ASKARI wa Jeshi la Magereza nchini wamepinga vikali utaratibu ulioanzishwa na uongozi wa juu wa jeshi hilo kuwakata mishahara na posho zao kwaajili ya kuchangia timu ya Jeshi hilo ya Prisons.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda mrefu umebaini kuwa uongozi wa jeshi hilo, ulitoa waraka kwa wakuu wote wa magereza nchini, na vitengo vyote kuwataarifu juu ya mpango wake wa kutaka kila askari kuanzia wa ngazi za chini mpaka juu kuchangia kiasi cha fedha kwaajili ya kuiwezesha timu hiyo.
Habari hizo ambazo hata hivyo uongozi wa jeshi hilo makao makuu ulisindwa kukanusha licha ya kutokuutolea maelezo kila wakati walipoulizwa na gazeti hili, zinaeleza kuwa tayari askari wameshaanza kukatwa fedha hizo.
Jitihada za kumpata msemaji wa Jeshi hilo, Omar Mtiga ili kuzungumzia suala hilo, zilishindikana baada ya kuambiwa kuwa Mtiga, yupo safari kikazi, na kila lipokuwa akipigiwa simu yake ya mkononi, alikuwa hapokei.
Chanzo cha habari hizi, kilisema kuwa askari walipaswa kuchangia timu hiyo baada ya kubainika kuwa hakuna fedha kabisa za kuiwezesha kujikimu inapokuwa kuwa katika mashindano yake hapa nchini.
“Sisi tunashangaa ni kwanini fedha zikatwe, wakati timu ina vyanzo vyake vya fedha kila mkoa, na kambi zote, askari sisi tunateseka kwa maisha magumu, tunaishi kwenye nyumba za kupanga mitaani huku, tunalipa umeme, maji, na matatizo mengi tu leo unaambiwa uchangie timu”Kilieleza Chanzo chetu hicho.
Taarifa zilizidi kueleza kuwa askari wa mikoani wameanza kukatwa kwenye mishahara yao ya mwezi Desemba, mwaka jana na wataendeela kukatwa pia mishahara ya Juanari Mwaka huu, ila kwa wale wa Dar es salaam, hususani makao Mkuu walikatwa kwenye posho zao za mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana.
Pia ilielezwa kuwa askari wa kikosi maalumu(KM) wa jeshi hilo waligomea kukatwa fedha hizo na kusababisha mgogoro mkubwa mpaka ilipotolewa taarifa kutoka juu kuwa kwa askari wa KM, iwe ni hiari kwa anayependa kuchangia.
Pia kilieza kuwa fedha hizo zinakatwa kulingana na cheo cha askari husika, kuanzia cheo cha chini kabisa cha Wadern mpaka Mkuu wa kambi(RSM), anakatwa sh. 10,000, Mkaguzi Msaidizi(A/INSP), mpaka mkaguzi(INSP) ni sh. 20,000, Mrakimu msaidizi(ASP), mpaka Kamishna msaidizi(ACP), wanapaswa kulipia sh. 30,000.
Aidha, habari hizo zilieleza kuwa askari wengi wameonyesha kukasirishwa na kitendo cha uongozi wa juu wa jeshi kushindwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha, za kufanya shughuli hizo na kuamua kuwakata askari hao, ambao wengi wao wanaishi maisha duni na mishahara midogo isiyowakimu.
“hakuna timu iliyokuwa na miradi mingi hapa nchini kama Prisons, mpaka leo kila gereza kuna shamba la kuchangia timu, huko Songwe, Lindi, Mtwara kuna mabwawa ya chumvi na mashamba ya mbao kwaajili ya timu hiyo leo inalipiwa na askari?”kilisema Chanzo hicho cha habari
Kwa mujibu wa taairfa hizo za ndani ambazo vyanzo hivyo vya habari vinaeleza kuwa Aprili 20, hadi Augosti, 25, mwaka jana, kulikuwa na kozi ya uongozi daraja la kwanza chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya, ambapo askari 698 walitoa sh. 28.,000 kila mmoja, kuichangia timu hiyo, Augosti, 1, waliripoti askari wapya zaidi ya 800, ambao kila mmoja lilipa sh. 56,000 kwaajili ya timu hiyo, hivi sasa kuna wanafunzi 62 wa kozi ya GOS chuo cha Ukonga Dar es salaam, nao wametoa sh. 28,000 kiloa mmoja kama mradi wa timu.
Baada ya kushindikana kupatikana kwa maelezo ya msingi kutoka ndani ya jeshi la magereza kuhusu malalamiko hayo, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, lakini baadaye aliagiza msemaji Mkuu wa Wizara hiyo kulizungumzia suala hilo.
Akizungumza Msemaji Mkuu wa Wizara, Isaac Nantanga, alikiri kuwepo na utaratibu huo ndani ya Jeshi hilo na kusema kuwa jeshi liliamua kufanya hivyo kwa nia ya kuilinda timu hiyo kwa muda huu ambao ipo katika mchakato wa kucheza mechi za kimataifa.
Alisema kuwa kukatwa kwa fedha hizo kulitokana na timu kutokuwa na miradi yake binafsi, pia jeshi hilo halina miradi ya kiuwezesha timu hiyo.
“ mpango huu upo na ni kweli kuwa wanakatwa fedha hizo, utaratibu huo ulitokana na mahitaji makubwa ya kifedha, na serikali haifanyi biashara, kwa hiyo tukaamua askari hao wachangie timu yao, hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuichangia, kwani faida inayopatikana kwa wao kufanya vizuri ni sifa ya jeshi la magereza.
“Menejimenti ilikaa ikaona ili kuipa msukumo na kupata fedha za haraka ni askari waichangie, lakini hili ni zoezi la dharura, tu hivi karibuni litafanyiwa marekebisho au kusimamishwa”alisema Nantanga.
Akijibu swali kuwa kwanini waliamua kutumia nguvu kukata fedha hizo bila ya kuwauliza askari wahusika, Nantanga alisema kuwa ilikuwa vigumu kuwauliza askari mmoja mmoja, na kufuata maoni yao kwani askari ni wengi sana.
“aliongeza kuwa kama yametokea malalamiko hayo, itabidi waangalie namna ya kubadilisha mpango hiyo ili kuondoa kero za malalamiko ya askari hao.
“ ieleweke pia kuwa lengo siyo kuwakomoa askari hao, ilikuwa ni nia njema tu ya kutaka kuiokoa timu hiyo, ili iweze kujikimu, sasa tutajitahidi kuondioa kero hiyo”alisema
Nantanga, alikanusha shutuma zilizotolewa na askari hao, kuwa wamekuwa wakitishiwa mara nyingi na wakubwa kuwa kama watakataa kuchangia timu hiyo, hawatapata mikopo wala kupitishiwa fomu za kwenda kusoma, au kupitishiwa fomu za kuomba mikopo benki mara watakapo hitaji.
“sidhani kama kweli makao makuu wanafikia hali hiyo ya kuwatishia askari wao, kama ndivyo huo sio utaratibu.”alisema.
Hivi karibuni Jeshi hilo limekuwa likikumbwa na kashifa kadhaa ambazo zimepelekea kamishna Mkuu wa magereza Augustino Nanyaro, kuzikanusha tuhuma zote zilizoelekezwa kwake na askari wa chini wa jeshi hilo.
Moja ya tuhuma kubwa ambayo ilielekezwa kwa kamishina Nanyaro, ilikuwa ni ile ya kutumia magari ya jeshi hilo kwa shughuli zake binafsi.
Nanyoro alilalamikiwa kutumia zaidi ya magari matano ya jeshi hilo ambayo yananywesha mafuta ya serikali kutoka bohari kuu Keko.
Gazeti hili lilielezwa na vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya jeshi hilo kuwa magari hayo ni lenye namba za usajiri STK 1000, aina ya Mercedes Benz, STK 1964, Toyota Land Cruiser GX, STK 1026, Land Rover 110, STJ 9515, Nissan Patrol na Land Rover 110, lenye namba T 170 ATH.
Katika mazungumzo na gazeti hili miezi miwili iliyopita , Kamishna Nanyaro alikanusha kuwatumia katika kazi zake binafsi askari hao wa ngazi za chini ikiwemo madai ya kuwafanyisha kazi katika kiwanda chake cha mbao kilichopo Kitunda.
Wakati Kamishna Nanyoro akieleza hayo, baadhi ya askari magereza wamesisitiza kuwa madai anayoyakanusha bosi wao ni ya kweli na kwamba yakichunguzwa vizuri ukweli wake utabainika.
Walisema kamwe hawatishiki na kauli alizozitoa kuwa anakusudia kuitisha gwaride la kuwatambua na mwandishi wa habari anayeripoti habari za sakata hilo ajiandae kukutana naye mahakamani kwa sababu wana uhakika na walichokieleza.
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment