Na Deogratius Temba
FEBRUARI mosi mwaka huu Shirika la umeme nchini (Tanesco), lilizindua wiki ya ‘Tanesco’ sambamba na mkataba wa huduma kwa wateja.
Tutanambua kuwa hadi leo, shirika pekee linalotoa huduma ya kuzalisha na kusambaza umeme nchini ni Tanesco, huwezi kupata nishati hiyo mahali pengine na kuitumia kihalali bila kupitia Tanesco.
Sheria ya umeme iliyokuwa ikitumika ilikuwa ikiitaja Tanesco kama mzalishaji pekee na msambazaji wa umeme nchini, hii iliongeza ukiritimba wa kuapata umeme, umangi meza uliijaa Tanesco na kuijona kama mwisho wa matatizo.
Sasa sheria mpya ya umeme ya mwka 2008, iliyopitishwa naBunge imekaribisha wawekezaji binafsi kutoa huduma ya kuzalisha umeme na kuihuzia Tanesco. Bila shaka hii inaweza kuondoa ukiritimba na kuchokoza Tanesco au kushtua kutoka usingizini ili iboreshe na kuimarisha huduma zake.
Kwa sasa huduma za Tanesco zinakwamishwa na rushwa, hali kadhalika wizi wa mafuta ya transifoma, kwani shirika linajiendesha lenyewe kifedha, kila kitu kipo, vitendea kazi vinaridhidha isipokuwa baadhi ya miundombinu ya kusafirishia umeme hasa kwenye gridi ya taifa ambayo inahitaji ukarabati kidogo ili kudhibiti upotevu wa umeme.
Doa lingine ambalo linaitia aibu Tanesco ni jinsi ya kudhibiti mafundi uchwara wasio na taaluma ya umeme lakini wanawanganishia wateja umeme mitaani kinyume na sheria. Vishoka hawa hawa ndiyo wachokonuzi wa mita za wateja na kuwafanya wateja kutumia umeme ambao haupiti kwenye mita. huu ni wizi na ni uhujumu uchumi.
Tanesco haiwezi kujiendesha kama itaibiwa, kwani fedha zinazolipwa na wateja ndizo zinazotumika kununua umeme kutoka katika vyanzo vingine kama ule unaotokana na gesi wa Songas, ule ya Mitambo ya mafuta ya IPTL, na vyanzo vingine.
Katika uzunduzi huo, Waziri mwenye dhamana na Nishati nchini, Wiliam Ngeleja, aliwaambia wafanyakazi wa shirika hilo, kuwa kama wanataka kutoa huduma bora kwa wateja wao ni lazima waondokane na tabia ya kudai na kupokea rushwa ili watekeleze vizuri mkataba wa huduma kwa wateja uliozinduliwa.
Ngeleja anasema vitendo vya rushwa vinavyofanywa na wafanyakazi vinalipaka matope shirika hilo na kulipunguzia heshima mbele ya jamii.
Kwa Mujibu wa utafiti uliofanywa na asasi ya Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA), imelitaja shirika hilo, kuwa wanaongoza kwa kuomba na kupokea rushwa. Wakati polisi na Mahakama zilifuata nyuma ya Tanesco. Waziri Ngeleja anaeeleza kuwa hilo ni doa na linatakiwa kusafishwa mara moja
Waziri anawataka wafanyakazi hao wa Tanesco kuhakikisha wanakuwa mfano bora katika utendaji wao na kuepuka vitendo hivyo vya rushwa.
Anasema kuwa rushwa inawanyima masikini huduma na kama mkataba wa huduma kwa wateja utazinduliwa halafu rushwa ikaendelea kuwepo ni dhahiri kuwa jamii inayotegemea kupata huduma za Tanesco itaikosa. Shirika linasemwa vibaya na watu wengi kutokana na huduma yake isiyoridhisha.
Anasema : “Hii si kwa bahati mbaya bali inatokana na unyeti wa shirika katika maisha ya wananchi hata wale ambao si wateja wenu wa moja kwa moja,”
Mkataba wa huduma bora kwa wateja kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Steven Mabada, una umuhimu kwa wateja na wananchi kwani unaainisha haki na wajibu wa mteja na pia wajibu na haki za shirika hilo kama mtoa huduma.
Mabada anasema kuwa mkataba huo pia unaongeza uwazi wa jinsi Tanesco itakavyotekeleza shughuli za kutoa huduma na nini mteja atarajie kutoka kwa shirika hilo.
Ngeleja akielezea mkataba huo, anasema zipo changamoto nyingi ambazo shirika hilo linatakiwa lizishughulikie ikiwemo kufanya matengenezo ya mfumo wa usafirishaji na usambazaji ili huduma nzuri ipatikane kwa wateja.
Anazidi kueleza kuwa Tanesco inatakiwa kubuni njia za kupunguza matumizi ya umeme kama vile kuwahimiza wateja kutumia vyombo vyenye kutumia umeme kidogo zaidi na ufanisi.
Waziri ngeleja, pamoja na hayo anawataka wafanyakazi wa Tanesco kuhakikisha wanatoa elimu kwa wateja kuwakumbusha wajibu wao na stahili zao katika mkataba huo.
“Kama mnataka kutoa huduma bora, kwa wateja wenu ni lazima watumishi wabadilike kwa kuepuka vitendo vya kuomba na kuchukua rushwa kwani hali hiyo inatia aibu na fedheha shirika na kurudisha nyuma juhudi za wanajamii katika kuweka nishati hiyo muhimu ya umeme kwenye sehemu zao za kuishi,” anasema Waziri Ngeleja na kuongeza
“zamani shirika hili liliheshimika sana hadi nje ya nchi, lakini leo, kuna kundi la watu wanalitia aibu, hawa wala rushwa, vishoka ni lazima muwatoe , ili muondokane na aibu hii. Hatuwezi kuwabeba hawa halafu hata huduma nzuri tunayoitoa kw awatu ikakosa kuonekana”
Inaelezwa kwamba Tanesco kuanzia mwaka 2006 hadi 2008, imekuwa na mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kuongeza wateja kutoka wateja 28,000 hadi kufikia wateja 57,000.
deojkt@yahoo.com
0784/ 715 686575
Mwisho.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment