Popular Posts

Friday, September 9, 2011

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Ni Vita ya wazee na vijana
*Wenye umri mkubwa watakiwa kupumzika siasa
*Wazee wagoma, wasema ‘uzee ni hazina’
*Vijana wakerwa kuitwa ‘Vuvuzela’
Na Sauli Giliard
WAKATI ushindani wa kisiasa ukiaminiwa kuwa ni vita ya mtu na mtu au vyama na vyama, hali imebadilika na kuhamia katika umri wa kati ya vijana na wazee.
Wazee wanaopigwa vita na vijana sasa ni wale walioko Bungeni kwa muda mrefu na hawataki kung’atuka ili kupisha mawazo mapya ya vijana kupenyeza katika chombo hicho cha kutunga sheria.
Wabunge walioko majimboni, wengi wao wakionekana wakiwa na umri wa makamo wanawaona vijana wanaotangaza nia ya kuwang’oa majimboni sasa ni wapiga kelele mithili ya tarumbeta zinazotumika katika michuano ya kombe la dunia maarufu kama ‘vuvuzela’.
Akizungumza na Tafakari wiki hii, Katibu Mkuu wa Mtandao wa Dira ya Vijana nchini (TYVA), Deogratius Siale anasema, baada ya kuonekana vijana wanashindwa kuingia katika vyombo vya kufanya na kutekeleza maamuzi, sasa wamekuja na mkakati mpya wa kuhakikisha vyama vinawakubali na kuwasimamisha katika uchaguzi ujao.

Siale ameeleza TYVA itahakikisha inawaunga mkono wale wote waliotangaza nia na kuonekana wanaweza kuongoza kwa manufaa ya kupigania sera zote za kuwainua vijana na wananchi wote kwa ujumla wake.
“Tumeshabainisha kuwasaidia vijana katika kugombea nafasi za udiwani na ubunge. Kwa sasa hatuna mtandao mkubwa sana, tunafanya kazi ndani ya mikoa sita, lakini adhma yetu ni kuhakikisha tunawapa nguvu na hata walioko mbali na mikoa tulipo kwa sasa wapate wasijione wametengwa,” anasema.
Anasema, kitendo cha wanaotangaza nia kufananishwa na ‘mavuvuzela’ ni changamoto na kero kubwa kwao na inadhihirisha ni namna gani walioko kwenye nyadhifa wasivyopenda mabadiliko.
Anabainisha kwa sasa jumuiya hiyo ya vijana inajiandaa kutoa vipaumbele vyao vya uchaguzi Mkuu wa mwaka huu baada ya kuketi katika kikao kitakachokaa Julai 15 na kuzambaza kwa vyama vya siasa.
Katika kile kinachoonekana nafasi za ubunge ni zaidi ya upinzani wa mtu na mtu ama vyama kwa vyama na badala yake ni umri nao unahusika ni hatua iliyofikiwa na baadhi ya watangaza nia kubainisha wanaong’ang’ania ubunge angali wakiwa na miaka 60 na zaidi hawawezi kuwasaidia wananchi.

“Wanaowania uongozi wakiwa na miaka zaidi ya 60 ni vigumu mno kuwaletea wananchi maendeleo. Wanapaswa kutulia nyumbani na kuandika vitabu na kuishauri serikali,” anasema Festo Kaswaga aliyetangaza kugombea jimbo la Ismani, linaloongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wiliam Lukuvi.
Zikiwa zimebaki miezi mitatu kufanyika kw auchaguzi Mkuu hapo Oktoba mwaka huu, tayari kundi kubwa la vijana limeshajitokeza kutangza nia ya kugombea Ubunge huku, wazee wakiendelea kuwabeza.
Vijana wengi wameonekana kusukumwa pia na kauli za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwa ni wakati w akuwawezesha vijana na amedhamiria kuwaingiza katika serikali yake.
Aidha vijana wamesukumwa na kauli mbiu ya Umoja wa Vijana (UVCCM) ya mwkaa huu inayosema “
Hadi sasa Mbunge mkongwe ambaye amejitokeza na kujitetea ni Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Samweli Malecela ambaye amepinga waziwazi kutoona tatizo la wazee katika uongozi na kusema kama wakongwe wana uwezo wa kuishauri serikali “basi wana uwezo wa kuongoza.”
Wakwanza kuibua mjadala wa ukomo wa ubunge alikuwa waziri Mkuu Mizengo Pinda mbaye alishauri kiwe ni kipindi kisichozidi miaka 15, kauli iliyosdababishwa kupingw ana wabunge wenzake.
Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango -Malecela, amepinga pendekezo la Waziri Mkuu kwamba muda wa kuwa Mbunge usizidi miaka 15.
Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM) na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti (CCM) ni miongoni mwa wabunge waliokaa muda mrefu bungeni ambao hivi karibuni walitamka uamuzi wa kung’atuka.
Mbunge wa Mtera, John Malecela na Mbunge wa Njombe Kaskazini, Jackson Makweta (wote wa CCM) pia ni wakongwe ambao hawajaeleza nia ya kuachia nafasi hizo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Wakichangia maoni juu Ya hoja hizo, Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes amesema sema wananchi pekee ndiyo wanaofahamu muda na umri anaostahili mbunge wao kuwatumikia.
Alitoa mfano wa Mbunge wa Njombe Kusini, Anne Makinda, Mzindakaya, Malecela na Kimiti kuwa ni miongoni mwa watu wenye michango endelevu inayotokana na uzoefu wao bungeni.
Mbunge wa Tabora, Siraju Kaboyonga pia alipingana na mapendekezo ya kuweka ukomo na umri kwa wabunge kwa malengo ya kumfanya Mbunge asikae muda mrefu na kusema ni chanzo cha kuyapotezea majimbo maendeleo.
Akitolea mfano wa majimbo ya mkoani Tabora aliyodai yamekuwa yakibadilisha wabunge kila kipindi cha uchaguzi isipokuwa Tabora Mjini, Kaboyonga amesema majimbo yasiyobadilisha mara kwa mara wabunge yana maendeleo tofauti na yanayobadilisha.
Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko (CCM) alikubaliana na Waziri Pinda kwa kusema wabunge wanaokaa muda mrefu wamebaki kufanya kazi kwa mazoea. Mwisho

No comments:

Post a Comment