfano mzuri ni Jumanne iliyopita, ambapo Waziri wa Kilimo Profesa Jummane Maghembe, alikuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti, ilipofikia sehemu ya wabunge kukaa kama kamati, muda wabunge wengi walikuwa wamekamata shilingi kwenye mshahara wa Waziri na wengi walionekana kulalamika na kuikataa bajeti ile. Cha kushangaza, Bunge lilipiga kura ya kukataa kuongeza muda ili kukwepa maswali na hoja zaidi juu ya Bajeti ya Kilimo hii ilikuwa ni aibu kwa Bunge na hatukujua walikuwa wanataka kukimbilia wapi wakati tunawalipa. Nilisikitika sana kuona wabunge wakishangalia kuwa muda wa bunge umeisha ili hali tukujua kuwa taifa hili lina changamoto kubwa hasa kwenye sekta ya kilimo hata dhana ya KILIMO KWANZA waliotuletea haieleweki ina manufaa gani kwa mkulima masikini.
Hali ya bunge sio nzuri kwasababu serikali imefanikiwa kuligawa bunge, wafanyabiahsara, wawekezaji, matajiri nao wamefanikiwa kuwateka wabunge sasa nchi yetu imeuzwa imebaki mikononi mwa wezi tutaweza kuiokoa? Kazi kwetu!! Jumapili njema!! Niachie ujumbe 0715 686575.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment