Popular Posts

Monday, January 25, 2010

Ripoti ya Maaskofu, Masheikh kuhusu hali ya migodi ya madini Tanzania -4

Na Deogratius Temba

KATIKA mfululizo wa ripoti hii ya maaskofu, mwishoni mwa mwaka jana tuliishia katika sehemu ya tatu, ambapo viongozi hao wa dini waliangalia hali ya ukuaji wa uchumi unaozingatia utu wa binadamu katika migodi yetu.

Wiki hii ripoti hiyo inagusa sehemu ambapo viongozi hao wa dini walijadili kwa pamoja na wananchi kuu ya tathimini na fidia ya mali za wananchi wanaozunguka madini, bila shaka mawazo na maoni ya viongozi hao, yanaweza kushadiana na ile ripoti ya Tume ya Rais ya kupitia mikataba ya madini, maarufu kama (Tume ya Jaji Bomani) ya mwaka 2007.

“ Mtakatifu Augustino aliwahi kusema ‘Hisani haiwezi kuwa ni mbadala wa haki ilioyonyakuliwa au haki iliyonyakuliwa haiwezi kufidiwa kwa hisani’ wazo hili lina nguvu katika mazingira ambayo misaada hutolewa kwa wahitaji badala ya haki wanayostahili kulipwa.

Hata hivyo mahitaji hayana budi kuthibitishwa kwa mujibu wa haki ya muhitaji. Ufidiaji katika maeneo ya madini, japo umefanywa kwa baadhi ya watu bado fidia hiyo ni tata. Wengi kati ya walipewa fidia hizo hawajaridhika; swali tulilokumbana nalo, sana katika ziara yetu lilionyesha hamu ya watu kutaka kujua kama fidia hizo zilikuwa ni hisani au ni haki yao kwa mujibu wa sheria.

Mchakato wa tathimini na ulipwaji wa fidia katika maenmeo tofauti

Watu waliohojiwa walieleza kuwa kigezo cha ulipwaji wa fidia hakikuwa wazi. Katika kijiji cvha Katoma, wilayani Geita, mgomba mmoja ulitathiminishwa kwa sh. 11,000. Thamani hiyo iliotokana na viwango vya mwaka 1974. watu wengi walilipwa wastani wa fidia y a sh. Milioni mbili. Katika zoezi hili mkazi mmoja aliyeondolewa katika eneo lake alilipwa sh. 400,000 kwa ardhi yake yenye ukubwa wa nusu hekari pamoja na nyumba, migomba na mihogo.

Katika kijiji cha Kakola, huko Kahama watu walilipwa kati y ash. 35,000 na 200,000. Elias Mujiga, aliueleza ujumbe kuwa alilipwa sh. 66,000 kama fidia ya nyumba yake , nyumba ya kulala wageni yenye vyumba 22 na bustani ya mapapai. Ni wazi kwamba hakukuwa na uwazio katika zoezi hilo.

Katika maeneo mengine waliokuwa na mali kama vile walipewa viwango totafuti vya fidia. Pamoja na viwango tofauti ujumbe ulielezwa kuwa baadhi walilipwa usiku nje ya ofisi badala ya muda wa kawaida wa kazi.

Kwa upande mwingine wakazi na wachimbaji wadogo wadogo, wa kijiji cha Kakola walisema kwamba hakukuwa na utaratibu mzuri wa kulipa fidia. Ni watu 44 tu waliopewa fidia hiyo, na fidia yenyewe haitoshi kuwafanya waishi maisha yao ya kawaida.

Kulikuwa pia na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu uharibifu uliosababishwa na shughuli za madini. Katika kijiji cha katoma wilaya ya Geita, ujumbe uliona nyumba zilivyoharibiwa kutokana na mtikisiko uliosababishwa na milipuko inayotoka katika machimbo ya madini ya Geita.

Huko nyamongo, Tarime watu walieleza kwamba milipuko inayotokana na barudi kwenye migodi imekuwa ikirusha mawe angani na kudondokea nyumba zao. Hakuna fidia yoyote waliopewa kutokana na tatizo hilo badala yake ilisememekana kwmaba mmiliki w a kiwanda cha kuchambua pamba cha Copcot Ginnery kilichopo mkabala na lango la kuingilia lango mkuu la mgodi ndiye hulipwa fidia kila mara kunapotokea milipuko migodini na kuadhiri mali zake.

Wakati huo huo kuna familia saba zinazoishi nje kidogo ya lango hili, famiali hizi nazo zinapata vumbi lote la mgodini pamoja na usumbufu mwingine unaotokana na shughuli za uchimbaji wa madini hiyo inatokana na wao kukataa kuhama bila kulipwa fidia.

Pale nyamongo, Tarime wakazi wake hawakuridhishwa na tathimini iliyofanywa kwa mali za mashamba. Viongozi wa vijiji wanashutumiwa kwa kuwashawishi watu kukataa kuhama. Hata hivyo kuna watu walikataa kuhama na wanaendelea kuishi jirani sana na mgodi hali ambayo kimsingi ni hatari sana kwa maisha yao.

Kama ilivyokuwa huko mara, katika kijiji cha Nyakabele, kiasi cha kama watu 110 ambao mashamba yao yalithaminishwa ni watu 39 tu ndiyo walipata fidia na watu 71 bado wanaendelea na kusubiri na hawajui kama watalipwa au la.

Suala hili la Nyakabale lilifikishwa kwa aliyekuwa waziri Mkuu Edward Lowassa alipokuwa katika ziara yake Geita mkoani Mwanza, septemba 2007, aliamuru mwekezaji kulipa fidia kabla ya mwezi Desemba 2007, lakini hadi tunaimaliza kazi hii machi 2008 hakuna kilichokuwa kimefanyika.

Watu waliohamishwa katika maeneo yao bado wanasubiri kulipwa fidia, wana kijiji pia wanalalamika kuwa eneo lote lisilopimwa linamilikiwa na mwekezaji kwani mpaka unapanuliwa kila siku.

Maelezo kama haya yalitolewa hata huko tarime, kwani wakazi wa eneo hilo wawajui mipaka halisi ya eneo la mgodi. Kwa mujibu w a wakazi hao mgodi unapanuka mara kwa mara hakuna hata kiongozi mmoja aliyekuwepo mkutanoni pale aliyekuwa akijua mipaka halisi ya mgodi. Kama alivyosema mkazi mmoja wa kijiji cha matombo kuwa kampuni ya uchimbaji madini kila mara hupanua eneo lake. “ wanachukua mashamba yetu maeneo yetu ya malisho ya mifugo barabara na kila kitu,”

Inaonekana kana kwamba wawekezaji wana haki na popote pale ilipo dhahabu. Wanakijiji wamekuwa wakijiuliza swali kuwa ni lini basi wawekezaji hawa wataweka uzio kuzunguka eneo la mpaka walioruhusiwa kisheria?
Itaendelea wiki ijayo…………
Simu 0784/ 15 686575
Ripoti hii Inapatikana pia kwenye
www.deotemba.blogspot .com
Mwisho

No comments:

Post a Comment