Popular Posts

Saturday, January 16, 2010

Wawezaji Kilimanjaro wazusha migogoro

Na Deogratius Temba

WAWEKEZAJI katika Mashamba ya kulima zao la Kahawa Mkoani Kilimanjaro, wamedaiwa kuwa chanzo cha migogoro kati yao na wananchi wanaowazunguka kutokana na kushindwa kutekeleza masharti ya mikataba walioingia na vyama vya ushirika vya msingi.
Mashamba 41 yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 24,000, mkoani Kilimanjaro yanamilikiwa na vyama vya ushirika vya msingi vilivyokabidhiwa na serikali baada ya kuyataifisha kutoka kwa Wazungu mwaka wa 1971.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, mkoani Kilimanjaro kwa msaada wa asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Gemsat), umebaini kuwa migogoro hiyo imepelekea kuibuka kwa vurugu ambazo zimesababisha uharibifu wa miundombinu na na kuiadhiri kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wa kawaida.

Pia imebainika kuwa chanzo cha migogoro hiyo ni wawekezaji hao kushindwa kufuata taratibu za mkataba na leseni za biashara walizo omba.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, mmoja wa viongozi waandamizi wa mkoa wa Kilimanjaro, ambaye alikataa kutajwa jina lake gazetini alisema baadhi ya vyama vya msingi vimeingia mikataba na wawekezaji wasiokuwa na mitaji ya kutosha kuweza kufufua na kuendeleza zao la Kahawa.
Alisema kutokana na kuwepo kwa rushwa inayotolewa kwa viongozi wa vyama vya ushirika baadhi ya wawekezaji hawalipi kodi ya pango la ardhi, kulingana na mkataba wa uwekezaji.
“Hili suala ni zito, tumefanya uchunguzi, tarayi tumebaini jinsi ambavyo mikata hii haifuati taratibu za uwekezaji, tumepeka taarifa kwa wanaohusika na hivi karibuni mikata hiyo itapitiwa upya,”alisema.
Uchuguzi umebaini pia kuwa wawekezaji wengine wanakodisha mashamba hayo kwa wafanyabishara wengine badala ya wao wenyewe kuyafufua na kupelekea kutumika kulima mahindi, Alizeti na Maharagwe.

Mrajisi wa Mkoa wa kilimanjaro, Kasya Kasya, alikiri kuwepo kwa migogoro hiyo na kusema kuwa tayari ofisi yake inashughulikia migogoro iliyoripotiwa kwake ikiwa ni pamoja na kushauri baadhi ya mikataba ivunjwe na mashamba kurudishwa kwa wamiliki.

“Tulipopata taarifa za migogoro hiyo, tuliunda kamati yakupitia mashamba yote ambayo ilituletea mapendekezo ambapo tumeshauri mikataba yote ya mashamba ipitiwe upya ikiwa ni pamoja na kuivunja ile inayoonekana kuwa na utata.

“Tatizo lingine ni kuwa wajumbe wa vyama vya msingi wanaokaa na kumpitisha mwekezaji hawana uelewa wa mikataba hiyo ambayo imeandaliwa kisheria, ina wapa mwanya mawakili wa wawekezaji kuisaini bila shida,’alisema Kasya.
Kasya alisema mkataba wa Vasso unaonekana kuwa na utata, kwa mujibu wa taarifa alizonazo ofisini kwake, na wameshauri Mwekezaji huyo aagizwe kufuata mkataba na alime kahawa na siyo maua.

Aidha,Mrajisi huyo alikiri kutokuwa na taarifa za mgogoro wa mwekezaji wa Vasso na wananchi na kuahidi kufuatilia kwa katibu tawala wa Wilaya ya Moshi.

“Hili la Mgogoro wa wananchi wa Dakau siku pewa taarifa, lakini nipe muda nimpigie DAS, kwasababu yeye ndiye mtendaji wa Wilaya,”alisema Kasya.

Wakizungumza wananchi wa kata ya Okaoni Wilaya ya Moshi, ambao wamekuwa na mgogoro na mwekezaji wa shamba la Vasso Agriventure, walisema mkataba wa mwekezaji huo umezusha mgogoro kutokana na yeye kukataa kulima kahawa kama alivyotakiwa na kulima maua ambayo yanatumia maji kwa kiasi kikubwa.

“Hapa migogoro haiwezi kuisha bila kuangalia upya mikataba kwani mwekezaji amevunja makubaliano, amelima maua leo hii wananchi wananaza kugombania naye m,aji kwasababu maua yanahitaji maji mengi, alisema mjasiriamali Maris Makoyi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment