Mali za ‘swaiba’ wa Lowassa kukamatwa
BANGKOK, Thailand
MAHAKAMA kuu nchini huenda ikaamuru kukamatwa kwa mali za aliyekuwa Waziri Mkuu Thaksin Shinawatra ambazo zenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 2.29 alizipata kwa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Waziri mkuu huyo aliyepinduliwa mwaka 2006 ndiye aliyeiahidi Tanzania kuipatia teknolojia ya kutengeneza mvua baada ya kutembelewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Edward Lowassa ambaye naye aliondoka madarakani baada ya kukumbwa na kashfa ya ufisadi.
Pamoja na sababu ya kuondoka madarakani kwa viongozi hao kufanana, Shinawatra ndiye aliyeanza baada ya kupinduliwa na jeshi ikiwa wiki chache baada ya Lowassa kurejea nchini akiwa na ahadi hiyo.
Lowassa naye alilazimika kujiuzulu mwaka uliofuata baada ya kukumbwa na kashfa ya Richmond, hali iliyomfanya Rais Jakaya Kikwete kulivunja baraza la mawaziri na kuunda jipya.
Jopo la majaji tisa wakisoma huku hiyo, walikubaliana kwa pamoja kuwa,
Thaksin na mkewe wa zamani walimiliki hisa katika kampuni kubwa ya mawasiliano ya Shin Corp ambayo aliiunda akiwa na wadhifa wa waziri mkuu.
Jopo hilo pia lilikubaliana na hoja kwamba aliweza kubadili sera za serikali hususani za usimamiaji wa simu hali iliyoinufaisha kampuni hiyo ya familia ambayo ndiyo iliyokuwa inaongoza kwa utoaji wa huduma hiyo nchini Thailand.
Wataalam hao wa sheria waliamuru kwamba hisa zake alizokuwa anamiliki kisirisiri katika kampuni ya Shin Corp wakati akiutumikiwa wadhifa huo zilisababisha sera za serikali kuinufaisha kampuni, hali iliyoleta mgogoro wa kimaslahi.
Wakati wakisoma maamuzi hayo, nje ya mahakama kulikuwa ulinzi mkali kutokana na hofu ya serikali kuwa, huenda wafuasi wa Shinawatra wakapinga hukumu hiyo kwa kuleta vurugu.
Hata hivyo, kwa maamuzi yoyote yale, hali ya machafuko ya kisiasa inatarajiwa kuibuka.
Mahakama kuu inachunguza kwa makini iwapo kampuni ya mwanasiasa huyo ilikuwa na utajiri wa kutupwa kabla hajaingia katika siasa ama ilikuja kuupata mara baada ya kuupata na kuutumikia kati ya mwaka 2001-2006 alipoondolewa na jeshi.
Ikithibitika, huenda mali hizo za thaani ya dola bilioni 2.29 za familia yake zikakamatwa katika benki zilizopo Thailand.
Taarifa zilizopo ni kwamba utajiri wa Thaksin na baadhi ya ndugu zake wasiojulikana uko salama katika benki za nje ya nchi.
Waziri Mkuu huyo anatumikia kifungo cha miaka miwili jela alikuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo ya kesi hiyo kupitia njia ya vieo ilhali akiwa uhamishoni Dubai baada ya kufanyika maadalizi hayo.
Awali, maamuzi ya kwanza yalimnufaisha mwanasiasa huyo baada ya jopo la majaji kutupilia mbali mashitaka dhidi yake kwa maelezo kuwa hayakuwa halali.
Upande wa utetezi ulishauri kuwa kuwepo tume maalum ya ya kumchunguza Shinawatra pamoja na aliokuwa amewateua ambao walikuja kujihusisha na mapinduzi dhidi yake.
Katika ujumbe uliosikika jana, Thaksin alisiistiza kuwa, amepata fedha hizo kwa “jasho lake, nguvukazi na ubongo wake” na si kwa udanganyifu.
Serikali inayoongozwa na waziri mkuu wa sasa, Abhisit Vejjajiva ilitarajia kwamba hukumu inayotarajiwa itarudisha amani lakini alilitaka jeshi la nchi hiyo kuwa makini dhidi ya wafuasi wa Thaksin Shinawatra waliovalia fulana nyekundu kwani huenda wakaleta vurugu.
“Tunategemea mazuri,” msemaji wa serikali, Panitan Wattanayagorn alisema na kuongeza, "Ni kweli wengi wanahofu kutokea mabaya lakini tuko tayari kukabiliana na lolote lile.”
Katika kesi hiyo, majaji wataangalia iwapo Thaksin alivunja sheria kwa kuchuma mali hizo pamoja na familia yake kwani hakupaswa kumiliki hisa kwenye kampuni akiwa waziri mkuu.
Aidha korti hiyo itaangalia iwapo utawala wake ulitekeleza sera amazo moja kwa moja ziliinufaisha kampuni hiyo ya familia yake, kosa abalo linajulikana kama ‘ufisadi wa sera’.
Wakosoaji wa Thaksin wanatarajia kuona kiongozi huyo akitiwa hatiani kama mchakato wa kuitakasa siasa za Thailand ambazo mwaka 2006 zilitawaliwa na maandamano yakitoa wito wa kupinduliwa kwa kiongozi huyo naliyetuhumiwa pia kutoeshimu katiba ya utawala wa kifalme wa Bhumibol Adulyadej (82).
AP
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
No comments:
Post a Comment