Daudi Mwakawago mwanaisiasa jasiri aliyepingaia ukweli
* alisisitiza kuwa mahakama haiwezi kumsdafisha mtu
*Alilia viongozi kuwa na wajibu wa kuwajibika
Na Deogratius Temba
FEBRUARI 25, mwaka huu haitasahaulika katika maisha ya wanafamilia wa Balozi, Daudi Ngleutwa Mwakawago na marafiki zake. Pia kwa Watanzania wote wazalendo na wapenda amani ya taifa hili.
Unaposiki jina la Balozi, Mwakawago, sio jipya au geni kwani ni mtu aliyelitumika taifa kwa kipindi kirefu katika nyadhifa mbalimbali na kuliwakilisha taifa nje ya nchi kama balozi. Akiwa nyum,bani baada ya kupumzika amekuwa msitari wa mbele katika kulitetea na kulipigania taifa kwa kukemea waziwazi jinsi ambavyo taifa linaendeshwa na wajanja. Hakuogopa kutamka bayana kuwa mafisadi wafukuzwe kazi au nyadhafa zao serikalini.
Ameonyesha kuwa kwake taifa mbele na maslahui baadaye, unapofika nyumbani kwa balozi Mwakawago, Msasani Maduka mawaili, Kinondoni Dar es salaam, huwezi kuamini kama ndiyo makazi ya Balozi au waziri Mstaafu.
Balozi Mwakawago, atakum,bukwa kwa ujasiri wakle kutokuogopa kuwa wazi kukosoa na kusema ukweli pale anapoona viongozi wenzake wa kisiasa wanafanya madudu.
Mwaka jana pamoja na kuwa yeye alikuwa Katibu Mtendaji wa pili wa chama Cha Mapinduzi(CCM), aliwashauri viongozi wa serikali wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe katika nafasi wanazoshikilia kwa sasa ili kupisha uchunguzi huru kuhusu madai hayo.
Balozi Mwakawago alikuwa hodari wa kusema bayana bila kuogopa kuwa yeye ni mtumishi wa serikali mstaafu, alisema wale wote ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi kwanza wanapaswa kujibu tuhuma zinazowakabili na baada ya hapo wajiondoe katika nyadhifa zao ili uchunguzi huru ufanyike.
Alisema ili kuimarisha utawala bora nchini, ni wakati muafaka sasa wale ambao wametuhumiwa kwenda kwa Rais ambaye amewateua na kumueleza haja yao ya kujiondoa katika nafasi wanazoshikilia.
"Tujenge utamaduni wa uwajibikaji, wanatakiwa waende kwa aliyewateua, wamweleze kwamba wametuhumiwa na wameamua kukaa kando ili uchunguzi huru ufanyike. Wananchi wanawaangalia, wananchi sasa wanajua haki zao kuliko huko nyuma, viongozi lazima wafahamu hilo, pia wanafahamu dhana ya uwajibikaji kuliko hapo zamani” hii ni moja ya kauli zake za mwishoni kabla ya kufariki.
Katika mahojiano yake na gazeti moja alisema kwa wale ambao wana dhana kwamba Mahakama itawasafisha wanajidanganya kwani katika siasa hakuna ushahidi wa Mahakama, na hata wakisafishwa na vyombo vya sheria bado wananchi wataendelea kuamini tuhuma hizo ni za kweli kwa kuwa bado wamekalia nyadhifa ambazo wametuhumiwa wakiziongoza.
"Ni kweli Mahakama inaweza kukusafisha, lakini pia ni vema kuwa makini maana ukienda Mahakamani, unaweza kuvuliwa nguo zaidi, tuhuma nyingi zaidi zinaweza kuibuka. Mahakama si mchezo itaenda kila eneo na mambo mengi yanaweza kuibuliwa," alisema hayo wakati wa uhai wake.
Kuondoka kwa Mwakawago, ni pengo ambalo taifa hili lililokidhiri kwa kila aina ya uchafu wa ufisadi, rushwa na unafiki wa kisiasa linaupata kwani wazee kama hawa ndiyo waliotakiwa kukemea. Hatuna wazee wengi wa kudiriki kusema kwani wengi wanogopa kutishiwa au kusimamishiwa mafao yao ya pensheni wanayolipwa serikalini.
Ni masikitiko makubwa sana tumepotelewa na mzee muadilifu. Hawa ndio wale wazee ambao walitoa kafara maisha yao kwaajili ya taifa la Tanzania. Hawakupatikana hata na doa lolote litakalomzuia asipewe nafasi ya kitaifa kuhudumia Taifa.
Wazee kama hawa, laiti wangekuwa na uroho wa madaraka, kwakweli ndiyo hasa ambao tungewahitaji wangekuwa viongozi wa leo katika kipindi kibaya cha uroho wa pesa kama hiki.
Tanzania tunahitaji watu kama hao. Wamekufa masikini wa mali, lakini wamekufa wakiwa matajiri wa Roho na uaminifu.Ndiyo historia aliyoiacha huyu mzee Mwakawago. Nchi yetu ili iendelea kusonga mbele inabidi mioyo yetu ibadilike iwe kama ya hawa wazee wetu.Watu waliojitolea maisha yao kuishi kama watu wa kawaida tu bila kujilimbikizia mali. Mzee Rashid Kawawa, Mzee Mwakawago na Mzee Julius Nyerere mwenyewe, ni wa Tanzania ambao historia yao inabidi isimuliwe kwenye vitabu waisome dunia nzima.
Hatuwezi kulalamika wakati Mola anaamua kumchukua kiumbe chake. Kwa sababu kifo siyo balaa wala siyo laana, bali ni majaliwa yake Mola na kifo ni faradhi. Bila kifo hatuwezi kwenda kupumzika mbinguni, kifo ni mlango ambao tumejaliwa wote kuupita lakini kila mwanaharakati wa uzalendo wa taifa hili, anapaswa kujitambua kuwa amempoteza Baba.
Mambo aliyoyasisitiza kila mara.
Daima Marehemu Balozi Mwakawago, alisisitiza katika mambo manne muhimu ambayo tunapaswa kuyajifunza na kuona kuwa yanaifanya Tanzania kutofautiana na nchi nyingine. Mambo hayo ni; Lugha, anasisitiza kuwa lugha ya Kiswahili ni muhimili wa kuunganisha watanzania tangu kabla ya uhuru hadi miaka zaidi ya 45 ya uhuru. Anasema nchi nyingine hazina utamaduni huo na hii ni zawadi.
Hakuna ukabila, Marehemu alikuwa akisisitiza kuwa Tanzania inatofautina pia na mataifa mengine kutokana na kutokwepo kwa ukabila. Hakuna unyanyasaji na ukandamizaji, umangi umafutwa na watu wanaishi na viongozi wa kidemokrasia waliowachangua wenyewe. na Uongozi, ambapo anasema kuwa watanzania wamejaliwa karama ya kuongoza tofauti na mataifa mengine hakuna mtu anayeogoza kwa ubabe au kutumia mbinu za kidikteta.
Kila mara balozi alikuwa akionyesha kuwa hajachoka na akichoka anasema kuwa kuwa amechoka lakini bado ana nguvu.
Wasifu wa marehemu Daud Mwakawago
Marehemu alizaliwa Sepetemba 19, 1939 kitongoji cha Wende, Kijiji cha Tanangozi Iringa vijijini. Alisoma shule ya msingi ya Mlandege iliyoko Iringa Mjini kati ya mwaka 1947 hadi 1953.
Elimu ya Sekondari, balozi Mwakawago aliipata katika shule ya sekondari ya Malangali, Mufindi, Iringa na baadaye shule ya sekondari ya kati (Middle School) ya Tabora 1958 hadi 1959.
Marehemu alipata elimu ya Chuo katika Chuo Kikuu, cha Makerere nchini Uganda kati ya mwaka 1960 hadi 1963 ambapo alitunukiwa shahada ya Elimu, (BA. Edu), Vyuo vikuu vingine ni Upasla nchini Sweden, Manchester, Uingereza na baadaye alitunukiwa shahada ya Udaktari wa heshima (PhD), na Chuo Kikuu cha New Stomesinre cha Marekani.
Kazi alizofanya balozi Mwakawago
Marehemu balozi, Mwakawago alikuwa mkufunzi katika chuo Kikuu cha TANU, Kivukoni mwaka 1965 hadi 1970, ambapo mwaka 1970 aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, hadi alipokwenda kugombea Ubunge wa jimbo la Iringa Vijijini mwaka 1970 hadi 1990.
Akiwa Mbunge aliendelea kuwa Kivukoni na mwaka 1971 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo hicho, hadi mwaka 1972.
Mwaka 1972, Marehemu aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari na Utangazaji hadi 1977, mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa waziri wa habari na Utamaduni, Mwaka 1983 hadi 1987 Waziri wa Maendeleo ya Vijana na Utumishi, na mwaka 1991 hadi 1994 alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Mwaka 1991 hadi 1994 alikuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, mwaka 1994 hadi 2003 alikuwa balozi wa kudumu wa umoja wa mataifa, kazi ambayo kwa sasa inafanywa na Balozi Augustine Maiga. na baadaye mwaka 2003 hadi 2004 aliteuliwa kuwa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa(UN), nchini Siera Leone.
Baadhi ya matukio aliyowahi kushiriki.
Marehemu aliwahi kuwa mwenyekiti wa kundi la 77, (Group of 77) ambalo linawakilisha nchi zinazoendelea katika vikao vya umoja wa mataifa hasa katika masuala ya maendeleo.
Alikuwa pia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa mwaka 1996 hadi 2000, Mwenyekiti kamati ya mambo ya nje ya Bunge mwaka 1989 hadi 1990, Mwenyekiti wa mkutano wa Kimataifa wa amani na usalama wa nchi za kusini mwa Afrika 1989 hadi 1990.
Simu. 0784/ 715 686575
Inapatikana pia: www.deotemba.blogspot.com
Mwisho
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment