Popular Posts

Wednesday, May 26, 2010

‘Mikopo elimu ya juu yazidi kubanwa’

*Watakao soma sayansi ndio watakao kopeshwa 100%
*Mamia ya wanafunzi hatarini kukosa mikopo
Na Mwandishi Wetu,
WAKATI wahitimu wa elimu ya sekondari wakijiandaa kujaza fomu za kuomba vyuo vya elimu ya juu na mikopo kwaajili ya mwaka wa masomo 2010/11, masharti kwa wakopaji yamezidi kuonbgezeka.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) George Nyatega, iliyopatikana katika Tovuti ya Bodi, watakaokopeshwa asilimia 100, mwaka huu ni wale watakaosoma kozi za masomo ya sayansi pekee katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
Tofauti ya miaka mingine ambapo Bodi imekuwa ikikopesha wanafunzi wanaochukua kozi za sayansi ya jamii, sanaa na biashara kwa asilimia 100, kwa kuzingatia uwezo wa mwanafunzi husika mwaka huu vyuo ambavyo havina kozi za sayansi havitakuwa na wanafunzi watakaokopeshwa kwa asilimia hiyo.
Nyatega ameeleza kuwa Bodi imemua kutoa mikopo kwa wanafunzi watakao chukua kozi za sanyansi kwa asilimia 100, ya gharama za chuo husika ili kuongeza ari ya Watanzania wengi kusoma kozi hizo zenye wataalamu adimu nchini.
“ Katika mikopo ya mwaka huu Bodi inaweza kutoa karo kwa asilimia 10 hadi 100, kwa kufauta gharama zinazotozwa kwa vyuo vya umma na binafsi, na kwa kuzingatia aina ya programu ya msomo atakayosoma”amesema.
“Kiwango cha juu ya sh. Milioni 2.6 , kilichowekwa kama ukomo wa karo kwa vyuo vinavyotoa kozi za sayansi mitatu iliyopita ndicho kitakachotumika mwaka huu wa masomo 2010/11. hii ni kutokana na kukua kwa mahitaji ya mikopo na uchache wa fedha katika bajeti ya Bodi,”.
Amesema hata hivyo kwa wanafunzi watakaosoma kozi nyingine za sayansi ya Jamii, Biashara na nyinginezo bodi itaendelea kutoa mikopo kwa kufuata kiwango cha ada cha mwaka wa masomo 2008/2009, bila kuangalia kama vyuo hivyo vimeongeza karo zake kwa kipindi cha mwaka wa masomo wa 2010/2011 na bila kuzingatia kama ni mwanafunzi anayendelea na masomo au anayeanza.
Kwa upande wa fedha za kufanya mazoezi ya vitendo amesema Bodi itatoa kiasi cha sh. 10,000, kwa siku 56 tu kwa kuzingatia matokeo ya uwezo wa mkopaji (Means Testing), na fedha hizi zinaweza kutolea kwa kuanzia kiwango cha asilimia 10 hadi 100, kwa programu zote zinazohitaji kufanya mazoezi ya vitendo kama ilivyopendekezwa na Chuo husika na kuridhiwa Tume ya vyuo Vikuu (TCU).
Aidha kwa kufauta utaratibu wa kutoa mikopo kwa kuzingatia uwezo wa muombaji bodi pia itatoa fedha kwa mahitaji maalumu ya vitivo (Special Faculty
Requirement), kwa kuanzia asilimia 10 hadi 100. Hii itafanyika kwa utaratibu wa kuangalia programu zinazohitaji kulipiwa fedha hizo kama ilivyoanishwa kwenye utaratibu wa vyuo vikuu vya umma.
Kwa mujibu wa utaratibu huo mpya wanafunzi watakaopewa mikopo kwa ajili ya utafiti ni wale waakaosoma kozi zilizopendekezwa na bodi tu ambazo ni Udaktari wa binadamu, wanyama, upasuaji wa meno na uuguzi.
Kozi nyingine ni Ufamasia, uandisi, usanifu majengo na kilimo.
Masharti mengine kwa mikopo mwaka huu ni wanafunzi watakaojisajili ziadi ya mara moja katika vyuo vikuu vya elimu ya juu kutokukopeshwa.
“ Kwa muda wote tangu Bodi ilipoanza kazi miaka mitano iliyopita imekuwa ikikumbana na tatizo la wanafunzi kujisajili katika vyuo zaidi ya kimoja, hali hii imesababisha mlalamiko makubwa ya wanafaunzi ni kuhusu kucheleweshewa mikopo na mikopo kutopelekwa katika vyuo wanavyosoma”
Mipango iliyowekwa ya kupambana na tatizo hili ni kwamba Bodi haitatoa mkopo kwa mwanafunzi yeyote wa elimu ya juu atakayekuwa amejisajili au amesajiliwa katika Chuo vyuo viwili.
Kwa upande wa wanafunzi wanaohama kutoka chuo kimoja kwenda kingine watachelewa kupata fedha zao za mikopo hadi fedha za kwanza zitakazo kuwa zimeelekezwa kwenye chuo alichosajiliwa awali zitakaporejeshwa bodi.
Kutokana na hilo, Bodi imeeleza kuwa watakaokuwa na sifa za kupata mikopo ni wale ambao majina yao yatawasilishwa Bodi na TCU pekee na sio vyuo ili kudhibiti kulipa waliojisajili mara mbili.
“Orodha itakayozingatiwa na kufanyiwa kazi ni ile itakayowasilishwa Bodi na TCU au NACTE pekee, majina yeyote yatakayowasilishwa na Chuo moja kwa moja kwenda bodi hayatafanyiwa kazi au kukubaliwa kama orodha ya waombaji wa mikopo,” ameleeza Nyatega.
Wanafunzi 30,246 waliomaliza kidato cha nne Novemba 2008, na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano, ndiyo waliohitimu mwaka huu na wanatarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini baada ya kuhitimu kidato cha sita.
mwisho

No comments:

Post a Comment