KUMEKUWEPO na malalamiko kutoka kwa wananchi na wadu wengi wa sekta ya madini hasa wananchi waishio katika maeneo ya madini ambapo wamekuwa wakidai kuwa hawafaidi chochote katika madini hayo. Kutokana na hayo mwaka huu viongozi wa dini waliungana na kufanya ziara ya pamoja katika migodi yote nchini ambapo waliandika ripoti yao.
Wakati mwingine wananchi wanasozunguka maendeo ya madini wamekuwa wakilalamika kuadhiriwa kiuchumi na kiafya na shughuli za uchimbaji wa madini. Mwandishi Wetu, DEOGRATIUS TEMBA, anatuletea mfululizo wa Ripoti hiyo ya Viongozi wa Dini.
VIONGOZI wa Dini ni watu walioteuliwa na Mungu katika jamii wakiwa na jukumu la kuhubiri amani, utangamano na utii wa Mungu wana wajibu wa kutatua migogoro na kujenga maadili mema na matumaini kwa watu waliokata tamaa ya kushindwa maisha. Wao ni waponyaji wa majereha na waletaji wa matumaini mapya kwa watu na viumbe kwa ujumla.
Hivi karibuni, kumekuwa na mjadala wa kiuchumi na kijamii kuhusu faida inayopatikana kwenye tasnia (sekta) ya madini.
Kutokana na mjadala huo kupokelewa kwa hamasa kubwa hapa nchini, viongozi wa dini walifanya ziara yenye lengo la kuwawezesha kuona, kupata taarifa na kudhibitisha ukweli dhidi ya hisia na maeno ya kutia chumvi yaliyoibuka ndani ya jamii na katika uwanja wa uchumi.
Martin Luther King aliwahi kusema katika hotuba yake Mei 17,mwaka 1956, kuwa “ Kuna hatari kwa mtu anayeamini sana katika mabadiliko kama ilivyo kwa mtu asiye amani kabisa. Mtu anayeamini sana katika mabadiliko husema huna haja ya kufanya lolote kwa sababu(mabadiliko) lazima yatokee. Hivyo hivyo mtu asiyeamini kabisa husema hana haja ya kufanya lolote kwa sababu mabadiliko kamwe hayataweza kutokea haya hivyo tunastahili kuanzisha msimamo wa kiuhalisia,”
Msimamo wa kiuhalisia daima chimbuko lake ni kwa wale wasiopendelea upande wowote, ila husimamia ukweli tu. Kwani ukweli daima huwaweka wafuasi wake huru.
Kwa njia ya kufanikisha ujumbe wetu, tulikutana na viongozi wa serikali, katika ngazi za wilaya hadi kijiji, pamoja na jamii husika. Vile vile tulikutana na watendaji pamoja na wasimamizi wa makampuni ya madini na migodini.
Hivyo basi ripoti hii inajumuisha yale tulioyoshuhudia na kusikia katika maeneo ya madini katika ziara yetu. Pia ina maelezo mafupi ya wenyeji wa maendeo husika kuhusu yale tuliyoshuhudia yakitendeka pale makampuni ya madini yalipoanza shughuli katika migodi hiyo. Kwahiyo ripoti hii inahusisha bila upendeleo taarifa zilizopatikana kuhusu masuala ya haki za binadamu, uharibifu pamoja na fidia ya kujikimu, uhamiasishwaji wa watu na adhari zake.
Ripoti hii inadokeza kuhusu hali ya kiuchumi ambayo ndiyo chimbuko la mjadala mkali uliozuka kuhusu kukosekana kwa mchango wa sekta ya madini katika taifa letu.
Mwisho tumejadili kuhusu kitu gani kifanyike pamoja na hatua za aina gani zichukuliwe ili kurekebisha mambo na kuleta amani na utangamano kwa jamii za maeneo ya migodi na y a le ya karibu.
Ni imani yetu kuwa ripoti yetu hii maalumu inayotokana na ziara ya baadhi ya vuiongozi wawakilishi wa dini ambao ni Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT), Baraza la Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) na Baraza la Maaskofu Katoliki Nchini(TEC), itaeleweka na kupokelewa kama mchango wetu ili tuweze kuleta mabadiliko mazuri katika nchi yetu.
Sehemu ya pili ya ripoti hii tutaangalia ziara wilayani Geita na Tarime, na baadaye tutaangalia Bulyanhulu, Kahama na Nzega, na Mara Kaskazini na kumalizia na Buhemba, ambako maaskofu walipenyeza na kujionea hali ilivyo na baada ya kutoka nje ya migodi walikutana na wananchi na kuuzungumza nao.
Taarifa hii inakirfi na kupongeza kqazi nzuri iliyofanywa na kamati ya Jaji Mark Bomani. Kwa msingi huo kutanabaisha kuwa kazi hii haitolewi kupinga matokeo ya kazi ya Tunme ya Bomani, bali kuongeza nguvu katika kufikia utekeelzaji wa mapendekezo yaliyotolewa. Zaidi ya hayo, ripoti hii inatolewa ili kujazia mapendekezo tunayodhani yanastahili kuzingatiwa toka katika yale tuliyoyaona na kuyasikia.
Itaendelendelea wiki ijayo……..
0784/ 715 686575
Elimu ni kujifunza! Tunajifunza kwa kusoma! Karibu katika Blog hii ili tufundishane na kubadilishana Mawazo
Popular Posts
-
*alikubali kushindwa kwa siasa za Kijamaa *hakujilimbikizia mali Na Deogratius Temba WAKATI taifa linaadhimisha miaka 10 ya kifo cha mwasisi...
-
Na Deogratius Temba KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku hamsini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya ...
-
KAMPALA Uganda Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ARVs, zikitumika sambasamba na dawa mseto aina ya (co-Trimoxazole), ...
-
Na Deogratius Temba. NI takribani miaka mitano tangu ililipo ibuika suala la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyokwapua sh. Bilioni ...
-
*Ilizamishwa ziwani na wakaoloni baadaye ikafufuka *Ina Umri wa miaka 98, mwaka 2013 itavunja rekodi ya dunia Na Deogratius Temba MV Liemba ...
-
Na Deogratius Temba SERIKALI imesema makazi ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mzee Abdul Jumbe, yaliyoko Kigambo...
-
*Ni ajali iliyoweka historia kwa kuua *Bado usalama wa ziwani haujaimarika Na Deogratius Temba MEI 21, mwaka huu taifa limetimiza miaka 14 ...
-
, tutaendanayo mpaka uchaguzi Mkuu 2010 Na Deogratius Temba MWISHONI mwa wiki iliyopita Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi, (CCM), w...
-
TITLE OF THE PROJECT The effect of Water Conflict between Investor of VASSO Estate and Villagers in Kibosho Dakau, Moshi Kilimanjaro JOURNAL...
-
Taasisi ya mafunzo ya Jinsia (GTI) inayomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) inaendelea na mafunzo ya kuwanoa wanaharakati kuanzia ...
kırklareli
ReplyDeletetekirdağ
giresun
adıyaman
manisa
RR3JZ