TGNP yazindua hambuzi wa sera ya Kilimo kwanza,ajira na maisha endelevu
Katika kuhakikisha Tanzania inakuwa taifa lenye kufuata usawa wa kijinsia katika umiliki wa rasilimali zake, Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) mwaka huu umefanya uchambuzi wa kina kupitia na kutoa maoni yenye mtazamo wa Kijinsia sera ya KILIMO KWANZA, na Ajira, maisha endelevu na biashara.
Muadhiri mwandamizi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa TGNP, Bashiru Ally, amesema katika uchambuzi huo kuwa kutokana na serikali kudhararu na kukipouuza KILIMO, kumesababisha kupotea kwa ajira na watanznaia kugeuzwa kuwa watumwamanamba na kunyanyaswa na wawekezaji.
“Hili ni suala la mapambano kuhusu utu na uhai wetu,adhari za kupoteza ajira ni kugeuzwa kuwa watumwa, na kudharauliwa na wawekezaji. Tujiulize nani atatuondoa ktuika kwenye minyororo hii? “ amesema Bashiru.
Mataifa ya ulaya na amerika yamefilisika kutokana na mitikisiko ya kifedha, yamehamia Afrika kuongeza uporaji ili kukuza mitaji yao. “Tuimarishe mijadala ya kijamii vijijini bila kuogopa”
Bashiru ameishauri jamii kujitahidi kupata taarifa kwa kushiriki katika mijadala ya pampoja vijijini au katika mitaa yao, ili kupta taarifa za kitu ganio kinaendela katika taifa lao, na watafute nafasi ya kutoa maoni yao. “Kutokuwa na taairfa za kutosha kunaweza kukusababisha kukusa fursa zilizopo katika nchi yako na ukakosa kukubali au kukosoa”
Mchambuzi na mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,Profesa Aida Isinika, akichamnbua sera ya kilimo anasema: “ uwekezaji wa serikali kwenye kilimo ni mdogo sana ni wa manenoi kuliko matendo kwani kasi ya kiutendaji katika kupunguza umasikini ni ndogo. Ni lazima kuongeza utendaji na kuweka mikakati endelevu inayotekelezeka”
Katika sekta binafsi fursa zipo kwenye mikopo, wkati dirisha dogo linalotajwa kuwa lipo katika benki ya rasilimali Tanzania(TIB) mkulima mdogo hawezi kwenda kukopa hapo kwani kiasi cha kukopa ni kuanzia Sh. Milioni 100 hadi Bilioni 1, na uweke amana ambazo mkulima mdogo hawezi kumiliki kama hati za nyumba, mashamba makubwa na vitu vingine.
Katika mchakato huu, KILIMO kwanza kimeonekana kama ni ajenda ya watu wakubwa wenye mitaji kwasababu, nguzo ya kwanza ya sera hiyo ni kuleta mapinduzi katika kilimo na kusababisha mapinduzi ya kijani. Wakati miundombinu yta barabra ni mibovu, kutoka shambani ili kufikia masoko ni tataizo kubwa.
Katika uchambuzi huo, Profesa Isinika anaainisha kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa kilimo nchini Tanznaia hasa kile cha wazalishaji wadogo. asilimia 74 ya ajira zote zinatokana na kilimo,asilimia 95 ya chakula kinachotumia hapa nchni kinatoakna na wakulima wadogo,asilimia 30 ya biadhaa zinazouzwa nchi za nje zinataka kwao, asilimia 65 ya malighafiu zinazotumika viwandani hapa nchini.
Asilimia 9o ya chakula kinachozalishwa kinatokana na wakulima wadogo wakati 99 ya ardhi inayolimwa inalimwa na wakulima wadogo wanawake wakiwa ni nusu ya wakulima wadogo.
Pia katika kuzalisha, KILIMO KWANZA kinataka kuwepo na viwanda vya mazao, wakati taifa linatatizo kubwa la upoatikanaji wa umeme wa uhakika, mikoa mingi ay wilaya zinazolima kama vile Namtumbo na Songea Vijijini hawana nishati ya umeme ya Gridi ya Taifa, kwani wakati mafuta ya mitambo yakipanda bei kila mara wao bado wanatumia umeme wa majenereta yanayotumia mafuta
Mwanaharakati mwingine Amina Mcheka amesema kuwa sera ya kilimo kwanza haiajamsaidia mkulima wa chini, maeneo ya kulima yenye maporio yameachwa bila kuwagawia wananchi, wakulima amabo wanamiliki ardhi nzuri wananyang’anywa na kupewa wawekezaji.
Marjorne Mbilinyi anasema kuwa serikali inatakiwa kuelewa kuwa ajira ni kupaumbele kwani hatuwezi kuzungumza habari ya kupunguza umasikini bila kuzngumzia ajira. “katika kilimo wafanyabiashara wakubwa wamekuja na mbegu zilizopunguzwa vinasaba, wafanyabiasahara wa makampuni makubwa wamegeuka kuwa wauaza mbolea, pembejeo za kilimo, dawa; hii inaonesha jinsi ambavyo mfumo wa ubeparfi umeingia kwenye kilimo na kusambabsha tabaka kubwa” anasemna Marjorine
Tom Laizer kutoka Muungano wa Vikundi vya wakulima(MVIWATA) Morogoro anasema kuwa mapngao wa kilimo kwanza umezinduliwa bila kuwaeleza wananchi jinsi ya kupoata taarifa na fursa za kilimo. Wanaopata ni wawekezaji pekee.amesmea neon mapinduzi ya kijani ni neno ngumu ambalo sii kila mkulima anaweza kulizungumzia. “ Kilimo kwanza ni mpango wa kuwafukuza wakulima wadogo masikini kutoka kwenye ardhi yao na kuwapatia wageni, kwani kwa miaka ya hivi karibuni inaonekana kuwa migogoro ya ardhi inaongezeka.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
steroid satın al
ReplyDeleteheets
ZM0LHP