Popular Posts

Thursday, December 17, 2009

Wanaomkosoa JK ndiyo wanaomsaidia

KWA kipindi cha takribani miaka miwili na nusu utawala wa raia Jakaya Kikwete, umekuwa ukikosolewa na wanasiasa mbalimbali, wanaharakati na wanahabari kuwa utendaji wake usuasua au kulegalega.

Pengine wakosoaji wamekuwa wakieleza kuwa baadhi ya wasaidizi wa rais mdiyo kikwazo cha maendeleo, na kjukiidhiri kwa vitendo vya uvujivu na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wanaomkosoa rais Kikwete kila mara wanakuja na hoja zao za wazi wazi na kuziweka mezani kuwa rais ameshindwa kufanya hivi na vile, wanatoa njia na suluhisho ili afanikiwe katika uongozi. Wandishi wa habari na wachambazi wa masuala ya siasa wamekuwa na kasi kubwa ya kila mara kumkosoa na kumweleza mkuu huyo wa nchi kuwa bado ana safari nzito ya kufanya kazi kutokana na kushindwa kuwasimamia ipasavyo wasaidizi wake.

Kila mara rais ametakiwa kjufanya maamuzi mazito ili kulinusuru taifa na wanyanganyi waovu wasio na uzalendo.

Hao wanaoitwa wakosoaji wa rais mara nyingi wamekuwa wakimlaumu kwa kushindwa kuwa adhibu wasaidizi wake, wanaomwangusha katika utendaji wavivu, wanaofanya kazi kwa mazoea na wala rushwa.



Kutokana na kukosolewa huko, raia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM), wakati mwingine imemsaidia na hata wakati mwingine kufautilia kwa ukaribu shutuma dhidi yake.

Amekuwa akiangalia malalamiko hayo kama yanaenda sambamba na kushindwa kwake kutelekeleza ahadi zilizopo katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005.

Wakosoaji hawa wamegeuka kuwa maadui na pengine wanaweza kuitwa ‘waahini’, hapa ndipo mwandishi Ngungi wa Thiongo, alipoandika juu ya “ An Enemy of the People” maana yake “Adui wa watu” huyu ni yule anayetetea mema, hapo ndipo palipo na ushindi.

Safu hii imetuhumiwa na watu kadhaa kuwa ninaandika vibaya kuhusu rais, ninamkosoa kwa kila jambo, na sioni mema anayoyafanya. Binafsi sidhani kama ni kweli ninamkosoa rais Kikwete, na kama ninamkosoa ni kidogo nan ukosoaji wangu ni kumsaidia ili abadilike, aangalie na kupima kama kweli zinamgusa au la! Na hilo ndilo jukumu lake.

Leo ninaandika makala hii nikiwa nilishaamua kutokuandika katika safu hii, kwa kipindi cha wiki nne zijazo ambazo nitakuwa mapumzikoni, lakini nimelazimika kutokana na kuchokozwa na baadhi ya watu wanaodai kuwa ni makada wa chama na ni marafiki wa Rais.

Sidhani kama kweli ni marafiki wa rais nafikiri ni maadui zake lakini mimi ninawaita ni maadui kwasababu hawamtakii mema, wanapinga asikosolewe na kutumia mlango huo kumchafua. Baada ya makala yangu ya Jumapili iliyopita ya Desemba 13, nilipokea jumbe nyingi kupitia katika simu yangu ya mkononi, moja ambayo imenigusa na kunifanya kuandika leo ni ile iliyosema” Wewe ni mtu wa ajabu sana, kila unapoandika nikiangalia unamkosoa Mhe! Rais tu, hakuna hata siku moja unampongeza kwa kazi zake, wewe huna lolote na ni Kanjanja”, hii ndivyo ilivyokuwa meseji hiyo.

Kwanza ieleweke kuwa jumbe za kunitukana siziogopi maana hizo tumezizoea, ukimtukana mwandishi wa habari makini unajisumbua, mtu huyu aliyeuandika ujumbe huo, aliniandikia zaidi ya meseji 10 kwenye simu yangu Jumapili ya Julai 12, mwaka huu akinituhumu kuwa sina lolote kwababu ninawaandika vibaya kina Andrew Chenge, Rostam Aziz, na wengine, nilimjibu kuwa ametumwa na anaowasemea.

Tukio la kupokea ujumbe huu wa juzi na kundi la watu ambao kwao kila wakiamka wanafikiri tu jinsi ya kumsafisha na kumsifia rais Kikwete, na kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, na kumpamba kwa unafiki ili wailambe miguu yake. Na huko si kumsaidia bali ni mumwangamiza.

Kwanini ninasema hivyo, kiongozi yeyote duniani anaongoza kwa kufuata maoni ya watu, tadhimini za watu au wanaongozwa ndizo zinazomfanya kiongozi ajue kuwa anakubalika au la, kama huwezi kusikiliza maoni ya watu kuhusu wewe huwezi kujirekebisha.

Tunajifunza kutokana na makosa yetu na madhaifu tunayoonyesha na kukosolewa. Ukizuia watu wasiku-jaji, na kukutadhimini umeangamia kiuongozi, rais Kikwete analijua hilo ndiyo maana anakubali, kukosolewa, anatulia, anarekebisha pela anapoweza, pamoja na kuwa anakwamishwa na wasaidizi wake hao.

Mfano mzuri ni Taarifa za Kituo cha Taasisi ya utafiti na elimu ya Demokrasia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Redet) ilivyokuwa awali, Taasisi hii ilikuwa ikitoa ripoti yake inaonyesha wazi wazi kuwa Chama tawala au Rais ameshuka kiwango, wadau wanampa maneno yao anajirekebisha na kweli wakati mwingine akipifanyiwa tadhimini anaonekana kubadilika.

Siku hizi na katika serikali ya awamu ya nne, kumeibuka makundi au vikundi vya watu walioishiwa kiakili, ambao kwa kukosa uwezo wa kufikiri ipasavyo hawajiamini, wanahangaika kutafuta nafasi ya rais kupongezwa kwa kila jambo analolifanya. Kwao kumpinga rais ni dhambi, hawataki kusikia mtu anakosoa au kusema kuwa rais ameshindwa kufanya kitu. Lo! Huyo rais ni Mungu? Je hakosei? Je hasahau? Na kama anakosea si anatakiwa kukosolewa ili ajisahihishe? Hawa wameishiwa kiakili.

Kundi hili linatia aibu na bila shaka haijawahi kutokea katika taifa hili tangu lizaliwe mwaka 1961, watu wanaibuka tu mitaani na kuanza kumpongeza rais kwa kila jambo, wakipinga wanamkosoa rais, binafsi niweza kusema kuwa hili ndilo kundi ambalo linataka kumwangusha Kikwete katika utawala wake linataka ashindwe kujirekebisha ili lipate nafasi ya kuja kumwengua kisawasawa, litakapokuwa tayari.

Kundi hili ni la kifisadi nimekuwa nikilitaja kila mara kuwa lina fedha nyingi na linatumia nguvu hiyo kumdanganya rais Kikwete. Limdekuwa likifadhili vikundi kuandamana na kuunga mkono hoja chafu. Linajua watanzania ni masikini wanashinda ya fedha linawahonga nguo na pombe ili waandamane bila kujua wanaandamania nini. Mwezi Augost 2006, kundi hili lilifadhili watu waliojiita wanaCCM pale mwanza wakaakumua kuipinga filamu ya Darwins Night Mare, iliyokuwa ikionyesha kuwa watu wa Mwanza wanakula ‘mapanki’ Vichwa vya samaki, badala ya minofu, lakini ukweli wakijua kuwa wanakula.Huu ni ujinga.

Cha ajabu na kinachotia aibu, vijana wenzangu wanazuoni wanaojiita kuwa ni shirikisho la wana CCM walioko Vyuo Vikuu waliandamana huko Mbeya siku ya Jumanne wiki hii kwa ajenda ya kuwapinga wote wanaompinga rais na kumkosoa, hili ni kundi lilikosa kazi, na kama kweli ndiyo wasomi wetu basi hawajui heshima ya Digrii wanazozisomea.

Kundi la pili ni la wana-dini wanojiita Baraza la habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita) kwa aibu nalo limefanya maandamano yake jana jumamosi, kupinga watu wanaomkosoa rais na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kushughulikia mafisadi. Haya makundi hayataji kama yanampinga nani, je ni wanahabari wakosoaji, au ni wanasiasa wenzao ndani ya CCM au ni wapinzani?

Makundi haya yanapoteza mwelekeo wa taifa letu wanamdanganya rais kuwa wanaampenda na wanamsaidia kwa kumpongeza kwa kila jambo kuwa wanamwangamiza, wanaomsaidia rais ni wanaomkosoa.

Nawatakia sikukuu njema ya Krismas, na mwaka mpya 2010, mwenyezi Mungu atusaidie ili tufanye vizuri mwakani, tutaonana mwakani Mungu akitujalia.
0784/715 686575

No comments:

Post a Comment